
Profesa katika Sheria za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa ya Gregorian cha Papa Rome, Padre James J. Conn, SJ, akizungumzia marekebisho hayo ameiambia Redio Vatican kwamba, kuna mabadiliko maalum matatu , hasa katika uharakisha wa kushughulikia kesi za wanaondoa wanaotaka kubatilisha ndoa; kuondolewa kwa haja ya mahakama kutoa hukumu mara mbili kwa tukio na kisha tena kupelekwa katika mahakama ya rufaa, kwa maana kwamba, inatosha kuzingatia maamuzi yaliyotolewa na mahakama kwa mara ya kwanza, iwapo yanayoona kwamba , kuna ushahidi wa kutosha kwa ndoa kutanguliwa, na wahusika wanaweza kufunga ndoa ndoa mpya kwa mujibu wa sheria Kanisa (au katika kupokea miungano ya ndoa ilifungwa kwa sheria za kiraia , wakati huo huo kutambuliwa na Kanisa).
Pia kuanzishwa kwa uwezekano wa kesi kusikilizwa na hakimu mwenye uzoefu mara moja, kama hatua ya kupunguza mzigo wa wingi wa kesi katika mahakama za majimbo, ambako watu wenye ujuzi ni wachache); Na uundaji wa kueleka mchakato wa kesi katika baadhi ya kesi , kutolewa maamuzi moja kwa moja na Askofu mahalia, kwa kesi ambazo zina ushahidi wa kutosha kutolewa hukumu ya kubatishwa na pande zote mbili zinaamini muungano wao ulikuwa batili. Katika mchakato huu hasa unaonyesha dhamira Papa Francisco kugawana madaraka na Maaskofu wa majimbo duniani kote.
Prof Conn, SJ, aliendelea kufafanua kwamba - kinyume na uvumi uliotolewa na baadhi ya vyombo vya hata katika vyombo vya Kanisa, mabadiliko yamefanyika katika misingi ya uelewa wa Kanisa la asili na muundo wa kimsingi wa ndoa, na hivyo hakuna mabadiliko kaika Madhumuni msingi na wigo wa mfumo wa Kanisa mahakama. Na wala hakuna mabadiliko katika mafundisho ya Kanisa juu ya kutengua ndoa, alisema Prof. Conn, SJ. Na kwamba, nayaraka mpya za mabadiliko hazibadilishi kanuni zinazofuatwa na Mahakimu katika kubatilisha ndoa na wala hazibadili uhalali wa ndoa, hivyo, ndoa kubatilishwa linabaki ni jambo linalohitaji uwepo wa ushahidi wa kutosha .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni