
Papa kwa uchungu, amewatia moyo Wakristo akisema, ndugu zangu wapendwa kwa hakika hakuna Ukristo usioandamana na mateso. Na alieleza na kukumbusha juu ya Heri” Heri yenu ninyi watu wakiwatukana , wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu juu yangu ,furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni”. Leo hii hilo linatokea mbele ya dunia na viongozi wameshindwa kusitisha uovu huo. Wakristo wanapita katika kipindi kigumu cha njia ya mateso , kama ilivyokuwa kwa Kristo mwenyewe.
Papa alieleza na kukumbuka Madhulumu haya kwa Wakristo, Taifa la Armenia likiwa moja ya Mataifa ambako Wakristo wengi waliipita njia hii ya mateso. Taifa la kwanza kuongokea Ukristo. Papa alieleza na kuwakumbuka pia Wakristo wa Libya, Misri, Iraki wanaochinjwa kama kuku kwa kuitangaza Injili ya Kristo.
Papa amesali ili Bwana leo hii aweze kutufanya sisi sote kusikia ndani ya mwili wake Kanisa, upendo mkuu kwa ajili ya wafia dini wa wakati wetu na pia katika kuwa tayari kufa kifo dini. Na kwamba , hakuna Mkristo mwenye kujua hatima ya maisha yake mbele ya uso huu wa madhulumu. Na hivyo ni vyema kuiomba neema ya Bwana ili kama hili litatokea siku moja , tuwe na ushupavu wa kutoa ushahidi wetu kama wafia dini wengine walivyotuonyesha. Na hasa Wakristo wa Armenia.
Papa Francisko awali alitoa barua kwa Patriaki mpya wa Cicilia ya Armenia, ambayo ni tahafifu mpya kwa ajili ya ushirikiano na Makanisa ya Mashariki, barua ya tarehe 25 Julai 2015. Aidha taarifa za awali zinaeleza, kabla ya Ibada ya Misa , viongozi hawa wawili, walipata nafasi ya kubadilishana zawadi, tukio linalotajwa kuwa ni ishara ya wazi ya umoja wa kikanisa unaoridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko na Mwenye Heri Gregorio Pietro Ghabroyan , Patriaki wa Cecilia ya Armenia. Imetajwa hizi ni hisia wazi na ukweli hai wenye kuhamasishwa na Upendo wa Kikristo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni