Week Hot newz

Roho yenye udadisi mwingi huwa na mwelekeo wa kujitenga na Mungu- Papa .



(Vatican Radio) Roho ya udadisi mwingi, huzaa hali kutatanikiwa na ghasia na fujo ya kujiweka mbali na Roho wa hekima , ambaye huleta amani, alieleza Papa Francis katika homilia yake wakati wa Misa Alhamisi asubuhi katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta .

Papa alitoa homilia yake kwa kutafakari masomo ya siku , ambamo somo la kwanza, lilieleza, hali ya kiroho kwa mwanamme na mwanamke, Wakristo wa kweli , wanaoishi katika hekima ya Roho Mtakatifu. Na hekima hii inayowafanya wasonge mbele kwa busara , utakatifu na dhamira safi.

Tafakari ya neno la Mungu, Jumapili ya 33 ya Kipindi cha Mwaka C wa Kanisa

Tunaendelea kama kawaida katika kipindi chetu, tafakari masomo Dominika, na leo tunatafakari masomo Dominika ya 33 ya mwaka C wa Kanisa.

Tayari tunaelekea kumaliza mwaka wa Kanisa, yaani tukiijongea Dominika ijayo iliyo Dominika ya mwisho ambapo tutasherehekea Sikukuu ya Yesu Kristo Mfalme wa ulimwengu. Masomo yote matatu yanachukua sehemu ya tafakari juu ya mwisho wa dunia, ambayo hasa ndiyo tabia ya Dominika zote za mwisho wa mwaka wa Kanisa. Tabia hii kwa kifupi twaiona katika somo la pili ambapo inaonekana katika jumuiya ya kwanza ya kikristu na hasa kati ya Wakristo wa Thesalonike watu walianza kuacha kufanya kazi wakitarajia ujio wa pili wa Bwana kuwa karibu.

Katika hilo Mtakatifu Paulo anawaonya akiwaambia yakuwa yampasa kila mmoja kufanya kazi, uvivu unaojilaza katika subira ya ujio wa Bwana haukubariki. Katika hili tunaweza kuona pia thamani ya kazi katika maisha ya mwanadamu. Kazi iwayo yote iwe ya mikono au ya kiakili au ya kiroho ni ya maana mbele ya Mungu, aliyesema mkaitiishe nchi.

Mpendwa msikilizaji, kama nilivyokwisha dokeza yakuwa masomo yetu, yatupa hali itakavyokuwa wakati wa mapambazuko ya uzima wa milele, tunakutana na hali hiyo katika lugha inayotisha na pengine yaweza kumfanya mtu aogope, na hasa katika ile hali ya kutarajia maneno ya faraja na huruma. Hata hivyo hali hii ya kutisha ina maana yake na baadaye itawekwa sawa na Mungu mwenyewe. Tunajua hilo kwa sababu kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu hata kama ni zito na kali lakini huwekewa mafuta na kugeuka kuwa Neno na tangazo la matumaini kwa mpokeaji aliyeshiba imani!

Mpendwa msikilizaji, kwa sababu hiyo basi yafaa kutenganisha kati ya maneno au lugha itumikayo na ujumbe ambao Mungu apenda kutupatia. Lugha inayojitokeza katika masomo ya Dominika za mwisho za mwaka ni lugha ya kiufunuo, lugha ambayo tunakutana nayo daima katika kitabu cha Ufunuo. Ni wa namna hiyo basi kila mmoja wetu awe makini katika kupembua ujumbe wa Neno la Mungu, asije akaangukia katika shimo la upotoshaji wa Habari Njema.

Mpendwa msikilizaji, tunasema hili kwa sababu ulimwengu wa leo ambao umejaa fitina, ujangili pamoja na ughaidi unaweza kumfanya mtu badala ya kujenga matumaini na kusonga mbele katika kutafuta amani, basi akaona hakuna haja kwa maana ni mikasa tu ndiyo inayotuzunguka! Kuna baadhi ya wenzetu ambao pasipo kutafakari na kuchekesha vema huibuka na mahubiri vitisho kuhusu mwisho wa dunia na huwajengea watu imani ogopeshi ambayo haizaliwi toka upendo wa Kristu msalabani bali katika vionjo vya watu, imani inayosisitiza hukumu badala ya upendo wa Mungu kwa wanadamu.

Mpendwa mwana wa Mungu, tazama upendo wa Mungu pale msalabani, u-wazi anapomwambia yule mwizi tangu leo utakuwa pamoja nami mbinguni! Bwana hapendi tumwogope bali tumpende, kwa maana hakuna atakayepatilizwa kumbuka anasema “walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu! Inatosha tu pasipo kuogopa kusubiri na katika subira hiyo basi tutaziponyesha nafsi zetu. Upendo wa Mungu haurudi nyuma, jicho alilomtazama Zakayo ndilo hilohilo jicho la milele ambalo atatutazama nasi katika nyakati za mwisho na sasa. Katika hii basi Mungu anatudai kutumaini daima kama ambavyo yeye ni tumaini la kweli.

Kwa nini jambo hili? Jambo hili linakuja katika tafakari kwa maana katika maisha yetu kuna kishawishi kikubwa cha kuacha njia ya Bwana, njia nyembamba, njia ya maisha na kufuata njia pana, njia ya kupoteza, njia ya kifo wakati wa taabu na shida katika maisha yetu ya kila siku. Kumbukeni daima njia ya wokovu ni ndefu, ni siri ya Mungu ambayo hufunuliwa kwa kila mmoja wetu katika tumaini la kweli. Ndiyo kusema nabii Malaki anasema kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia lenye kuponya katika mbawa zake. Kumbe siri ya Mungu tunaigundua katika kulicha jina lake na kutumaini wokovu pasipo kusita.

Mpendwa mwana wa Mungu, wanaolicha jina la Mungu ni wale ambao kila siku ya maisha yao hutekeleza nyajibu zao katika familia na mahali pa kazi kwa upendo usiodai faida bali unaolala na kujisimika katika matumaini na upole wa moyo. Katika kujenga tumaini basi ni rahisi yatakapojitokeza matukio ya kutisha tunayoyasikia katika Injili, mwamini kusima na kusonga mbele katika subira pasipo woga na kulicha jina la Bwana.

Hili lina maana ya kwamba tusihangaike kutafuta namna ya ajabu ya kuishi ukristu wetu bali namna ya kawaida iliyojaa mapendo thamini kwa ndugu na jirani kama alivyofanya Msamaria mwema. Tukitenda kile cha kawaida kama Mtakatifu Thereza wa Mtoto Yesu, basi tutakuwa na uhakika wa kujipatia njia nyembamba hata katika mateso tunayokumbana nayo kila siku ya maisha yetu.

Basi mpendwa, tunapoelekea kufunga mwaka wa Kanisa tunaalikwa kuwa na kitu cha kuweka mbele ya Mungu kama tiketi yetu ya kuonana naye, na hivi basi usisahau kabisa yakwamba tumaini lako na imani yako tendaji inayojenga familia ya Mungu ndizo tiketi mwafaka kwa ajili ya sherehe hiyo.

Mpendwa msikilizaji, Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake ya Kitume Mwanga wa Imani , anatufundisha kuwa mwanga wa imani unadai kuwekwa katika huduma ya sheria ya haki, na amani, mwanga huo unakuwa ni uwezo unaoongeza nguvu katika mahusiano ya binadamu, na katika kuboresha maisha ya pamoja na mshikamano wa kijamii. Imani inafanya sisi kufahamu usanifu wa mahusiano kati ya binadamu kwa sababu imani huzingatia msingi ya adilifu katika muono wa sheria za Mungu. Na hivyo imani inakuwa huduma kwa manufaa ya wote.


Mpendwa, imani ni zawadi ambayo inadai kutunzwa pia ili isipotee na haipaswi pia kutunzwa tu katika moyo wetu bali lazima ijitokeze nje ili kuweza kushirikisha wengine tumaini la kweli na upendo wa Mungu kwa ajili ya wote. Imani huimarisha wengine na hivi tukaweza sote kuwa tayari kuisubiria siku ya mwisho kwa furaha.

Nikutakie furaha na tumaini la kweli katika Mungu Mkuu, mpaji wa mapaji na zawadi zote za mbinguni. Tumsifu Yesu Kristo.
Tafakari hii imeletwa kwako na Pd Richard Tiganya, C.PP.S.

St. Albert the Great

St. Albert the Great
St. Albert the Great
Feastday: November 15
Patron of Scientists

Albert the Great was one of the Church's greatest intellects. He studied at the University of Padua and later taught at Hildesheim, Freiburg-im-Breisgau, Regensburg, and Strasbourg. He then taught at the University of Paris, where he received his doctorate in 1245. He was among the first and greatest of the natural scientists, gaining a reputation for expertise in biology, chemistry, physics, astronomy, geography, metaphysics, and mathematics. He was also very learned in biblical studies and theology.

Daily Reading for Friday, November 15th, 2013


Reading 1, Wisdom 13:1-9

1 Yes, naturally stupid are all who are unaware of God, and who, from good things seen, have not been able to discover Him-who-is, or, by studying the works, have not recognised the Artificer.
2 Fire, however, or wind, or the swift air, the sphere of the stars, impetuous water, heaven's lamps, are what they have held to be the gods who govern the world.
3 If, charmed by their beauty, they have taken these for gods, let them know how much the Master of these excels them, since he was the very source of beauty that created them.
4 And if they have been impressed by their power and energy, let them deduce from these how much mightier is he that has formed them,
5 since through the grandeur and beauty of the creatures we may, by analogy, contemplate their Author.
6 Small blame, however, attaches to them, for perhaps they go astray only in their search for God and their eagerness to find him;
7 familiar with his works, they investigate them and fall victim to appearances, seeing so much beauty.
8 But even so, they have no excuse:
9 if they are capable of acquiring enough knowledge to be able to investigate the world, how have they been so slow to find its Master?

Responsorial Psalm, Psalms 19:2-3, 4-5

2 day discourses of it to day, night to night hands on the knowledge.
3 No utterance at all, no speech, not a sound to be heard,
4 but from the entire earth the design stands out, this message reaches the whole world. High above, he pitched a tent for the sun,
5 who comes forth from his pavilion like a bridegroom, delights like a champion in the course to be run.

Gospel, Luke 17:26-37

26 'As it was in Noah's day, so will it also be in the days of the Son of man.
27 People were eating and drinking, marrying wives and husbands, right up to the day Noah went into the ark, and the Flood came and destroyed them all.
28 It will be the same as it was in Lot's day: people were eating and drinking, buying and selling, planting and building,
29 but the day Lot left Sodom, it rained fire and brimstone from heaven and it destroyed them all.
30 It will be the same when the day comes for the Son of man to be revealed.
31 'When that Day comes, no one on the housetop, with his possessions in the house, must come down to collect them, nor must anyone in the fields turn back.
32 Remember Lot's wife.
33 Anyone who tries to preserve his life will lose it; and anyone who loses it will keep it safe.
34 I tell you, on that night, when two are in one bed, one will be taken, the other left;
35 when two women are grinding corn together, one will be taken, the other left.'
36
37 The disciples spoke up and asked, 'Where, Lord?' He said, 'Where the body is, there too will the vultures gather.'

Meno ya tembo: Maafisa TRA na Bandari mbaroni...


Meno ya tembo yaliyokamatwa
POLISI nchini Tanzania wamesema shehena ya meno ya tembo yaliyokamatwa katika bandari ya Zanzibar ni sawa na tembo mia tatu na watano, yakiwa na thamani ya karibu shilingini bilioni nane, sawa na karibu dola milioni tano za Kimarekani.
Watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na meno hayo, huku maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, na mmoja wa Mamlaka ya Bandari pia wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Maaskofu Ufilipino, wametoa wito wa Novena.


Maaskofu Katoliki wa Ufilipino, wametoa wito wa Novena, sala na fadhila, kwa waathirika na familia zilizopigwa vikali na maafa ya kimbunga kilichopita hivi karibuni na kuua mamia ya watu na kuharibu mali nyingi, zikiwemo nyumba. 


Mosinyori Pedro Quitorio , Mkurugenzi wa vyombo vya habari katika Baraza la Maaskofu Katoliki ya Philippines , alisema fedha zitakazo tolewa wakati wa kipindi cha Novena , iliyoanza Jumanne 12 na

Kwaheriii Dk. Sengondo Mvungi







Papa atembelea Ikulu ya Italia - "Quirinale"

Baba Mtakatifu Francisko Alhamis hii 14.11.2014 majira ya saa nne, kwa mara ya kwanza tangu kuwa Papa mwezi March mwaka huu, alifanya ziara rasmi, kumtembelea Rais wa Italia, Mheshimiwa Giorgio Napolitano, aliyekuwa akimsubiri katika jengo la Ikulu la Qiurinale. Papa amefanya ziara hii Ikulu kama kulipa fadhila kwa Rais Giorgio ambaye alimtembelea Papa June 8, mwaka huu. Papa Francisko ametembelea makazi haya ya Rais wa Italia, ya Quirinale, ambayo awali yalikuwa ni makazi ya Papa kwa karne nyingi hadi 1870.


Baada ya ukimya wa miaka mingi, ziara za Papa kutembelea Quirinale, zilianzishwa mwaka1939 na Papa Pius X11 alipomtembea Mfalme wa Italy Emmanuel 11 aliyekuwa akiishi katika jengo hilo. Na Mapapa waliofuatia wakaiga pia utamaduni huu wa kutembelea Ikulu wa Italia kama ishara ya mahusiano mazuri.

البابا فرنسيس يقدم عبر المجلس البابوي "قلب واحد" مساعدة أولية لضحايا الإعصار في الفيليبين




صدر بيان عن المجلس البابوي قلب واحد (كور أونوم) جاء فيه أنه وعلى أثر إعصار "هايان" الذي ضرب الفيليبين نهاية الأسبوع الفائت مسببا مقتل أكثر من عشرة آلاف شخص، قرر قداسة البابا فرنسيس ـ من خلال المجلس الحبري "قلب واحد" ـ إرسال مساعدة أولية بقيمة مائة وخمسين ألف دولار لإغاثة السكان. وأشار البيان إلى أن هذا المبلغ المالي الذي سيتم توزيعه من خلال الكنيسة المحلية على المناطق الأشد تضررا من الكارثة الطبيعية، سيُستخدم من أجل دعم أعمال إغاثة النازحين والمتضررين من الفيضانات كما ويشكل علامة ملموسة عن قرب الحبر الأعظم الروحي من كل الأشخاص والمناطق المتضررة من الفيضانات.
إلى ذلك عبّر رئيس أساقفة مانيلا عاصمة الفيليبين الكاردينال لويس أنطونيو تاغل عن تضامنه مع الأمة كلها شاكرا المؤمنين في الرعايا على مساعدتهم السخية. وفي السياق نفسه، قدم مجلس أساقفة إيطاليا الكاثوليك مساعدة مالية بقيمة ثلاثة ملايين يورو تضامنا مع ضحايا الإعصار. هذا وتجدر الإشارة إلى أن البابا فرنسيس ـ وبعد صلاة التبشير الملائكي أمس الأحد ـ قد عبر عن قربه من شعب الفيليبين والمنطقة بأسرها على أثر الإعصار الذي ضربها، وحث الجميع على رفع الصلاة وتقديم المساعدة الملموسة.

St. Frances Xavier Cabrini

St. Frances Xavier Cabrini November 13
Patron of immigrants
Died: 1917

St. Frances Xavier Cabrini, Virgin (Feast day November 13) St. Frances was born in Lombardi, Italy in 1850, one of thirteen children. At eighteen, she desired to become a Nun, but poor health stood in her way. She helped her parents until their death, and then worked on a farm with her brothers and sisters.
One day a priest asked her to teach in a girls' school and she stayed for six years. At the request of her Bishop, she founded the Missionary Sisters of the Sacred Heart to care for poor children in schools and hospitals. Then at the urging of Pope Leo XIII she came to the United States with six nuns in 1889 to work among the Italian immigrants.

Daily Reading for Wednesday, November 13th, 2013

Reading 1, Wisdom 6:2-11

2 hear this, you who govern great populations, taking pride in your hosts of subject nations!
3 For sovereignty is given to you by the Lord and power by the Most High, who will himself probe your acts and scrutinise your intentions.
4 If therefore, as servants of his kingdom, you have not ruled justly nor observed the law, nor followed the will of God,
5 he will fall on you swiftly and terribly. On the highly placed a ruthless judgement falls;
6 the lowly are pardoned, out of pity, but the mighty will be mightily tormented.

Kanisa, Majimbo, Parokia,jumuia na watu binafsi waanza kuchangia wananchi wa Ufilippini


BABA  Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko na majonzi makuu taarifa za mahangaiko ya wananchi wengi wa Ufilippini kutokana na kukumbwa na tufani ambayo imesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.
Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuchangia kwa hali na mali juhudi za kuokoa maisha ya mamillioni ya watu waliofikwa na janga hili kutokana na kukumbwa na tufani cha Haiyan kilichotokea nchini Ufilippini, hivi karibuni. Kutokana na mwaliko huu wa Baba Mtakatifu, Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki, Majimbo, Parokia na watu binafsi kutoka sehemu mbali mbali za dunia wameanza kuchangia juhudi za kuokoa maisha ya watu walioathirika na tufani.

Maungamo ni ubatizo wa pili katika utakaso wa dhambi

JANA Jumatano , Papa Francisko amewataka waumini wote kujenga tabia ya kuugama dhambi kwa unyenyekevu na kuomba msamaha kwa Mungu , kila mara wanapotenda dhambi, ili kupata neema za utulivu wa moyo na furaha.
Wito huu ni sehemu ya ujumbe wa Papa kwa waumini, ambao ameutoa kupitia Katekesi yake ya Jumatano, kwa mahujaji na wageni , waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Alisema kama ilivyo katika ubatizo ambamo dhambi ya asili na dhambi zingine hutakatifushwa,

Papa achangia dolla 150, 000 kwa wahanga wa maafa nchini Ufilippini

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuguswa na mahangaiko pamoja na mateso ya wananchi wa Ufilippini waliokumbwa na maafa ya kimbunga cha Hayain hasa katika visiwa vya Leyte na Samar na kusababisha zaidi ya watu elfu kumi kupoteza maisha, ametoa kiasi cha dola za Kimarekani, 150, 000, kama awamu ya kwanza ya mchango wake kwa waathirika wa maafa haya.

Mchango huu umetolewa na Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki Cor Unum. Fedha hizi zitatolewa kwa Kanisa mahalia, ili kusaidia watu walioathirika kwa mafuriko. Hiki ni kielelezo cha imani tendaji, kama njia ya kuonesha uwepo wake wa karibu kwa watu wananchi waliokumbwa na maafa.



Papa ahimiza, tujikabidhi katika Mkono wa Mungu aliyetuumba

Sote ni lazima tutaipita njia ya kifo. Na ni muhimu kutambua kwamba, katika maisha haya kuna njia mbili, moja ni njia inayongoonzwa na shetani na njia nyingine ni ile inayo elekea kwa Mungu. Baba Mtakatifu Francisko ameeleza katika homilia yake, wakati wa Ibada ya misa mapema Asubuhi, Jumanne hii katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta la hapa Vatican

Pope Francis Embraces a Modern Leper and the World is Drawn to its Knees

  
May this beautiful action of love by Pope Francis, a new Francis, draw the whole world back to God.

VATICAN CITY (Catholic Online) - On Wednesday, November 6, 2013, Pope Francis traveled through the crowd of the faithful gathered in St Peters square to hear his weekly catechesis. This is a tradition of the modern popes. Each, in their own manner and style, teach the Christian faithful on an aspect of living the Christian life.

The whole world paused in the face of an authentic witness of God's love and Mercy on Wednesday.  The gates of hell were rattled. We all beheld the very heart of the Gospel of Jesus Christ spoken in a language much more powerful than words.

Salamu za pole kufatia kifo cha Kardinali Domenico Bartollucci

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani Amani

Shukrani,
Paskal linda | mtumishilinda@gmail.com

Kumbuka: Barua pepe hii ilitumwa kupitia kifaa cha Fomu ya Anwani kwenye http://paskal-linda.blogspot.com

BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIIDIMIWE AMINA

Shukrani,
julie smith | ju2004lie2004@yahoo.com
Rest in Peace

Shukrani,
Life Giving Church | lifelivingchurch@gmail.com

Maaskofu wanaangalia vyombo vya mawasiliano ya jamii


Uinjilishaji wa roho za watu Barani Ulaya ni mada ambayo imeongoza mkutano wa siku tatu wa Maaskofu wenye dhamana na vyombo vya mawasiliano ya jamii kutoka Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Ulaya, (CCEE). Maaskofu wameangalia kwa kina na mapana changamoto na vyombo vilivyopo vinavyoweza kutumika kwa ajili ya kutangaza Habari Njema ya Wokovu kwa Makanisa Barani Ulaya, eneo ambalo linaendelea kupokea idadi kubwa ya watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Tanzia: Kardinali Domenico amefariki dunia

TUNASIKITIKA kutangaza kifo cha Kardinali Domenico Bartollucci kilichotokea leo Asubuhi Jumatatu hii 11. 11 2013. Kardinali amefikwa na mauti akiwa na umri wa miaka 96.
Kwa kifo chake, Idadi ya Makardinali imebaki 200, ambamo kati yao wenye haki ya kikatiba kupiga kura ni 109 na wasiokuwa na haki ya kupiga kura ni 91.
Marehemu kwa muda wa miaka mingi alikuwa ni Mkurugenzi wa Muziki Mtakatifu wa Kipapa katika kanisa ldo la Sistini ndani ya Vatican. Alifanywa kuwa Kardinali na Papa Benedikto XV1, wakati wa kikao cha Makardinali "Consistory" tarehe 20 Novemba 2010.

Sera za utoaji mimba ni kutaka kupandikiza majanga kwa Jamii!

Baraza la Maaskofu Katoliki Angola, Sao Tome na Principe linasema, sera za utoaji mimba ni mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, ni kinyume cha Amri za Mungu; utamaduni na utambulisho wa wananchi wa Angola. Wananchi wanakumbushwa kwamba, maisha ya