Week Hot newz

Batarokota: Nilimpenda Hayati 2-Pac nikiwa na miaka 16


MOROGORO,Tanzania
NYOTA wa muziki wa Bongo fleva na Mziki wa Asili ya Kitanzania nchini Tanzania,Batarokota, amesema alianza kumpenda sana msanii wa rap wa nchini Marekani Hayati 2-Pac tangu alipokuwa na miaka 16.
Batarokota ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 42, amedai kuwa alianza kununua kanda za Hayati 2-Pac akiwa shule ya msingi  na alipenda sana kusikiliza nyimbo zake ikiwemo Dear Mama karibu miaka ya nyuma na kuimba nyimbo za Hayati 2 pac katika maonyesho mbalimbali.
“Nilianza kuvutiwa na Hayati 2 Pac na Snoopy  nikiwa na miaka 16, lakini sikuonyesha chochote mbele ya wazazi na rafiki zangu.
“Baada ya Hayati 2 Pac kufariki hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na mziki wa rap hip hop naona nguvu zimeniishia sana,” alieleza Batarokota.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni