Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu
Katoliki (KCCB), Askofu Philip Anyolo, ametangaza rasmi juu ya ujio wa
Papa nchini Kenya kwamba itakuwa mwezi Novemba 2015. Hilo limo katika
barua yake kwa Waamini Wakristo aliyoitoa kwa niaba ya Maaskofu,tarehe 27, Agosti, 2015. Askofu Anyolo kasema, "Baba
Mtakatifu amekubali mwaliko wa Maaskofu wa kuitembelea Kenya mwezi
Novemba 2015.Anyolo Askofu, wa Jimbo la Homabay, pia anasema , ziara ya Papa ni ziara ya kichungaji, na hivyo Kanisa litashirikiana na Serikali ya Kenya, katika maandalizi na ufanikishaji.Askofu Anyolo ameeleza na kuomba sala za waamini na msaada wa kihali kwa ajili ya kufanikisha ziara ya Papa nchini Kenya.
Maaskofu wa Kenya katika ziara yao akitume ya kila baada ya miaka mitano katika Ofisi za Idara ya Curia ya Roma na Kiti Kitakatifu , waliyoifanya hapo 13-17th, Aprili, 2015, walitoa mwaliko kwa Baba Mtakatifu alitembelee taifa la Kenya.
Katika ziara hii ya kwanza kwa Papa Francisco kuzuru bara la Afrika, pia atatembelea Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni