Week Hot newz

Batarokota historia yake kwa ufupi!



Nyimbo hapo juu ni ya kisukuma iliyopitwa na Mama Nyamoko akiwa na Msanii Batarokota.

Mwazirishi wa blogu hii ni Paskal Linda  Mgundu maharufu  Batarokota Pichani kushoto alizaliwa 1974 Kijiji cha Kigamboni katika Hospitali Teule ya Kigamboni Mkoa wa Temeke jijini Dar es salaam. 

Batarokota kabila ni Msukuma kutoka kijiji cha Nyashigwe kilomita 35 kutoka jijini Mwanza kaskazini mwa nchi ya Tanzania.
Batarokota ni mtoto wa kwanza katika familia ya Baba na Mama Beatus Linda iliyopo Nyamhongolo kijijini katika jiji la  Mwanza, yenye watoto saba (7)  kwa majina ni Happy Linda ambae ni marehemu aliyefariki tarehe 9/Mai/2007 maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam(rest in peace sister Happy Linda), Naomi linda, Zakaria Linda (dj zhari),Yohana linda (y brain), Monical linda na Norbert Linda.
Batarokota ana mke na watoto wanne na alifunga ndoa Jumamosi ya tarehe 5/Machi/2011 katika kanisa Katoriki la Mtakatifu Partic la mjini Morogoro,Batarokota alifunga ndoa na Sara Abed Linda.Na kabla ya ndoa alifanikiwa kupata watoto wawili na wawili baada ya kufunga ndoa.
Watoto wanne wa Batarokota wakwanza alizaa na mchumba wake wa kwanza Saula Athony Kapama ambae kwa sasa ni marehemu aliyefariki tarehe 9/Agosti/2005 Sumve Matare kwa ajali ya Treni ya abiria iliyokuwa ikienda Dar essalaam, Saula Kapama alimwachia Batarokota mtoto mmoja jina Ng`wibis Linda ambae alizaliwa Agosti 2000 katika Dispensary ya St Michael  mtoto wa pili wa Batarokota ni Shija Paskal ambae alizaliwa Desemba 2006 katika Hospital ya Bugando jijini Mwanza, Batarokota alizaa mtoto na rafiki wake wa kike Ruti Fidel Kanuti na Mtoto wa tatu wa Batarokota ni mtoto wa kike Makrina Juliana ambae alizawa Novemba/ 2011 mjini Morogoro katika Hospital ya Morogoro amezaa na mke wake Sarah Dile Linda na wanne ni Telezia wa Yesu aliye zaliwa Desemba,2013

. 
ELIMU
Batarokota amesoma shule ya msingi Igoma, nakumaliza shule 1990 na alifanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari 1991 katika shule ya sekondari Buswelu na kufanikiwa kumaliza mwaka 1994, baada kidato cha tano na sita Mweli Sekondari  1997.

Na mwaka 2010 Batarokota akufanikiwa kujiunga na  chuo cha Powercomputer kilichopo jijini Mwanza- Tanzania na kuahitimu masomo kutengeneza computer, tovuti, blogu, grafics, Logo design, video editing and production baada ya kumaliza masomo ya computer Batarokota aliendelea na masomo ya Computer Nchini - Kenya katika chuo cha Moi na kumaliza masomo ya Diploma miaka 3, 2013.

Na picha chini Batarokota akiwa ofisini kwake anakofanyia shunguli za design na kutengeneza matangazo.

BATAROKOTA  AMEFANYA SHOW MAENEO MENGI

Mwaka Novemba/1994 Batarokota alifanya show ya kuwaanga kidato cha nne katika shule ya Buswelu Sekondari na Mgeni rasmi alikuwa Hayati Paulo Bomani.Mwaka.

 Julai/1996 Batarokota alialikwa katika show ya kusaka mrembo wa Kigamboni Miss Kigamboni katika ukumbi wa CCM kivukoni .Katika show alikuwa wamealikwa wasanii Fune with Sanse kiongozi wao J- Mtambo na kundi lake la POSOJU.

Mwaka Agosti/1998 ,Batarokota alikalibishwa na kundi lake la G tha Dunia katika ukumbi wa Liberty Hall jijini Mwanza, siku hiyo walikuwa wanazindua singo ya wimbo wao 'upendo kwa mama' wasanii walio alikwa ni Mr 2, Dr KB, BWV, Makamanda wa Gola, Daz P, na wengine wengi.

Mwaka, 2004 Batarokota akiwa na kungi la G THA Dunia alialikwa pamoja na wasaniii H- Baba, J- Mo, Mr Paulo, Solo Thang, Vick Kamata na BWV. katika kufanya show kubwa iliyo fanyika katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora show hii iliandaliwa na Zizou Entertnment.

Mwaka2004 , 25,Desemba. Batarokota alialikwa yeye pamoja na msanii wa nyimbo za kiasili Mama Nyamoko (Suzana Nyamoko), kwenye show ya kuwaburudisha watu wa Geita siku ya kristimasi katika ukumbi wa Lake View Hotel .

Mwaka 2013,Machi, Batarokota amefanya show aliyo alikwa jijini Nairobi katika ukumbi wa Brokriny uliopo Gethorai 44 onyesho hili lilifadhiriwa na Princess Studio. 


MAISHA  
Kipaji cha Batarokota kilianza kuonekana toka akiwa shule ya msingi Igoma mwaka 1987, Akiwa shuleni alikuwa akicheaza ngoma za asilia kwenye kundi la shule na alikuwa akifundishwa na Mwalimu Matongo ambae nimarehemu na Mwalimu Mayuyu ambae kwa sasa ni mwana kwaya wa Mtakatifu Bakita katika kanisa la Romani Katoriki Igoma.

Wanafunzi ambao Batarokota anakumbuka walio kuwa wanacheza wote ngoma ni Tasi Kosinatantine, Paskal Makaka, Peter Makuke,Frimat Lyimo na wengine wengi.

Tarehe 9/Januari/1998, Batarokota alianziha kundi la mziki wa kurap jijini Mwanza kwa jina G THA Dunia, kundi hili G Tha Dunia lilikuwa ni moto wa kuotea mbali ambalo lilitikisha kanda ya Ziwa na lilikuwa likiundwa na Paskal linda a.k.a Batarokota, Juma Hassani a.k.a Big D na Danny Ngollo a.k.a Ngollo 2. Kundi hili lilifanikiwa kurekodi albamu nchini Kenya ambayo ilikuwa ikiitwa '' ONE DAY'' ambayo ilirekodiwa Agosti/1998 mjini Nairobi, Kenya katika studio ya SYNC SOUND STUDIO chini ya Producer Mahamud Omari a.k.a Mr M O .Album hii ya ''One Day'' ilikuwa imajazwa na nyimbo kumi ambazo ni 'one day' jina la albam, 'upendo kwa mama', 'kiama','ogopa 666' , 'nimzuri tu', 'baby shake', 'wenyewe kwa wenyewe', 'watoto kwanza' , 'total balaa' na 'majonzi'. 

Baada ya kukaa nalo kundi hilo Batarokota aliondoka na kuachana na kundi hili 2004 na kwenda Dermank kwa ajili ya kufundisha ngoma Wadenish.Tarehe15/,februari/2006 Batarokota alirejea kutoka Dermank na kuanzihsa kundi jipya liitwalo Watu wa Gola liliko jijini Mwanza, alianzisha kundi hili akiwa na Juma Hassani a.k.a Big D, Kundi hili Watu wa Gola walifanikiwa kurekodi nyimbo mbili 'Tumerudi' na 'vichwa vya kale' nyimbo hizi zimerekodiwa katika studio ya M.O. Record iliyopo Pasiasi jijini Mwanza chini ya mtayarishaji Q the Don na Dj Zari. 


TUZO  KATIKA SANAA
 Mwaka 2001 tarehe 4/Machi msanii Batarokota akiwa na kundi lake la G THA Dunia,Kundi hili walifanikiwa kupata zawadi ya cheti cha ushindi wa best single rap katika wimbo wa -upendo kwa mama- cheti hicho kilitolewa na Gloryhood Music Award ya jijini Mwanza .

Mwaka 2004,Octoba 22-23, Batarokota alifanikiwakupta cheti cha kuudhulia na kushiriki Music Crossroads Tanzania Workshops jijini Mwanza.

Mwaka 2014 msanii Batarokota alifanikiwa kuingia kwenye tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award 2014 (KTMA 2014) kama nominiss katika kategori ya Wimbo bora wenye Vionjo vya Asili ya Kitanzania na wimbo wa kisukuma uitwao `Kwejaga Nyangisha` 


NYIMBO MPYA AKIWA NJE YA KUNDI 
 Batarokota kwa sasa ana nyimbo saba ambazo amesha kamilliza kwa ajili ya maandalizi ya albamu yake mpya atakayo zindua hivi karibuni yenye nyimbo  sita ambazo ziko tiyari ni 

` hongera mama` na  `amani` nyimbo hizi zimerekodiwa Mwaka 2003 Januari katika studio Mushroom Studio jijini Nairobi Kenya chini ya mtayarishaji Teddy Karanda Harrison na Dj Zari.

Nyimbo vingine ni `Sukurubu` ambayo imerekodiwa Multimedia Studio jijini Mwanza mtayarishaji Alon Mikomangwa wasanii walioshiriki kwenye nyimbo hii ni Ceni na Castro kutoka DRC, Kongo na nyimbo nyingineni `sauti ya haki` na `kwejaga Nyangisha` zimerekodiwa Januari,2012 studio ya Sky Studio iliyopo Kihonda Morogoro watayarishaji Orecy Owden na Julius Chares.

Nyimbo nyingine ni ya kisukuma ihitwayo `irombo rise`iliyo rekodiwa 6/Decemba/2012 katika studio za Sunlight Records Mazimbu road -Kihonda Morogoro mtayarishaji King Maroh.

KUINGIA KATIKA SIASA 
Msanii Batarokota ameingia rasimi katika siasa tarehe
18/08/2015 katika chama cha ATC-Wazalendo na kupata kadi namba 223643 alikabidhiwa kadi na Afisa wa Chama mkoani Morogoro Mjini-Tanzania

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni