Week Hot newz
-
SIKU moja baada ya kifo cha Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela (95), mazishi yake yanatarajiwa kufanyika wiki m...
-
Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake kwa Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Majilio, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi ...
-
Na Paskal Linda,Vatican. 19/12/2013 Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Desemba 2013 amefanya mazungumzo na Papa ms...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, leo tunasherehekea na kushangilia sherehe ya familia Takatifu. Masiha amezaliwa ndani ya familia hii....
-
Ndege iliyokuwa imetekwa Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shir...
-
Na Dina Ismail, Dar es Salaam MSANII wa muziki wa asili nchini, Pascal linda maarufu kama Batarokota amewaomba mashabiki wa muziki nc...
Vatican: Papa Francis hayuko hatarini
MAKAO Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani, yamekanusha vikali uvumi ulioenea kwamba Baba Mtakatifu, Francis, yuko hatarini kwa kuwa kundi la kimafia linamuwinda kumfanyia uhalifu kwa kile kilichoelezwa kuhusu uamuzi wake wa kufanya mageuzi katika kanisa hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari wa Vatican, Frederico Kardinali Lombard, alikiambia kituo cha habari cha ABC kwamba hakuna sababu za wazi zinazoweza kuwafanya kuwa na wasiwasi.
“Tuna utulivu wa kutosha, hakuna haja ya kuanza kuwekeana mashaka,” alisema.
Habari zilizonukuliwa hivi karibuni zilimtaja Nicola Gratteri anayeheshimika nchini Italia kwa msimamo wake kinyume na kundi hilo la Mafia akisema kuwa uamuzi wa Baba Mtakatifu kutaka kulifanyia marekebisho kanisa ulilikasirisha kundi hilo la kijasusi.
“Siwezi kusema kama Mafia wanaweza kufanya kitendo hiki, tunawajua kuwa ni watu hatari,” aliongeza Lombard.
Gratteri alilianyia uchunguzi wa kutosha kundi hilo lenye nguvu duniani lenye makazi yake Calabria, Kusini mwa Italia katika sehemu inayoitwa Ndrangheta.
Aliyaongea hayo kwenye kipindi cha televisheni alipokuwa anazindua kitabu chake cha maji matakatifu, kinachohusu Kanisa Katoliki na vikwazo linavyopata katika eneo hilo la Ndrangheta.
Grateri ananukuliwa akisema kuwa uamuzi wa Papa utaangusha nguvu ya kibiashara iliyoko katika mamlaka za Vatican ikiwemo Benki ya Vatican iliyokuwa inafanya biashara zilizolaumiwa kama ni za kiukoo kati ya makleri wa eneo hilo.
Ingawa kwa kiasi kikubwa mauaji yaliyokuwa yanapangwa na Mafia yamepungua kwa kiasi kikubwa tangu miaka ya 1990, matendo ya kihalifu bado yanafanywa na vikundi vinavyojihusisha na ukahaba na watumiaji wa dawa za kulevya, hayo ndio makundi hatari kwa ukuaji wa uchumi wa Italia.
Koo kubwa zinazopatikana Italia kwa sasa zinahusisha, Wasisili wa Cosa Nostra, Wakamora wanaotoka mji wa Napoli, na Kalabrian maarufu kama Ndrangheta, ambao unasadikiwa kuwa wenye nguvu katika matendo ya kihalifu, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Tayari Baba Mtakatifu ameshatangaza kufanya mabadiliko makubwa katika kanisa, akitaka kanisa la kimaskini kwa ajili ya maskini, na ndani ya wiki hii ameshazungumza mara mbili katika misa zake za asubuhi akikemea vitendo vya rushwa na fedha chafu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni