Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ib...
Braeking News: Al shaabab walimezima shambulizi la kuvizia la Marekani leo
Wenyeji wa eneo hilo wanasema waliamshwa na milio ya risasi na ndege za kivita zikitua na kuondoka
Wapiganaji wa kundi
la wanamgambo la Al shaabab walimezima shambulizi la kuvizia
lililotekelezwa na makomando wa jeshi la Marekani usiku wa kuamkia leo.
Kwa
mujibu wa Afisa mmoja wa ngazi ya juu jeshini ambaye hakutaka jina lake
litajwe anasema kuwa shambulizi hilo lililotekelezwa na vikosi vya
usalama la Marekani kwa ushirikiano na majeshi ya Somalia yalifanikishwa
kwa kuruka kwa ndege za helikopta kwa kambi ya wapiganaji hao iliyoko
Awdhegle, takriban kilomita 50 Kusini mwa Somalia.
Afisa huyo amethibitisha kuwa Makomando hao wa Marekani walihusika katika uvamizi huo.
Awali
kundi la wanamgambo hao lilikuwa limesema kuwa lilizima shambulizi la
kuvizia lililotekelezwa katika mojawepo ya kambi zao kwa njia ya
helikopta.
Msemaji wa kundi hilo Sheikh Abdiasis Abu Musab
aliiambia Reuters kuwa walimpoteza mpiganaji mmoja katika shambulizi
hilo la usiku wa leo.Wenyeji wa eneo hilo wanasema waliamshwa na milio ya risasi na ndege za kivita zikitua na kuondoka.
Shambulizi hili limetokea siku moja tu baada ya ndege isiyokuwa
na rubani ya Marekani kushambulia kambi moja ya Al shaabab na kuuwa
wapiganaji 150.
Alshabab ilipinga idadi hiyo ya wapiganaji ikisema kuwa nambari hizo zimeongezwa chumvi.
Sheikh Abdiasis Abu Musab amenukuliwa akisema kuwa hawakujua ni jeshi lipi lililotekeleza shambulizi hilo ila waliwazima. ''hatujui ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo''''ndege
hizo za helikopta zilitua kwenye mto Shabelle na makomando wakaanza
kuvizia kambi yetu, hata hivyo tuliweza kuizima ila tulimpoteza mmoja
wetu''
''Walikuwa wamebeba roketi na bunduki za M16 mojawepo ya bunduki maarufu sana na jeshi la Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni