Week Hot newz

Mtunis:Kufungia Mwaka 2013 na Who`s Bad

Mtayarishaji na Muigizaji wa filamu za kiswahili nchini Tanzania Nice Mohamed ‘Mtunis’pichani amesema kwamba filamu yake ya Who’s Bad itakuwa kazi yake ya kufungia mwaka  2013 kwa kuzima kazi nyingine za filamu zilizoingia pamoja na filamu hiyo ambayo inafanya vizuri sokoni baada ya kuingia mitaani hivi karibuni.

“Kama ambavyo wengi wamenizoea ninapotoa kazi inakuwa ni bora na lazima ikimbize sokoni, sinema yangu ya Who’s Bad itafunga mwaka kama kazi bora nakuwa makini sana katika utengenezaji wa filamu na ndio kilichofanyika katika filamu hiyo wasanii wamekamua sana na kuonyesho uwezo wa hali ya juu,”anasema Nice.

Filamu hiyo imeshirikisha wasanii kama Patcho Mwamba na washiriki wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu, Mtunis amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kazi alizofanya ni kama Bar mead, Who’s Bad,Clinic Love na kusambazwa na kampuni ya Steps Entertainment.


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni