Ni lazima kugeuka watoto wadogo , maana ndiyo walio wakubwa katika ufalme mbingu. - AFP
Papa Francis anataja sala ya Zaburi ambayo inaonyesha ya kwamba malaika daima walivyo walinzi katika kila aina ya jambo lolote la binadamu na mbinguni. Bwana alimpatia Kila mmoja mwenza anaye muongoza na daima yupo nasi na hali halisi ya kweli, kama balozi wa Mungu kwetu sisi.Na Mungu anatushauri kuwa makini na kugundua uwepo wake , hata kama sisi tukiwaza kutenda ukatili na kufikiri tuko peke yetu si kweli , kwa maana yupo malaika .
Ni lazima kumsikiliza kwa makini sauti yake kwasababu anatushauri . Papa alisema, mara kwa amara tunapoijiwa na mawazo ya kufanya jambo fulani au kujisikia usifanye ni lazima kusikiliza na wala siyo kuwa wakaidi. Aliongeza ya kwamba Malaika walinzi wanatutetea daima na zaidi juu ya ubaya, na kubainisha pia mara nyingi tunafikiria kwamba tunaweza kuficha mambo mengi , na mambo mabaya ambayo mwisho wake lakini hayo yote yatajitokeza kwenye mwanga.
Malaika yupo kutushuauri na kutufunika ni kama vile ambavyo anagefanya rafiki yetu ambaye mara nyingi hatumwoni lakini tunamsikia , ni rafiki ambaye siku moja atakuwa na sisi katika furaha ya milele huko mbinguni.
Rafiki huyo lakini anahitaji usikivu , msindikizaji huyo ni wa kuheshimu na kusikilizwa katika safari yetu anaitwa usikivu kwa makini.Kila Mkristo anapaswa kuwa makini katika usikivu wa roho mtakatifu, Na usikivu wa roho mtakatifu unaanza pale kwenye usikivu wa ushauri wa huyo mwenza wetu katika safari. Ili kuwa wasikivu , papa anaelekeza ni lazima kugeuka watoto wadogo, ambao Yesu mwenyewe alisema ndiyo walio wakubwa katika ufalme wa Baba yake.
Na hivyo papa alimalizia akisema ya kwamaba Malaika walinzi ni wenza wa safari ambao wanatufundisha unyenyekevu, kama vile watoto wanavyotakiwa kusikilizwa. Na tuombe neema ya Bwanan ya kuwa wasikivu , wa kusikiliza sauti ya huyo mwenza wetu , na balozi wa Mungu aliye karibu nasi kwa jina lake, na sisi tunapata msaada kutoka kwake.