Baba Mtakatifu Francisko anawaambia watumiaji wa mitandao ya kijamii kwamba, Ufalme wa mbinguni ni kwa ajili ya watu wanaojiaminisha kwenye upendo wa Mungu na wala si katika mambo ya kidunia.
Katika kilele cha Mwaka wa Imani, Baba Mtakatifu anatarajiwa, Jumamosi jioni kuongoza Ibada ya kuwapokea Wakatekumeni kama kielelezo cha kuvuka Mlango wa Imani, tayari kumpokea Kristo katika hija ya maisha yao ya Kikristo. Ibada hii inatarajiwa kuhudhuriwa na wakatekumeni kutoka sehemu mbali mbali za dunia kama kielelezo cha Ukatoliki wa Kanisa la Kiulimwengu.
Jumapili asubuhi, kwa mara ya kwanza waamini watapata fursa ya kutolea heshima kwa masalia yanayosadikiwa kuwa ni ya Mtakatifu Petro, Mwamba wa Imani, aliyeyamimina maisha yake kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake. Ilikuwa ni Mwaka 1971, Papa Paulo VI alipopewa masalia haya yanayohifadhiwa kwenye Kikanisa cha Papa na kila mwaka ifikapo tarehe 29 Juni, Siku kuu ya Watakatifu Petro na Paulo miamba wa imani masalia haya hupelekwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Katika Sherehe ya Kristo Mfalme wa Dunia, Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kama kilele cha kufunga Mwaka wa Imani, Ibada inayotarajiwa kuanza saa 4:30 kwa saa za Ulaya. Katika Ibada hii, Baba Mtakatifu atawagawia baadhi ya waamini Waraka wake wa kichungaji baada ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani unaojulikana kama "Furaha ya Injili" "Evangelii Gaudium", itakayozinduliwa rasmi, Jumatatu ijayo hapa mjini Vatican.
Week Hot newz
-
Tunaendelea kama kawaida katika kipindi chetu, tafakari masomo Dominika, na leo tunatafakari masomo Dominika ya 33 ya mwaka C wa Kanisa...
-
Teach me, Lord Jesus, to be generous: to serve You as You deserve; to give, not counting the cost; to fight, not heeding the wound...
-
Uchunguzi wa mwili wa Askofu Józef Wesolowski, umekamilika na matokeo kwamba amekufa kifo cha kawaida. Kuf...
-
Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki limezindua tovuti yake inayotoa habari muhimu kuhusu mchango wa Kanisa Katoliki katika sekta ya elimu ...
-
Reading 1, Romans 6:19-23 19 I am putting it in human terms because...
-
NA OSCAR ASSENGA, TANGA-Tanzania.Gazeti Mtanzania. KATIBU wa Chama cha Watu Wenye Albino Mkoa wa Tanga (TAS), Mah...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, tuko tena pamoja katika ile habari ya furaha ndiyo kushirikishana mapendo ya Mungu kwa njia ya meza y...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni