Week Hot newz

Barua

BARUA KWENDA KWA MWENYEZI MUNGU:
MAHABUSU GEREZA LA KEKO SELO NO: 2
TAREHE 10/07/2013
MWENYEZI MUNGU,MUNGU WA IBRAHIMU, MUNGU WA ISLAEL,
MUNGU WA ISAKA,MUNGU WANGU  LEO NIMEISIKIA SAUTI YAKO,
NAFANYA BIDII KUTUNZA NA KUFANYA MAAGIZO YAKO,
MUNGU WANGU UNITUKUZE JUU YA MATAIFA YOTE,
BARAKA ZAKO ZOTE ZINIJALIA,
NIZIDISHIE BARAKA NIBARIKIE MJINI NIBARIKIWE SHAMBANI,
MUNGU UNIFANYA NIWE WA HERI KATIKA UZAO WA TUMBO LANGU NA KATIKA NCHI BWANA ULIYONIPATIA,
MUNGU BABA MUNGU MTAKATIFU SANA MUNGU MWANZO NA MWISHO,
MUNGU BABA WA MWANA YESU KRISTO NA ROHO MTAKATIFU UNIBARIKI NIINGIAPO NA NANITOKAPO,
UWAFANYE  ADUI WAINUKAO JUU YANGU KUPIGWA MBELE YA MACHO YANGU,
WAMENITOKEA KWA NJIA MOJA  WAKIMBIA MBELE YA MACHO  YANGU KWA NJIA SABA,
MUNGU BARAKA YAKO ZIKAE  JUU YANGU NA JUU YA MKE WANGU,
BARAKA ZIWE ZIIDI JUU YA WATOTO WANGU NA KATIKA FAMILIA YANGU,
MWENYEZI MUNGU  NIFANYE KICHWA SIO MKIA,
NAMI NIWE JUU ZAIDI NA SIO CHINI,
MUNGU NIFUNULIE HAZINA NZURI NAYO NI MBINGU,
KWA KUINYESHEA MVUA NCHI YANGU,
MWENYEZI MUNGU  BARIKI KAZI YOTE YA MIKONO YANGU,
 NAMI NITAKOPESHA WALA SITOKOPA TENA,

SHUSHA BARAKA SASA KWA NJIA YA KRISTO BWANA NA MKOMBOZI WANGU, AMINA.

Dawa za kulevya ni haramu!

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 20 Juni 2014 amekutana na wajumbe waliokuwa wanashiriki kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu uthibiti wa dawa za kulevya, tatizo ambalo linaendelea kusababisha majanga makubwa kwa watu wa nyakati hizi.

Auawa kwa kupigwa risasi

MKAZI wa Kijiji cha Masuguru, Kata ya Masagala, wilayani Kishapu, Juma Masalu (25), ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kuingia katika mgodi wa Almasi unaomilikiwa na Wiliamson Diamond. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Kamishina Msaidizi Kihenya Kihenya, alisema tukio hilo lilitokea Juni 13, saa 5 usiku wakati Masalu na wenzake 20 walipoingia ndani ya mgodi huo kwa nia ya kuiba mchanga wenye madini ya almasi.
Kamanda Kihenya alisema wakati wakiiba

Wadau wakutana kupinga ubakaji


Angelina Jolie ni mmoja wa wanaharakati maarufu wanaopinga dhuluma za kingono ikiwemo ubakaji
Viongozi wa kimataifa wanakutana jijini London kwa wiki nzima, kwa kongamano la kumaliza dhulma za kimapenzi katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.
Mkutano huo, wa siku nne umeandaliwa

Saratani ya mlango wa kizazi tatizo Tanzania


Rais Jakaya Kikwete, amesema Tanzania inatambulika kuwa ni moja ya nchi zenye kiwango kikubwa cha maradhi ya saratani ya mlango wa kizazi  Afrika ya Mashariki na kwamba inakadiriwa kuwa takriban wanawake 56 katika kila wanawake 100,000, hupata saratani hii.

Kadhalika, inakadiriwa pia kuwa zaidi ya watu 35,000 hupata saratani hiyo kila mwaka na zaidi ya watu 27,000 hupoteza maisha huku ripoti ikionyesha mwaka 2010 peke yake, wanawake 6,000 waligundulika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na  4,000 kati yao walikufa kutokana na maradhi hayo.

Rais Kikwete aliyasema hayo wakati akizungumza

Roho Mtakatifu anafundisha, anakumbusha, anasali na kufanya unabii!

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Siku kuu ya Pentekoste, tarehe 8 Juni 2014 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican wakati wa mahubiri yake anasema kwamba, Yesu aliwaahidia Mitume wake zawadi kutoka kwa Baba, yaani Roho Mtakatifu na ahadi hii inatekelezwa wakati wa Siku kuu ya Pentekoste.

Hili ni tukio endelevu linaojionesha katika maisha na utume wa Kanisa, kwani Roho Mtakatifu analihuisha Kanisa, anawafundisha, anawakumbusha na kuwasaidia waamini kuzungumza.

Papa Francisko anasema, Roho Mtakatifu ni mwalimu wa maisha yandani anayewaonesha waamini dira na njia ya maisha kama alivyofanya wakati wa Kanisa la mwanzo. Roho Mtakatifu ni njia kama alivyo Yesu mwenyewe, kwani anawasaidia waamini kumfuasa Kristo na kutembea katika nyayo zake. Roho Mtakatifu ni mwalimu wa maisha, ujuzi na maarifa katika uwepo na utume wa maisha ya Kikristo.

Roho Mtakatifu anawakumbusha waamini yale ambayo Yesu

Pentekoste

Tafakari imeletwa kwako na Pd Richard Tiganya, C.PP.S.  

Ni siku nyingine tena tunapokutana katika meza ya Neno la Mungu. Leo tunaadhimisha sherehe ya Pentekoste, sherehe ambayo katika kalenda ya litrujia huja siku hamsini baada ya pasaka. RealAudioMP3

Ni sherehe ambayo wakristu humshangilia Kristu mfufuka katika Roho Mtakatifu na kufurahia ukombozi ambao umeletwa na Kristo mwenyewe. Katika sherehe ya Pentekoste fumbo la pasaka hukamilika maana ni katika sikukuu hii Roho Mtakatifu hulishukia Kanisa ili likaendeleze kazi ya Kristu bila woga, likiwa na nguvu za kimungu. Ni sherehe ambayo kwayo Roho Mtakatifu huthibitisha muungano wetu na Mungu. Ujumbe wa Neno la Mungu unalala katika Roho Mtakatifu kuwa sheria mpya na nguvu ya Wakristu, taifa jipya lililoshikamana katika upendo na Mungu.

Katika somo la kwanza toka kitabu cha Matendo

Njoo Roho Mtakatifu!



Kumsadiki Roho Mtakatifu ni kukiri Nafsi ya tatu ya Fumbo la Utatu Mtakatifu, atokaye kwa Baba na Mwana na anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana. Huyu ndiye Roho Mtakatifu aliyetumwa mioyoni mwa waamini, ili kupokea uzima mpya wa wana wateule wa Mungu. RealAudioMP3

Katika Fumbo la Utatu Mtakatifu usiogawanyika, Mwana na Roho ni Nafsi tofauti lakini hawatenganiki. Tangu mwanzo hadi mwisho wa nyakati, Baba anapomtuma Mwanaye, anamtuma pia Roho wake anayewaunganisha na Kristo kwa imani ili waamini wakiwa wamefanywa waana waweze kumwita Mungu, Abba, yaani Baba.

Siku hamsini baada ya ufufuko wake nidyo Siku kuu ya Pentekoste, Yesu Kristo aliyetukuzwa mbinguni alimmimina Roho Mtakatifu pasi na kipimo, akamdhihirisha kuwa Nafsi ya Kimungu, hivi kwamba, Fumbo la Utatu Mtakatifu limefunuliwa kikamilifu. Utume wa Kristo na ule wa Roho Mtakatifu vilikuwa utume wa Kanisa, lililopelekwa litangaze na kueneza Fumbo la Umoja wa Utatu Mtakatifu.

Kwa ufupi, Roho Mtakatifu anajenga, anahuisha na kutakasa Kanisa. Roho Mtakatifu anawarudishia Wabatizwa hali ya kufanana na Mungu iliyopotezwa kwa njia ya dhambi na anawafanya waishi ndani ya Kristo uzima uleule wa Fumbo la Utatu Mtakatifu. Anawatuma washuhudie ukweli wa Kristo na kuwapanga katika kazi zao maalum, ili wote wazae tunda la Roho.

Hili ndilo Fumbo ambalo linatarajiwa kuadhimishwa na Baba Mtakatifu Francisko katika Siku kuu ya Pentekoste, Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya, kadiri ya taarifa iliyotolewa na Monsinyo Guido Marini Mshereheshaji mkuu wa Ibada za Kipapa.

Historia ya Kanisa la Sabato (4)

NDUGU yangu, ninatumaini nimekufikisha mahali pazuri. Hiyo ndiyo historia ya mshazari wa Kanisa la Wasabato. Kifupi haina mashiko na mtiririko wa kimantiki. Hata hivyo baada ya kuzaliwa kimtindo namna hiyo, Kanisa la Wasabato halikubaki moja kifikra na kimtazamo. Ukilichungulia ndani, Kanisa la Wasabato ni Muungano wa Vikundi vitatu vya Waadventisti; Kikundi cha Bw. Hiram Edson, kilichosisitiza zaidi mafundisho ya huduma ya Yesu Patakatifu pa Patakatifu mbinguni, Kikundi cha Bw. Joseph Bates, kilichosisitiza zaidi kufuata Sabato ya Agano la

Mwanamke Aadhibiwa kwa kumtelekeza mume


Roseline anadaiwa kuwatelekeza watoto wake wanaoishi na baba yao
Na Paskal Linda-Kenya.
Mwanamke mmoja nchini Kenya ameamrishwa na mahakama kumlipa mumewe shilingi elfu tatu au dola 35 kama hela za kukidhi mahitaji yake na watoto wake kila mwezi.
Mwanamke huyo kwa jina Roselyn Muyonga, ambaye anatuhumiwa kwa kuwatelekeza mumewe na watoto wake watatu , huenda akafungwa miezi mitano jela au kutozwa faini ya shilingi laki mbili ikiwa atakosa kutekeleza amri ya mahakama.
Mwanamume huyo hufanya kazi za kibarua.

Kila toba ni Pentekoste Mpya!

 Na: Paskal LindaKardinali Mauro Piacenza, mhudumu mkuu wa Toba katika barua yake kwa mapadre waungamishaji anasema kwamba, kila mara Mkristo anapoungama dhambi zake na kupokea msamaha, huruma na upendo wa Mungu kutoka kwenye kiti cha maungamo, kwa Mkristo hii ni Pentekoste Mpya! Siku kuu ya Pentekoste, ili ni fursa kwa waamini kujipatanisha na Mungu pamoja na jirani zao, ili kuweza kumpokea vyema Roho Mtakatifu anayemiminwa mioyoni mwao, tayari kumtolea Mwenyezi Mungu ushuhuda wa maisha adili na matakatifu!

Neema ya Sakramenti ya Upatanisho anasema Kardinali Piacenza ni mang'amuzi mapya ya Pentekoste kwani hapa Roho Mtakatifu anaendelea kulitakasa Kanisa la Kristo kwa njia ya huduma ya maungamo inayotolewa na Padre akiwa ameungana na Yesu Kristo, ili kusikiliza na kupima, kuamua na kutoa ushauri na hatimaye, kuponya dhambi kwa kumwondolea mwamini dhambi zake. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu anayetenda kwa njia ya wachungaji wake wanaojisadaka katika viti vya maungamano.

Mapadre wanakumbushwa kwamba, wamechaguliwa na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kuwahudumia watu wa Mungu si kwa mastahili yao wenyewe bali kwa njia ya neema ya Roho Mtakatifu inayowaunganisha kwa dhati kabisa na Kristo mwenyewe, ili kushiriki upendo na kazi yake ya ukombozi. Kwa sababu hii, Padre ni mhudumu wa huruma ya Mungu na daraja kati ya waungamaji na Kristo mwenyewe.

Mapadre wanachangamotishwa na Mama Kanisa kuwa wasikivu kwa Roho Mtakatifu na karama zake zinazoliwezesha Kanisa kujitakasa na kuwatakatifuza watoto wake kwa njia ya Sakramenti ya Upatanisho!

Upendo kwa Mungu na jirani!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
 
Baba Mtakatifu Francisko katika utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro amegusia mambo msingi katika maisha na utume wa Kanisa kwa kukazia zaidi na zaidi kanuni maadili na utu wema; utu na heshima ya binadamu; tunu msingi za maisha ya ndoa na familia: Yote haya ni kadiri ya Mafundisho ya Kanisa Katoliki na Kweli za Kiinjili na wala hakuna mabadiliko! RealAudioMP3

Baba Mtakatifu Francisko anapozungumzia masuala haya kwa unyenyekevu mkubwa kutokana na uzoefu wake katika shughuli za kichungaji kuna baadhi ya watu wanapata hisia kwamba, pengine anataka kubadilisha mafundisho na msimamo wa Kanisa Katoliki katika masuala haya, lakini ukweli wa mambo ni kwamba, anachofanya ni kuendelea kukazia masuala haya kwa mwelekeo mpya zaidi!

Ametuacha vibaya!

Amepaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu:

Siku arobaini baadaye ….. Mt. 1,23 – Mungu yu nasi leo tena tunasikia tamko hilo la Yesu mwenyewe.Maana yake nini? Hivyo tunaadhimisha leo uwepo wa Mungu kati yetu na uwepo wa Mungu kati yetu waoneshwa na kazi za watu wake wanaomtii Roho Mtakatifu.

I. Mdo 1,1-11
II. Efe. 1,17-23
III. Mt. 28,16-20

UTANGULIZI

Sherehe ya kanisa siku 40 baada ya sherehe ya Pasaka - kupaa mbinguni Bwana wetu Yesu Kristo. Mhubiri mmoja asema hakuna awezaye kukaa peke yake mke/mume ahitaji mke/mume mwema, mwalimu ahitaji wanafunzi wa kinyume chake nini?

Hivi pia kwa mkristo leo hii yupo Roho Mtakatifu na

Rais mpya wa Malawi aapishwa rasmi


Peter Muthirika anayeongoza chama cha DPP.
Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika ameapishwa rasmi baaada ya kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi kufuatia madai ya udanganyifu na wizi wa kura.
Mutharika aliibuka mshindi wa uchaguzi huo baada ya kujipatia zaidi ya asilimia 36 ya kura zilizopigwa.
Rais anayeondoka mamlakani Joyce Banda alikuwa katika nafasi ya tatu.
Banda amewataka wafuasi wake kuheshimu matokeo hayo.
Mahakama kuu ilipinga ombi la kura kuhesabiwa upya baada ya Banda kudai kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa katika shughuli hiyo.
Peter Mutharika aliwahi kuhudumu kama

Mchawi mtanzania jela miaka 3


Vifaa walivyopatikana navyo washukiwa walipokamatwa na polisi
Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.
Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.
Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation,

Tangazeni Injili ya Furaha kwa ari kuu zaidi!


Kamati kuu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini, CELAM, imehitimisha safari yake ya kikazi mjini Vatican iliyoanza tangu tarehe 20 hadi tarehe 28 Mei 2014 kwa kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko kuhusu maisha na utume wa Kanisa Amerika ya Kusini.

Katika mazungumzo na Baba Mtakatifu, Kamati kuu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini, linasema kuna haja ya kuendelea kuhamasisha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusoma, kutafakari na kumwilisha Waraka wa Kichungaji wa Baba Mtakatifu Francisko, Injili ya Furaha, "Evangelii Gaudium" huko Amerika ya Kusini.

Imekuwa ni fursa kwa viongozi hawa kumshirikisha Baba Mtakatifu Francisko yale yatakayojadiliwa na Maaskofu katika kongamano lao la mwaka, kuhusu familia linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 9 Agosti 2014. Baba Mtakatifu Francisko kwa kuangalia changamoto zilizopo kwa sasa anasema, pengine kuna haja ya kuadhimisha tena Sinodi Maalum kwa ajili ya Maaskofu wa Amerika ya Kusini, kama Kanisa lilivyofanya kwa Maaskofu Katoliki Barani Afrika, Sinodi iliyoitishwa kwanza kabisa na Mtakatifu Yohane Paulo II na kuridhiwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI.

Kamati kuu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Amerika ya Kusini na Caraibi, limepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na viongozi wakuu mjini Vatican pamoja na kutembelea baadhi ya Mabaraza ya Kipapa kuhusu masuala ya: Mafundisho tanzu ya Kanisa, Utamaduni, Familia, Mawasiliano, Uinjilishaji Mpya pamoja na Sinodi za Maaskofu. Viongozi hawa walibahatika kuzungumza pia na Tume ya Kipapa kwa ajili ya Amerika ya Kusini pamoja na Mabalozi kutoka Amerika ya Kusini wanaoziwakilisha nchi zao mjini Vatican ambao wamekabidhiwa hati kuhusu hali ya wakimbizi huko Amerika ya Kusini!

Umefunga na nani pingu za maisha?


Tupo bado kwenye chumba cha karamu ya mwisho tukisikiliza Wosia wa Yesu. Lugha inayotumika leo ni ya kimahaba, yaani, lugha ya upendo wa dhati kama ile ya wanandoa wanaopendana. Lugha hiyo ndiyo anayoitumia Yesu anapoagana na wafuasi wake, na kuwafanya kuhamasika kumsikiliza.

Katika Wosia huo ulio katika sura tano za Injili, neno upendo linatumika mara ishirini na sita. Kwa mara ya kwanza unalikuta kwenye fasuli ya leo: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu,” au vizuri zaidi lingetumika neno: “Kama” mkinipenda. Namna hii ya kuongea kwa upande wa Yesu ni ya kinyenyekevu, ya kuaminia, ya saburi na ya kujali, yaani inajali sana uhuru na hiari ya yule anayeambiwa; kama vile angesema: “Yote yanakutegemea wewe”.

Hiyo ni lugha huru ya Yesu aliye huru. Yesu anatumia lugha ya maelewano na ya makubaliano. Kama sote tujuavyo kwamba mambo mengine yanaweza kutendeka kirahisi, kwa ari na kwa moyo wote endapo yanafanyika kwa hiari, wasemavyo waswahili: “Ukipenda utakula nyama mbichi”.

Injili ya leo ina aya saba na kwa mara saba katika kila aya Yesu

Papa akamilisha Hija yake Mashariki ya Kati na wito wa amani

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu jioni alikamilisha hija yake Mashariki ya Kati na wito wa amani. Hija hii ya siku ya tatu 24-26 Mei 2014 kutembelea maneneo Matakatifu katika Nchi Takatifu aliikamilisha, akiwa mjini Jerusalem ambako hatua ya mwisho aliongoza Ibada ya Misa akiwa na Maaskofu wa Nchi Takatifu, katika jengo lenye Chumba cha Juu ambako Kristo, alifanya karamu ya mwisho, kinachojulikana kama “cenacolo”.

Baada ya Ibada, alielekea uwanja wa ndege wa Monte Scopes , ambako alipanda helkoputa hadi uwanja wa Ndege wa Ben Gourion wa mjini Tel Aviv, ambako aliagana na wenyeji wake, viongozi wa kanisa na serikali wakiongozwa na Rais wa Israel, Shimon Peres. Mahali hapo Papa pia kulifanyika gwaride la heshima la wanajeshi. Na kabla ya kupanda ndege alitoa salaam zake za mwisho kwa wote.

Wachambuzi wa ziara hii wanasema ,

Braeking news:20 wafariki katika ajali ya treni


Treni
Maafisa wa huduma za treni nchini India wanasema kuwa takriban watu 20 wanahofiwa kufariki katika ajali ya gari moshi katika jimbo la Uttar Pradesh.
Treni hiyo ya kubeba abiria iligongana na treni ya jizigo iliyokuwa imeemgeshwa katika kituo cha treni cha Chureb.
Mabehewa sita ya treni hiyo ya Gorakhdham Express yaling'oka kutoka kwenye treni hiyo.
Waokozi wanajaribu kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya treni hiyo na ambao bado wamekwama.
Treni hiyo ilikuwa inasafiri kutoka mjini Gorakhpur hadi katika jimbo la Hisar Haryana

Bikira Maria linda familia, vijana na wazee!



Baba Mtakatifu Francisko Jumapili tarehe 25 Mei 2014 baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Pango la Mtoto Yesu mjini Bethlehemu, amesali pamoja na waamini Sala ya Malkia wa Mbingu, mahali hapa ambapo Bikira Maria alimzaa Mtoto Yesu, akapata nafasi ya kuutafakari uso wa Yesu kuliko mtu mwingine yoyote duniani. Akasaidiwa na Mtakatifu Yosefu kumlaza Mtoto Yesu katika Pango la kulishia wanyama!

Baba Mtakatifu amewaweka wananchi na wakazi wote wa eneo hili chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, ili waweze kuishi katika haki, amani na udugu. Amewaweka pia mahujaji wote wanaotoka sehemu mbali mbali duniani kuja mjini Bethlehemu ili kujichotea neema kutoka kwenye kisima cha imani ya Kikristo, chini ya ulinzi wa Bikira Maria.

Baba Mtakatifu anamwomba Bikira Maria kulinda familia, vijana na wazee; kuwasaidia wale ambao wamepoteza imani na matumaini; awafariji wagonjwa, wafungwa na wote wanaoteseka; awaimarishe viongozi wa dini na Jumuiya nzima ya waamini, ili kweli waweze kuwa ni chumvi na mwanga wa katika Nchi hii. Baba Mtakatifu anamwomba Bikira Maria alinde huduma za elimu zinazotolewa katika eneo hili, lakini zaidi kutoka Chuo Kikuu cha Bethlehemu.

Baba Mtakatifu anapotafakari kuhusu Familia Takatifu, mawazo yake yanakwenda moja kwa moja mjini Nazaret ambako anatamani kwenda kutembelea Mwenyezi Mungu akipenda wakati mwingine tena. Ameonesha upendo na mshikamano wake kwa waamini wote wanaoishi katika eneo hili. Anamwomba Bikira Maria asaidie mchakato wa ujenzi wa udugu, mshikamano na amani
!