Week Hot newz

St. Joan of Valois

St. Joan of Valois
St. Joan of Valois
Feastday: February 4
1464 - 1505

Joan of Valois, 1464 - 1505, was the second daughter of Louis X1,  King of France, and Charlotte of Savoy, She was born on April 23,   1464. At the ge of two months she was betrothed to Louis, Duke of Orleans, and the marriage took place in 1476. There is no doubt  that it was invalid, for Louis of Orleans married her in fear of his life  if he did not comply with the king's orders to do so. Joan was by  no means a prepossessing figure: she was hunch-backed, lame and pock-marked. On her husband's succession to the throne he obtained a declaration that the marriage was invalid. Joan, therefore, was not to be queen of France; she was given instread the title of Duchess of Berry. If so it is to be, praised be the Lord, was her remark on this occasion.  And there, really is the basis of her holiness and the spiritual testament that she left in the Order of the Annunciation that she founded; by her choice of name for her nuns she emphasised the parallel between our Lady's *Be it done to me and her own If so it is to be. All her life she met with oppostion and countrered it with such gentle words these. There were difficulties without number. The pope seemed unwilling to give his approval, though Louis X11 approved readily enough, thinking perhaps that Joan, bound by vows, would be less likely to upset the verdict given in the suit of nullity; his fears were groundless, and in any case directly

Rais Tui Atua Tamasese Efi akutana na Papa Francisko mjini Vatican

Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumatatu, tarehe 3 Februari 2014 amekutana na kuzungumza na Rais Tui Atua Tupua Tamasese Efi wa Visiwa vya Samoa, ambaye baadaye alikutana na kuzungumza na Askofu mkuu Pitero Parolin, katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo ya viongozi hawa wawili, wamejikita katika hali ya uchumi na kisiasa pamoja na kuangalia mchango wa Kanisa Katoliki katika mchakato wa maendeleo na ustawi wa wananchi wa Samoa katika medani mbali mbali za maisha. Wamebadilishana mawazo kuhusu masuala ya kimataifa hasa umuhimu wa ushirikiano wa Kikanda, utunzaji bora wa mazingira katika nchi zilizoko kwenye Bahari ya Pacific.



DA and Agang to hold separate press conferences


On Tuesday, Democratic Alliance leader Helen Zille announced that Agang SA leader Mamphela Ramphele would be her party's presidential candidate in the upcoming general elections.
However, confusion arose on Friday over Ramphele's joining the DA.
According to a joint statement issued by Ramphele and Zille on Friday, the Agang SA founder would be welcomed into the DA at a press conference in Johannesburg on Monday.
However, following the joint statement being issued, a message from Ramphele was uploaded onto Agang SA's website.
"You may have by now seen 'joint' statements issued by the Democratic Alliance in which it is claimed that I will be accepting DA membership on Monday," she said.
"This is not true. Nor did I agree to any such statement."
On Sunday, Zille said Ramphele had reneged on the agreement to be the Democratic Alliance's presidential candidate at a meeting on Sunday despite the party negotiating in good faith.

Mchakato wa kukutana na Yesu!



Kadiri ya misale ya mwaka 1962 ya Papa Yohane 23 kipindi cha noeli kinaisha kwa sikukuu ya leo. Lakini baada ya marekebisho ya kalenda mwisho wa kipindi cha Noeli ni baada ya Sikukuu ya Epifania, yaani baada ya sikukuu ya ubatizo wa Bwana wetu. Aidha, ni mwisho wa kipindi cha Epifania.

Zamani sikukuu hii ilijulikana kama sikukuu ya Mweuo wa Bikira Maria, lakini sasa ni “Kutolewa Bwana”. Kabla kabisa sikukuu hii ilikuwa inaadhimishwa huko kwenye Kanisa la Mashariki likijulikana kama sikukuu ya Maonano, au sikukuu ya kukutana kwa

Polisi wavamia msikiti Mombasa


Ramani
Watu 3 akiwemo polisi wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa kwenye ghasia katika mji wa Mombasa, Kenya, baada ya polisi kuvamia msikiti unaosemekana kutoa mafunzi ya itikadi kali za dini ya kiisilamu
Polisi walitumia moshi wa kutoza machozi na risasi za raba dhidi ya waandamanaji na kuwakamata watu 100.
Viongozi wa mombasa wamelaani kitendo cha polisi wakisema kuwa ni kinyume na sheria.
Mashekhe wawili ambao wakihubiri katika msikiti wa Masjid Mussa walipigwa risasi na kuuliwa na watu wasiojulikana katika miezi ya karibuni.
Polisi wa Kenya wameuhusisha msikiti huo na kuajiri wapiganaji wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, ambalo mwaka jana lilishambulia jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi.

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya Nne ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa


Tunaendelea katika safari yetu ya tafakari masomo Dominika ya nne ya kipindi cha mwaka. Neno la Mungu latualika kuwachagua maskini. Katika kuwachagua maskini yatulazimu kuwa maskini wa roho tukitambua kuwa ufalme wa mbinguni unajifungamanisha na heri hiyo.
Katika somo la kwanza, Nabii Sefania anawaalika walio wacha Mungu, kutafuta daima haki na unyenyekevu, maana ni kwa njia hiyo katika siku ya hukumu Mungu atawahurumia. Anasema kwa hakika wale wote walioonewa na kutumainia jina la Mungu watabakizwa na hawatasahauliwa kamwe.

Nabii Sefania anakuja na mahubiri haya akisukumwa na hali ya maisha ya wakati wake katika kipindi kabla ya uharibifu wa Hekalu la Yerusalemu, na hasa mawazo juu ya mali. Katika kipindi hicho mali ilikuwa ni kipimo cha baraka toka kwa Mungu. Aidha, mtu alionekana kuwa wa maana kwa kuwa na mali. Basi Nabii Sefania na Manabii wengine, wanaona wakati fulani mali hupatikana kwa sababu ya unyonyaji wa maskini, na hivi wanaanza kukemea hali hiyo. Umaskini haukuwa tokeo la dhambi, bali tokeo la madhulumu toka kwa matajiri.

Nabii Sefania anakemea kwa nguvu zote jambo hili pamoja na kwamba alikuwa amezaliwa toka familia tajiri. Anawaalika watu kutambua ujio wa adhabu ya Mungu kama wataendelea na unyonyaji kwa maskini. Ndiyo kusema anawaalika kurudi kwa Mungu kwa njia ya toba na kutenda haki. Nabii anaona kufanya toba lazima kujikite katika kuwa maskini wa roho, kuwa wanyenyekevu daima kama karama msingi kwa ajili ya maisha ya kumpendeza Mungu.

Kwa njia ya Nabii tunatambua, nini maana ya umaskini wa roho, kumbe si hali ya mtu au nafasi ya mtu katika jumuiya bali njia ya kiroho, hali ya ndani ya mtu anayetafuta wokovu. Umaskini wa roho ni kutokuwa na hali ya kujitegemea na kwa namna hiyo kumtegemea Mungu. Ndiyo kusema, mwaliko kwetu hivi leo ni kutafuta namna ya kujinasua toka mali kwa ajili ya uzima wa milele.

Katika somo II toka barua ya Mt. Paulo kwa Wakorinto tunamwona Mungu anavyochagua mambo dhaifu ili kuaibisha wenye hekima. Mungu anachagua maskini wa roho badala ya wanaojigamba. Kumbe Paulo anawaalika Wakorinto waliochaguliwa na Mungu kwa njia ya Kristo, hekima ya Mungu, haki na shime yao kuwa makini katika hilo. Kwa nini Paulo anakuja na fundisho hili? Ni kwamba jumuiya ya Wakorinto ilijawa na utengano kwa sababu ya madaraka na utajiri. Utengano huu ulileta maudhi hasa kwa maskini!

Mt Paulo sasa anawaonya kwa maneno makali na hata yanayoweza kufanya mtu afikiri kuwa hekima si ya maana. Hekima na akili ni vya maana lakini lazima viwe kwa ajili ya huduma kwa watu na kwa Mungu. Mungu anachagua maskini na si fukara, kumbe umaskini wa roho, unaojali maisha ya watu na kumweka Mungu katikati ya safari ya wokovu wa wanajumuiya wanaoishi na kusafiri pamoja wakielekea mbinguni.

Katika somo la Injili, toka Injili ya Matayo, tunapata kutafakari Heri Nane za mlimani. Kwa kifupi Heri Nane ni ufupisho wa mafundisho mazima ya maisha ya kiroho na mwongozo wa namna ya kufika mbinguni. Mungu anawachagua walio maskini wa roho, yaani wale ambao huweza kuchagua njia ya unyenyekevu, huruma, msamaha, furaha, haki, utakatifu, amani, uvumilivu wakati wa taabu itokayo na utafutaji wa haki pamoja na taabu itokayo na dhuluma, kama ndio warithi wa uzima wa milele.
Mpendwa, yafaa kujiuliza, hivi Mungu apendezwa na umaskini? Mbona Injili yatualika kufanya bidii ili kuondoa umaskini katika maisha yetu? Ni kweli, Mungu hapendezwi na umaskini bali apendezwa na umaskini wa roho ambao huleta wokovu. Kuhusu mali, Bwana hatofautiani na manabii waliomtangulia, yaani haoni mali kama alama ya baraka toka kwa Mungu, lakini pia habezi mali. Sasa ataka nini!

Yafaa twende kuangalia neno mali kama lilivyotumiwa na Matayo na matumizi ya mali tuliyonayo! Tukitazama Injili ya Lk 16:9 tunaona neno mali hupata maana sahihi kiroho pale tunapogawanya mali hiyo kwa maskini. Hata hivyo Bwana huona hatari itokanayo na mali tunapoelekea mbinguni, angalia Lk 14:33 akisema hakuna anayeweza kuwa mfuasi wangu kama atashikama na mali. Fundisho la Bwana latudai kujibandua toka mali ili kumfuasa yeye na ndio msingi wa kuweza kuelewa nini maana ya kuwa maskini wa roho.

Mpendwa msikilizaji, mwaliko katika fundisho ni kujipatia uwezo wa kushirikishana mali tulizojaliwa na Mungu. Bwana hapendezwi na ufukara ambao huja bila kuchagua bali hupendezwa na umaskini ambao mtu anauchagua kwa ajili ya huduma ya Injili. Ndiyo kusema furaha kwa wale wanaochagua umaskini kwa ajili ya kujitoa kwa waliowahitaji ni tele na ya uhakika. Umaskini mwingine tofauti na huo si heri na si njia ya kiroho bali njia ya uvivu na kwa hivi hakuna furaha. Aidha umaskini wa roho unaokuja kwa njia ya uchaguzi wa ndani katika mlengo wa Injili ni mwito kwa ajili ya wakristu wote na si kwa tabaka fulani kati ya waamini.

Tukiitazama heri II yaani wanaheri wale wenye huzuni, tunapata kujiuliza swali, je Mungu apendezwa na huzuni? Kwa hakika hapana, kumbe heri hii ni kwa wale ambao wanahuzuni kwa sababu wanateswa kwa ajili ya imani yao. Heri inakuja kwa maana hali yao hiyo itaondolewa na watafarijiwa, na Mungu. Bwana akisonga mbele anatangaza tena heri kwa walio wapole maana watairithi nchi. Wapole ni wale wastahimilivu na wanyenyekevu. Bwana hasifu unyenyekevu na uvumilivu wa asili, yaani zawadi za Mungu kwa mtu tangu kuzaliwa kwake bali asifu upole na uvumilivu wa kiroho ambao mtu hujipatia mbele ya madhulumu ya haki zake, akionesha uvumilivu, akimtegemea Mungu pasipo kupambana kwa njia ya vita!

Mpendwa, katika msingi uleule wa upole Bwana anatangaza heri kwa wenye njaa na kiu ya haki kwa maana watashibishwa. Kwa heri hii, ataka tutambue na tupiganie haki kwa ajili ya wote kama ambavyo mtu hutafuta chakula kwa ajili ya kuishi. Ndiyo kusema, kama ilivyo njaa ya chakula basi ijengeke njaa na kiu ya haki. Mpendwa msikilizaji, Bwana anasonga mbele akitangaza heri wenye huruma, akitaka tuwe na huruma, huruma ambayo hujihusisha katika kuwasaidia wengine, yaani isiyoishia katika kusamehe bali katika kuhakikisha wengine wanapata kuishi na kuokoka. Heri hii inakuja kwa maana ufalme wa Mungu utakapokuwa umetimia nao watapata mmojawapo wa kuwasaidia na kuwafariji. Kristu katika hili anatangaza maisha mpya ambamo ubinafsi na magomvi si vitu vya maana bali mapendo na rehema kwa wengine.

Bwana anasonga mbele katika mafundisho yake akikazia usafi wa moyo kama kigezo cha kuweza kumwona Mungu. Katika heri hii, Bwana hazungumzii useja bali unyoofu na ukweli unaomfanya mtu asihangaikie fikira potofu kinyume na mapenzi ya Mungu. Huyu mwenye usafi wa moyo hagawanyi upendo wake na maisha yake kwa wafalme wawili yaani Mungu na shetani bali tu kwa Mungu. Ni kwa jinsi hiyo basi moyoni mwake hukaa mawazo na mapendo ya kimungu ambayo ndiyo umletea heri na furaha daima. Kilele cha heri hii ni kumwona Mungu.

Katika mambo msingi ambayo mwanadamu anayahitaji ni amani. Amani ni tunda la Roho Mtakatifu. Ni tokeo la kuzaliwa Mwana wa Mungu, kumbuka utukufu kwa Mungu juu na amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema. Bwana anatangaza heri kwa watenda na watafuta amani, yaani wapatanishi kwa ujumla. Neno amani katika Biblia halina maana tu ya kutokuwepo kwa vita bali hulenga ustawi wa watu, haki, furaha, afya njema na maisha maelewano. Mpendwa msikilizaji, maisha ya namna hii hujengwa na hivi Bwana anatangaza heri na baraka kwa wale watakaojishughulisha na ujenzi wa amani katika taifa la Mungu.

Mpendwa msikilizaji, Bwana akimalizia mafundisho yake pale mlimani anakuja na tangazo la heri kwa wale ambao katika kutenda heri hizi na hasa wakitafuta haki wataudhiwa na kudhulumiwa, akisema ufalme wa mbinguni ni wao. Kwa hakika awaye yote anayetafuta kutenda haki, atadhulumiwa na kunyanyaswa. Ndiyo kusema wadhulumaji huogopa ujio wa ukombozi na hivi kujiweka katika mapambano kinyume na ufalme huo. Bwana akijua hilo anatangaza heri kwa awaye yote atafutaye amani yakwamba akibaki imara atapata furaha na baraka za Mungu.

Tukumbuke pia kwamba, Bwana aliteswa, lakini alivumilia kiasi kwamba Mungu akamwadhimisha mno na kumpa jina lipitalo kila aina ya jina. Mpendwa, kupokea heri za Mungu si jambo jepesi, ladai kuzama katika maisha ya kiroho ili polepole kukuza roho ya mapendo na utii kwa Mungu. Tunaitwa kuwa watakatifu kama Baba yetu aliye mbinguni.

Mpendwa mwana wa Mungu nikutakie baraka na heri za mbinguni sasa na daima na milele. Tumsifu Yesu Kristo.

Tafakari hii imeletwa kwako na Pd Richard Tiganya C. PP.S.

St. Julius of Novara

St. Julius of Novara
Missionary and confessor with his brother, Julian. Julius was a priest, and Julian a deacon. They converted pagan temples into churches, commissioned to this undertaking by Emperor   Theodosius I.
 

Isola San Giulio
Julius of Novara (Italian Giulio di Orta), also Julius of Aegina[1] (died 401 AD) was a missionary priest to northern Italy.
His cult is centered at Lake Orta in the Novarese highlands, and in particular on the island which has been named for him since at least the eighth century,[2] Isola San Giulio, and where his presumed relics are preserved in the crypt, called scurolo, of a basilica dedicated to him.
Few facts are known about his career. In the earliest Vita, which dates from no earlier than the eighth century and is of a character as much legendary as historical, the account of his life is interlaced with that of his brother Julian (Giuliano), a deacon whose name is similar enough to suggest that they may have been the same person, but now we know (thanks to recent archaeological finds in Gozzano's previous parish church, S. Lorenzo) that they both existed. The Roman Martyrology commemorates only Julius. It has been said the Julius' name was recited as part of the Ambrosian Rite during the fifth and sixth centuries; however, it has also been claimed that this Julius referred to Pope Julius I.
Julius and Julian may have been Greeks who came to Rome before establishing themselves at Lake Orta. Their legend states that they were educated in the Christian faith by their parents. They are said to have been ordered by Theodosius I to destroy pagan altars and sacred woods and to build Christian churches. They built one hundred churches, according to their tradition. The ninety-ninth church is said to have been built at Gozzano, and dedicated to Saint Lawrence. Julian was buried there. The hundredth church was built by Julius on the island that bears his name; he dedicated it to Saints Peter and Paul.

Vyuo vikuu vinahamsishwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Uinjilishaji Mpya!

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 30 Januari 2014 amekutana na kuzungumza na Wajumbe wa Chuo Kikuu cha Notre Dame, chenye makao yake makuu huko Indiana, Marekani; chuo ambacho kilianzishwa kunako mwaka 1842 na Padre Edward Sorin, kutoka Shirika la Santa Croce.

Chuo hiki kwa sasa kimeamua kufungua tawi lake mjini Roma, ili kuendeleza mchakato wa kuwarithisha vijana wa kizazi kipya utajiri unaofumbatwa katika historia, tamaduni na maisha ya kiroho. Roma ni mji ambamo watakatifu Petro na Paulo waliyamimina maisha yao, kielelezo cha imani inayoendelea kuungamwa na mashahidi wa nyakati zote pamoja na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya: familia, shule na parokia

Aliyeponzwa na tattoo za Diamond afunguka


MWANADADA anayedaiwa kutoka kimahaba na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond’, Farida Msofe, amefunguka kuwa aliyekuwa mume wake ndiye chanzo cha yeye kuwa na mapenzi na msanii huyo. Farida ambaye hakutaka kumtaja jina mumewe huyo, alidaia kuwa alifikia hatua hiyo baada ya kuanza kumletea wanawake ndani ya nyumba yao akidai ni dada zake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Farida ambaye pia ni msanii wa filamu nchini, alisema kuwa ameishi na mume wake kwa miaka tisa lakini kadiri siku zinavyokwenda, ndivyo upendo unavyopoa na kitendo cha kufikia uamuzi wa kuwa na mapenzi na Diamond na kuchora tattoo zake ili kujibu mashambulizi kwa mumewe ambaye naye alijichora jina la mwanamke wake mgongoni.
“Binafsi nilikuwa nampenda sana mume wangu, lakini kitendo cha kuwa anakuja na hawara zake nyumbani kwa nyakati tofauti, huku nikiwapikia bila kujua, kilinifanya na mimi niwe na hasira hasa baada ya kumuona mume wangu

Vodka inawaua wanaume Urusi


Wanaume walevi Urusi
Idadi kubwa ya vifo vya mapema nchini Urusi vinatokana na watu kunywa pombe nyingi , hasa Vodka.
Ripoti hii ni kulingana na utafiti uliofanywa hivi karubini nchini humo.
Utafiti huo kwenye jarida la Lancet unasema kuwa robo ya wanaume nchini Urusi wanakufa kabla ya kufikisha umri wa miaka 55 na wengi wao wanakunywa sana pombe.
Watafiti walichunguza

Mbwana Samatta Mchezaji Bora Wa Mwaka

samattaMshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na mashabiki wa klabu yake ya TP Mazembe katika ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo iliyopewa jina la “Corbeau d’Or”. Samatta ambaye amepewa jina la utani la “Samagoal” na mashabiki wa TP Mazembe aliwabwaga wachezaji wengine watano waliokuwa wakishindana.
Baada ya zoezi zima la upigaji kura matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
1. Mbwana Samatta – Kura 248
2. Asante Solomon – Kura 219
3. Robert Kidiaba – Kura 200
4. Nathan Sinkala – Kura 97
5. Rainford Kadaba – Kura 67

BATAROKOTA AJA NA SONGI `IROMBO LISE`

Msanii wa ngw`anza  fleva toka jijini Mwanza Batarokota mkali wa kurap kwa lugha ya kishahili na kisukuma, msanii huyu ndani ya wiki hii ameibuka na audio ya songi mpya 'irombo lise`, nyimbo hii imerekodiwa ndani ya studio ya Sun light Record iliyo mji kasoro bahari mjini Morogoro maeneo ya Kihonda (Mazimbu Road) . Songi hiyo 'irombo lise' imerekodiwa na kutengenezwa midundo na watayarishaji Batarokota akishirikiana na King Malo. Akizungumnza kwa njia ya simu toka mjini Morogoro msanii Batarokota alisema `nashukuru Mungu mwaka umeanza na nimemaliza kurekodi nyimbo yangu ya kisukuma iitwayo `irombo lise` yaaani Dada yetu na sasa niko katika maandalizi ya video ` alesema msanii Batarokota .Pia baada ya kumaliza na audio Batarokota na sasa video ya song hili 'irombo lise' na kufanyiwa shootingi chini ya usimamizi wa kampuni ya Batarokota iitwayo Paskal Linda Blog kwa udhamini wa Zachalia Linda Entertinment.

Upatu unadhalilisha utu na heshima ya binadamu!



Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake Siku ya Jumatano, tarehe 29 Januari 2013 alikemea vikali tabia ya michezo ya upatu inayodhalilisha utu na heshima ya binadamu na kwa kusema kwamba, huu si Ukristo wala si ubinadamu; ni tabia ambayo inapaswa kukomeshwa ndani ya Jamii kwani inawasababishia watu majanga ya maisha! 


Baba Mtakatifu ameyasema hayo wakati alipokuwa anawasalimia wawakilishi wa Mfuko wa Yohane Paulo II wa washauri dhidi ya upatu kitaifa, ambao baadaye jioni waliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye

AZAM YAPANDA KILELENI, KIPRE AMKAMATA TAMBWE KWA MAGOLi

Azam FC imeonyesha kama wakizubaa, basi inabeba ubingwa baada ya kuichapa Rhino ya Tabora kwa bao 1-0 na kupaa kileleni mwa ligi.

Kwa ushindi huo, Azam FC imesikisha pointi 33 na kuiteremsha Yanga yenye pointi 32 ambayo ilikuwa inaongoza hadi mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.

Kabla ya kushuka uwanjani leo mjini Tanga, Yanga ilikuwa na pointi 31, pointi moja zaidi ya Azam FC, lakini sare dhidi ya Coastal imeifanya ishike nafasi ya pili.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Mbagala jijini Dar, bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast.



Azam inayofundishwa na Kocha Omog raia wa Cameroon ilionyesha soka la taratibu lakini pasi za taratibu na uhakika na mwisho ikafanikiwa kushinda.

Azam FC imeonyesha kama wakizubaa, basi inabeba ubingwa baada ya kuichapa Rhino ya Tabora kwa bao 1-0 na kupaa kileleni mwa ligi.

Kwa ushindi huo, Azam FC imesikisha pointi 33 na kuiteremsha Yanga yenye pointi 32 ambayo ilikuwa inaongoza hadi mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.

Kabla ya kushuka uwanjani leo mjini Tanga, Yanga ilikuwa na pointi 31, pointi moja zaidi ya Azam FC, lakini sare dhidi ya Coastal imeifanya ishike nafasi ya pili.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Mbagala jijini Dar, bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast.

Azam inayofundishwa na Kocha Omog raia wa Cameroon ilionyesha soka la taratibu lakini pasi za taratibu na uhakika na mwisho ikafanikiwa kushinda.

Wajawazito 1,500 wakutwa na VVU


Wajawazito 1,500 wakutwa na VVU 
JUMLA ya wanawake wajawazito 1,576 kati ya 42,712 waliopima

Yanga yashikwa, Azam kileleni


Mabingwa Yanga walishikwa kwa sare ya 0-0 ugenini mkoani Tanga dhidi ya Coastal Union na kushuhudia wakitema uongozi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya Azam FC kushinda 1-0 dhidi ya Rhino Rangers na kushika usukani wa ligi.

Mbeya City ambao waliianza siku ya jana wakiwa na pointi 30 sawa na Azam, nao walidondosha pointui mbili jana kufuatia sare ya 1-1 ugenini Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini.

Matokeo hayo yalimaanisha kwamba Azam sasa wako kileleni mwa msimam

Ni uchawi wa Uturuki, Oman Mkwakwani

WAKATI mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Yanga, wakitarajiwa kushuka kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga kuwavaa wenyeji Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ leo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewataka mashabiki watakaosafiri kwenda huko kuhakikisha wanakamilisha kununua tiketi za elektroniki.
Yanga iliyotoka kusaka makali

Jitahidini kuangalia ukweli katika jicho la Kristo!

Katika Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Mtakatifu Thoma wa Akwino, Mwalimu wa Kanisa na msimamizi wa Taasisi za Kipapa, Jumanne tarehe 28 Januari 2014, Taasisi za Kipapa zilifanya kikao cha hadhara kilichohudhuriwa na viongozi wa Kanisa, Serikali,

Makumbusho ya Vatican ni kati ya vivutio vikuu mjini Vatican!

Zaidi ya watu millioni 5. 5 walitembelea Makumbusho ya Vatican katika kipindi cha Mwaka 2013. Hii ni habari njema kwa kuona kwamba, kuna mamillioni ya watu wanaovutwa kutembelea hazina kubwa ya binadamu inayohifadhiwa kwenye Makumbusho ya Vatican. Watu zaidi ya millioni mbili kila mwaka hutembelea kitengo

Papa kuadhimisha Siku ya Watawa Duniani!



Baba Mtakatifu Francisko katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni sanjari na Siku ya Watawa Duniani, Jumapili ijayo tarehe 2 Februari 2014, kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.


Tiketi za kuingilia kwenye Ibada hii zinapatikana kwenye Ofisi za Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume iliyoko mjini Roma kuanzia Alhamisi tarehe 30 hadi Ijumaa tarehe 31 Januari 2014, kuanzia saa 2:30 hadi saa 7: 00 Mchana

Masalia ya Mwenyeheri Yohane Paulo II yaibwa mjini Aquila!



Askofu mkuu Giuseppe Petrocchi wa Jimbo kuu la Aquila, Italia amewaandikia waamini wake barua kuonesha masikitiko makubwa baada ya watu wasiojulikana kuvunja Madhabau ya Mtakatifu Petro della Jenca na kuiba masalio ya damu ya Mwenyeheri Yohane Paulo II na kufanya kufuru ndani ya Kanisa,

Imported mosquitoes caused Gauteng Malaria


Two cases of malaria reported in southern Johannesburg were likely caused by mosquitoes that were accidentally imported from malaria areas, the Gauteng health department said on Sunday.
"Although the Gauteng province is not a malaria endemic area, there have been cases where the malaria ...infected mosquitoes were imported into the province by people travelling from Malaria endemic areas...," spokesman Simon Zwane said in a statement.
These imported

Kardinali Polycarp Pengo ni mgonjwa


Pichani Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (70) ni mgonjwa, imetangazwa.

Taarifa ya kuugua kwa Kardinali Pengo, kiongozi wa kiroho anayeaminika kwa kukosoa uovu unaofanywa kwenye jamii, imetangazwa na Askofu Msaidizi wa kanisa hilo jimboni humo, Mhashamu Titus Mdoe.

Mdoe, alitoa taarif

Jengeni na kudumisha utamaduni wa kukutana na watu bila woga, ili kuwaonjesha Injili ya Furaha!

Liturujia ya Neno la Mungu, Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Mwaka wa Kanisa, inamwonesha Yesu akianza utume na maisha yake ya hadhara nje ya Mji wa Yerusalem, uliokuwa ni kitovu cha maisha ya kidini, kijamii na kisiasa. Yesu anaamua kuanza utume huu mjini Galilaya ya watu wa Mataifa, mji ambao ulikuwa na watu kutoka katika mataifa, tamaduni na dini mbali mbali, kielelezo cha

Church Leaders Meet Ukraine's President As Protests Spread



(Vatican Radio)-- Ukraine's embattled President Viktor Yanukovich has been meeting with church leaders as anti-government protests are spreading throughout the country. The talks came after the president met the European Union's enlargement commissioner who is in the country to mediate following battles that killed at least three demonstrators.

The office of Ukraine's President

Waraka kuhusu Elimu Katoliki wazinduliwa mjini Vatican

Majiundo ya majadiliano ya kitamaduni katika shule za Kikatoliki: ili kuishi kwa pamoja utamaduni wa upendo. Ni hati iliyowasilishwa kwa waandishi wa habari mjini Vatican na Viongozi wakuu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki, chini ya uongozi wa Kardinali Zenon Grocholewski

Ni hati ambayo imepitishwa na Baba Mtakatifu Francisko hapo tarehe 28 Oktoba 2013,

Pope Francis and French President discuss shared concerns



(Vatican Radio) Pope Francis met with French President Frannçois Hollande on Friday morning to discuss shared concerns and the good relations that exist between France and the Holy See. Following the papal audience, the President also held talks with Secretary of State, Archbishop Pietro Parolin and with the Vatican’s ‘foreign minister’ or Secretary for Relations with States, Archbishop Dominique Mamberti.

A statement from the

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya Tatu ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa

Tupo pamoja tena nawe katika jiji la upendo wa Mungu, yaani Neno lake ambalo daima latupatia uzima na pia latufanya tuwe huru katika maisha yetu kama kweli tunaliishi na kulifuata kwa unyenyekevu. Ni Dominika ya III ya kipindi cha kawaida cha mwaka A, kipindi cha matumaini kama ambavyo chajionesha katika mavazi ya Misa Takatifu, yaani rangi ya kijani.

Masomo tunayoyatafakari tunayapata katika kitabu cha Isaya 9:1-4, 1Kor. 1:10-13,17 na Injili Mt. 4:12-23. Masomo haya yanatupa mwaliko wa kuona na kuupokea mwanga wa Kristu unaoanza

Pope Francis: appeal for peace in Syria



(Vatican Radio) Pope Francis appealed for peace in Syria on Wednesday, offering prayers for leaders and policy experts gathering in Switzerland for a conference aimed at working toward a resolution of the Syrian civil war that has claimed more than 100 thousand lives and driven millions of people from their homes. Listen:

Speaking at the end of his weekly General Audience, Pope Francis said, “I ask the Lord to touch the hearts of all [parties and participants], that, looking only to the greater good of the so sorely tried Syrian people, they might spare no effort to reach as quickly as possible the cessation of violence and the end of the conflict, which has already caused too much suffering.”

The Holy Father went on to say, “I hope for dear nation of Syria [that it undertake] with conviction the path of reconciliation, concord and reconstruction with the participation of all citizens, in which everyone can find in the other, not an enemy, not a rival, but a brother to welcome and embrace.”

The “Geneva 2” international conference for peace in Syria opens Today, Wednesday, January 22nd, in Montreaux, Switzerland, with negotiations to continue in Geneva starting on Friday, January 24th.



Text from page http://en.radiovaticana.va/news/2014/01/22/pope_francis:_appeal_for_peace_in_syria/en1-766183
of the Vatican Radio website

Jifunueni wazi kwa Injili na maajabu ya Mungu – Papa

Jumatatu , Baba Mtakatifu Francisko, alisema uhuru wa Mkristo hupatikana katika utulivu wa kulisikiliza Neno la Mungu na kuliishi. Papa alieleza wakati akihubiri katika Ibada ya Misa, asubuhi, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, ndani ya Vatican. Papa alisema daima ni lazima kuwa tayari kuupokea ujumbe wa injili na miujiza ya Mungu aliyo ihifadhi kwa ajili yetu sisi.

Alisisitiza kwamba,

Wakristu toeni cheche za imani yenu kila siku.



Jumapili, Papa Francisko alifanya ziara ya Kichungaji , katika Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu la Roma , katika mtazamo wa adhimisho la 100 tangu Kanisa kuanzisha Siku ya Kimataifa kwa ajili ya kujali hali ya Wahamiaji na Wakimbizi.
Kanisa hilo, ambalo pia lina hadhi ya Basilika, lililoko karibu na Kituo cha Kikuu Treni cha Kati, jijini Roma , huendeshwa na Wamisionari WaSalesians ya Don

Taharuki ya Mtakatifu Yosefu! Mtu wa haki!



“Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa hivi. Maria mama yake, alipokuwa mchumba wa Yosefu, kabla hawajakaa pamoja alionekana na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mumewe Yosefu akiwa mtu mwadilifu, hakupenda kumwaibisha hadharani. Basi akanuia kumwacha kwa siri.”
(Mt 1:18-19)

Moja ya kifungu cha maneno

Nyumba ya Papa ni mali ya Wakatoliki wote!

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 16 Januari 2014 amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wanaotekeleza dhamana na utume wao kwenye Makazi ya Papa mjini Vatican. Baba Mtakatifu amewashukuru kwa huduma na ukarimu wanaowashirikisha wageni mbali mbali wanaofika mjini Vatican kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Baba Mtakatifu anasema kwamba, Nyumba ya Papa ni mali ya Waamini wote wa Kanisa Katoliki; mahali ambapo wanaonja tone la upendo na moyo wa ukarimu wa kifamilia pamoja na msaada wa kulinda na kudumisha imani ambayo ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mmiliki mkuu wa Nyumba ya Kipapa ni Yesu mwenyewe na wengine wote ni wafuasi na wahudumu wa Injili.

Baba Mtakatifu anasema kutokana uelewa huu, kuna haja kwa wafanyakazi hao kukuza na kudumisha majadiliano ya kina kwa njia ya sala, ili kuimarisha urafiki na uhusiano wa ndani kabisa, tayari kutolea ushuhuda wa upendo na huruma ya Mungu kwa watu wake. Wafanyakazi hawa anasema Baba Mtakatifu wanapotekeleza utume wao, kazi inaweza kuwa ni fursa ya kuwashirikisha wengine furaha ya kuwa ni sehemu ya Fumbo la Mwili wa Kristo, yaani Kanisa.

Baba Mtakatifu anawaalika kuwa makini katika kuisikiliza sauti ya Mwenyezi Mungu inayowaita kila siku, kumtumikia kwa ukomavu na moyo wa ukarimu. Baba Mtakatifu amewatakia wafanyakazi hawa pamoja na familia zao, kheri na baraka kwa Mwaka Mpya 2014.

Ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2014



Hali ya wakimbizi, wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum inahitaji kuangaliwa kwa usawa na ukamilifu zaidi, kwa njia ya ushirikiano wa kimataifa unaosimikwa katika mshikamano na huruma.

Hiki ndicho kiini cha ujumbe wa Siku ya 100 ya Wakimbizi na Wahamiaji inayoadhimishwa na Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 19 Januari. Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Mwaka 2014 unaongozwa na kauli mbiu “Wahamiaji na wakimbizi: kuelekea ulimwengu bora zaidi”.

Tafakari ya Neno la Mungu, Sherehe za Ubatizo wa Bwana



Mpendwa mwana wa Mungu, tuko tena pamoja katika ile habari ya furaha ndiyo kushirikishana mapendo ya Mungu kwa njia ya meza ya Neno lake.

Leo ndipo tunahitimisha kipindi cha Noeli kwa Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana na tunaanza kipindi cha kawaida cha mwaka wa Kanisa. Kumbe leo pia ni Dominika ya kwanza ya kipindi cha kawaida cha mwaka wa Kanisa.

Katika somo la kwanza Nabii Isaya anatupeni habari juu ya mtumishi wa Mungu ambaye anapokea Roho wa Mungu na kazi

Vatican kujieleza kuhusu kashfa za ngono


Papa Francis
Maafisa katika Vatican makao makuu ya kanisa katoliki, wanatarajariwa kuhojiwa na maafisa wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kingono ambazo makasisi wa kanisa hilo waliwatendea maelfu ya watoto.
Maafisa hao walikataa ombi la awali ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa unataka taarifa za kina kuhusu dhuluma za kingono wakisema kuwa visa hivyo vinapaswa kushughulikiwa na idara ya mahakama katika mataifa ambako visa hivyo vilitokea