
Karibuni ndugu msikilizaji wa Radio Vatican katika kipindi cha Liturujia ya Neno la Mungu, tukiwa tayari Dominika VI ya Kipindi cha Pasaka, ambamo tunasikia na kuona Bwana mfufuka akihaidi zawadi ya Roho Mtakatifu.


Mpendwa mwana wa Mungu, katika somo la kwanza (Mdo, 8: 5-8, 14-17) tunakutana na Filipo ambaye yuko mji wa Samaria akihubiri habari njema huko. Katika mahubiri yake hayo au tuseme kazi zake za kichungaji atatenda ishara nyingi na mojawapo ya ishara hizi ni watu kunasuliwa toka pepo wachafu, waliopooza kuponywa na ishara nyingine kama hizo zilengazo kuleta uhuru katika maisha ya watu.
Kwa hakika watu walifurahi kama mwandishi anavyosema “ikawa furaha kuu katika mji ule”. Mitume waliposikia kuwa Samaria wamepokea Neno la Mungu waliwatuma Petro na Yohane ili wawawekee mikono kwa ajili ya kushukiwa na Roho Mtakatifu, maana walikuwa wamebatizwa tu kwa jin