Week Hot newz

Moses Josiah aibuka na Macho yameona mengi!

Pichani kutoka kushoto Msanii wa bongo fleva na nyimbo asili ya Kitanzania Batarokota akiwa na mwanamziki wa nyimbo za injili Moses Josiah 

Malkia wa muziki wa gospel nchini bibie Rose Muhando hatimaye amemaliza kurekodi album yake mpya ya sauti pamoja na kurekodi nyimbo mbili kwenye video huko nchini Afrika ya kusini chini ya kampuni ya Sony Music Entertainment ya Afrika ya kusini.

Kwa mujibu wa taarifa alizotoa mwimbaji huyo hii leo amesema amekamilisha nyimbo tatu zilizokuwa zimebakia katika kukamilisha album hiyo ya sauti ambayo hata hivyo hajaitaja jina. Mwimbaji huyo ambaye aliingia mkataba na kampuni hiyo ya kimataifa mapema mwaka jana, tayari amepata mafanikio makubwa kwenye medani ya muziki wa injili nchini tokea atoe album yake ya kwanza ya ''Mteule uwe Macho'' hadi yasasa ya ''Utamu wa Yesu''.

Hapana shaka kwamba album mpya itakuwa na kiwango kikubwa zaidi cha usikivu si kwenye sauti tu pia muziki wake utakuwa umerekodiwa kwenye viwango vikubwa kitu ambacho kitalifanya jina la Kristo lizidi kutangazwa si Tanzania tu bali maeneo mbalimbali duniani. Kila la kheri Rose Muhando.
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2012/08/rose-muhando-akamilisha-album-mpya.html#sthash.kcdnx4hg.dpuf
MWANAMZIKI wa nyimbo za Injili hapa nchini Moses Josiah anayetamba sana Afrika Mashariki na Kati nyimbo zake kama  `Ruadha inmitelona` iliyoimba kwa kijaruo ,hivi karibuni ameibuka albamu mpya inayoitwa `macho yameona mengi.
Mwimbaji Elizabeth Josiah

Akizungumza na Batarokota Online kutoka jijini Mwanza, Nchini Tanzania Mwanamziki Moses Josiah alisema ` nimekamilisha albamu yangu yenye nyimbo nane ambazo ni wewe ni Mungu, Tazama, Ruadha inmitelona,Bwana wa Mabwana,Mwambie Yesu,Galilaya, yeye ndio na Mambo yameona mengi ambayo ndio imechukua jina la album katika kuandaa albamu hii nimeshirikiana na  Mwimbaji Elizabeth Josiah` alisema Moses Josiah

Albamu hii ya Macho yameona mengi inerekodiwa katika studio za EX2 Studio iliyo maeneo ya Mecco jijini Mwanza nchini Tanzania. Na albamu hii ilikamilika mwaka 2014 na kuwa tiyari ila matatizo anayoyapata Mwanamziki Moses Josiah ni kupata wasambazaji ili iweze kuwafikia wapenzi mziki wa injili na anaomba watu wenye kuitaji huduma yake ya kuinjirisha wawasiliane nae kwa facebook.com/Moses Josiah
 Pichani kutoka kushoto Msanii wa bongo fleva na nyimbo asili ya Kitanzania Batarokota akiwa na mwanamziki wa nyimbo za injili Moses Josiah