Week Hot newz

China na Marekani zaafiki vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini



Leo Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia majaribio silaha za nyuklia na makombora hivi majuzi.
Msemaji wa ikulu ya White House amesema Marekani na jamii ya kimataifa hawatavumilia “shughuli haramu za nyuklia” zinazotekelezwa na Korea Kaskazini.
Awali, ikulu ya White House iliishutumu Korea Kaskazini ikisema inawatumia raia wa Marekani kama rahani katika juhudi za kuendeleza ajenda yake ya kisiasa.

Bw Otto Warmbier, mwenye umri wa miaka 21, alikiri kuiba bango la kisiasa katika hoteli alimokuwa akikaa pamoja na kundi jingine la watalii mjini Pyongyang.
Marekani imeitaka Korea Kaskazini kumwachilia huru mwanafunzi huyo mara moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni