Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ib...
Usajili 2016/17: Mambo muhimu yaliyotokea sokoni Uingereza
Klabu za Ligi ya
Premia zilitumia zaidi ya £155m siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji
kipindi cha majira ya joto na kufikisha jumla ya pesa zilizotumiwa hadi
rekodi mpya ya £1.165bn.Klabu zilikuwa tayari zimetumia jumla
ya£1.005bn kufikia saa nne mchana Jumatano saa za Afrika Mashariki na
kuvunja rekodi ya mwaka jana ya £870m.
Klabu 13 za ligi hiyo kuu ya England zilivunja rekodi zao sokoni. Hapa chini ni mchoro unaoonesha matumzii ya fedha kwa klabu za Ligi ya Premia kwa miaka 10 iliyopita, Majira ya Joto.
Mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi ni Paul Pogba
Paul Pogba Amerejea Manchester United
£89m
Pesa ambazo Man Utd wamelipa kumnunua Pogba kutoka Juventus
£1.5m Pesa ambazo Man Utd walimuuza Pogba kwa Juventus 2012
£61.9m Faida ambayo Juventus wamepata
Hapa chini ni orodha ya wachezaji walionunuliwa ghali zaidi na kalbu za Ligi ya Premia msimu wa 2016-17:
Klabu zajitanua kutumia pesa
Klabu zilizovunja rekodi zao binafsi katika ununuzi
Manchester United: Paul Pogba (£89m)
Bournemouth: Jordon Ibe (£15m)
Liverpool: Sadio Mane (£36m)
Sunderland: Didier N'Dong (£13.6m)
Crystal Palace: Christian Benteke (£32m)
Hull: Ryan Mason (£13m)
West Ham: Andre Ayew (£20.5m)
West Brom: Nacer Chadli (£13m)
Leicester: Islam Slimani (£29m)
Watford: Roberto Pereyra (£13m)
Southampton: Sofiane Boufal (£16m)
Burnley: Jeff Hendrick (£10.5m)
Swansea: Borja Baston (£15.5m)
Klabu mbili za Manchester, City na United, zilitumia zaidi ya £150m.
Meneja mpya wa Manchester United, Jose Mourinho, alimnunua Paul Pogba kwa rekodi ya dunia £89m.
Pia walimnunua kiungo wa kati kutoka Armenia Henrikh Mkhitaryanna beki wa Ivory Coast Eric Bailly, wawili hao kwa £30m.
City,
chini ya Pep Guardiola, walinunua kiungo wa kati Leroy Sane kutoka
Schalke kwa £37m kisha wakalipa Everton £47.5m kumchukua beki John
Stones.
Chelsea na mmiliki wao Roman Abramovich, walimpa meneja mpya Antonio Conte nguvu mpya za kutumia pesa.
Alitumia
£120m, ikiwa ni pamoja na £34m kumrejesha beki Mbrazil David Luiz
kutoka Paris St-Germain na £33m kumpata mshambuliaji Mbelgiji Michy
Batshuayi kutoka Marseille.
Waliotawala mitandao ya kijamii
Ni mchezaji yupi aliyezungumziwa sana mitandao ya kijamii?
Ilikuwa ni difenda Mbrazil David Luiz aliyerejea Chelsea kutoka Paris St-Germain.
Kulikuwa
na ujumbe 330,000 katika Twitter kumhusu, akifuatiwa na Jack Wilshere
wa Arsenal, aliyetumwa kwa mkopo Bournemouth. Kulikuwa na ujumbe 108,000
kwenye Twitter kuhusu kiungo huyo wa kati.
Kipa wa Manchester
City Joe Hart, aliyeenda Torino kwa mkopo, saini mpya wa Tottenham
Moussa Sissoko na Samir Nasri wa Arsenal, aliyetumwa Sevilla, ndio
wachezaji wengine waliozungumziwa sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni