
Baba Mtakatifu Francisko anasema, Mzee Nelson Mandela alisimama kidete kulinda na kutetea utu na heshima ya raia wake; akajenga na kuimarisha umoja wa wananchi wa Afrika ya Kusini pasi na vita, wakitembea katika njia ya upatanisho na ukweli.
Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, mchango wa Mzee Mandela utakuwa ni changamoto kwa wananchi wa Afrika ya Kusini kusimama kidete kulinda haki na mafao ya wengi; wanasiasa wakiwa mstari wa mbele. Baba Mtakatifu anawapatia wananchi wote wa Afrika ya Kusini baraka zake za kitume, wakati huu wa maombolezo ya kitaifa!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni