MWENYEKITI wa Simba SC, Ahaj Ismail Aden Rage amewasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dares Salaam usiku huu akitokea Sudan na kusema kwamba;
“Mimi bado Mwenyekiti wa Simba SC,”.
Rage aliwasili kwa ndege ya shirika la Kenya saa 1:40 usiku na kutokea mlango wa Watu maalum (VIP) ambako alilakiwa na wanachama zaidi ya 200, waliokuwa kwenye mabasi sita aina ya Coaster.
“Umati huu uliokuja hapa ni kielelezo tosha sana kwamba kiasi gani wanachama wa Simba wana imani na Mwenyekiti wao, sasa leo sitasema mengi, nitakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari kesho saa saba mchana makao makuu ya klabu(Msimbazi),”alisema Rage.
Alipoulizwa kuhusu kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Jumatatu na kutangaza kumsimamisha, Rage alisema;
“Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, Kamati ya Utendaji haina uwezo wa kumsimamisha Mwenyekiti, usinimalizie utamu njoo kesho mchana Msimbazi,”alisema.
Watu zaidi ya 200 walifika Uwanja wa ndege tangu saa 11 na ushei jioni ya leo kumsubiri Rage wakiimba nyimbo mbalimbali za kumbeza Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na kumpamba Rage huku wakicheza ngoma.
Week Hot newz
-
SIKU moja baada ya kifo cha Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela (95), mazishi yake yanatarajiwa kufanyika wiki m...
-
Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake kwa Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Majilio, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi ...
-
Na Paskal Linda,Vatican. 19/12/2013 Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Desemba 2013 amefanya mazungumzo na Papa ms...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, leo tunasherehekea na kushangilia sherehe ya familia Takatifu. Masiha amezaliwa ndani ya familia hii....
-
Ndege iliyokuwa imetekwa Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shir...
-
Na Dina Ismail, Dar es Salaam MSANII wa muziki wa asili nchini, Pascal linda maarufu kama Batarokota amewaomba mashabiki wa muziki nc...

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni