Week Hot newz

West Ham yapeleka majanga Spurs.



West Ham wakipambana na Tottenham
Mabao mawili katika dakika 10 za mwisho yaliipa ushindi West Ham dhidi ya Tottenham na kuiwezesha kuingia nusu fainali ya kombe la Capital One ambapo itapambana na Manchester City. Tottenham walifungua mlango katika nusu ya pili wakati Emmanuel Adebayor alipofunga bao lake la kwanza tangu mwezi wa Mei.
Westham walisawazisha kupitia kwa Matt Jarvis na zikiwa zimesalia dakika tano mchezo huo kumalizika, Modibo

Mkalimani wa mazishi ya Mandela awa chizi


Thamsanqa Jantjie, mkalimani wa lugha ya ishara
Mkalimani wa lugha ya ishara katika siku ya mazishi ya kitaifa, ya aliyekuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa katika hospitali ya magonjwa ya ya akili.
Mkalimani huyo anashutumiwa kutoa ishara ambazo hazikuendana na kile kilichokuwa kikiongelewa.
Thamsanqa Jantjie "anaweza kuwa na matatizo", amekaririwa mke wake Siziwe akisema hayo.
Wataalam wa lugha ya ishara wamemshutumu kwa

Noeli ni Siku kuu ya imani



Na Paskal Linda,Vatican.
19/12/2013
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Desemba 2013 amefanya mazungumzo na Papa mstaafu Benedikto XVI, ili kutakiana kheri na matashi mema kwa ajili ya Siku kuu ya Noeli na Mwaka Mpya wa 2014. Baba Mtakatifu amekumbusha kwamba,

Chelsea yachapwa na Sunderland


Sunderland imesonga mbele hatua ya nusu fainali ya michuano ya ya Kombe la Capital One baada ya kuichapa Chelsea mabao 2-1.
Chelsea ilimiliki mchezo huo kwa muda mrefu katika dakika zote 90, huku Chelsea ikipata goli kutokana na mchezaji wa Sunderland, Lee Cattermole kujifunga mwenyewe.
Chelsea walionekana kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali hadi dakika za mwisho za mchezo,

Noeli iwe ni siku kuu ya imani na matumaini; mapendo na amani

Baba Mtakatifu Francisko katika Katekesi yake, Jumatano, tarehe 18 Desemba 2013, amewakumbusha waamini kwamba, siku hizi za mwisho mwisho za Kipindi cha Majilio ni mwaliko kwa waamini kujiandaa kiroho ili kumpokea Yesu anayezaliwa tena katika maisha yao.

Baba Mtakatifu anasema, Noeli ni Siku kuu ya furaha na matumaini kwa Mwenyezi Mungu ambaye ameamua kuja na kuishi kati ya watu wake kwa njia ya Mwanaye wa

Mzee Nelson Mandela alikuwa pia shujaa wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Baba wa Demokrasia ya Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela alikuwa pia kiongozi wa Tanzania, shujaa wa Watanzania na Baba wa wananchi wa Tanzania kama alivyokuwa kwa wananchi wa Afrika Kusini.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania na Afrika Kusini zina uhusiano wa kindugu na wa karibu sana kwa sababu ya kazi kubwa iliyofanywa na waanzilishi wa mataifa hayo mawili, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Mandela.

Maisha ya Mandela Afrika ya Kusini wanaikumbuka sana Tanzania

Wananchi wa Afrika ya Kusini wanaikumbuka sana Tanzania kutokana na mchango wake katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika, jambo ambalo limejenga urafiki na undugu wa dhati kati ya Afrika ya Kusini na Tanzania.

Tanzania chini ya uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa mstari wa mbele katika mapambono dhidi ya ukoloni na utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini kwa kuamini kwamba, binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja.

Yesu Kristo ndiye kiini na chemchemi ya furaha ya kweli!

Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake kwa Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Majilio, anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kufurahi kwani Noeli i karibu na kwamba, Kanisa linatumwa kutangaza Habari Njema ya Wokovu, hii ndiyo Injili. Kanisa si kimbilio la watu wenye nyuso za kukunjamana bali ni nyumba ya furaha! Kwa wale wenye majonzi wanaonja furaha ya kweli ndani ya Kanisa.

Furaha hii inatokana na utambuzi kwamba, mtu anapendwa

Chiefs banking on Madiba magic




Kaizer Chiefs will entertain the University of Pretoria at the FNB Stadium in an Absa Premiership match on Monday evening, kick-off at 8:30pm.
Chiefs racked up a third straight league victory when they beat Free State Stars 2-0 away from home in late November.
The Soweto giants are unbeaten at home this season, with four wins and two draws from six matches.
The Amakhosi are placed second on the Absa Premiership log with 21 points from 11 matches.
If they win their game against Tuks and log leaders Mamelodi Sundowns lose their derby match against SuperSport United on the same day, Chiefs will assume first place on the standings.

Mama Maria Nyerere,Kikwete wafunika mazishi ya Mandela


16th December 2013
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza katika mazishi ya aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, hayati Neson Mandela, yaliyofanyika katika kijiji cha Qunu nchini humo jana.
Rais Jakaya Kikwete na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, jana walifunika kwenye ibada maalumu ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, iliyofanyika kijijini kwake Qunu, Mashariki mwa Cape.

Tukio hilo lilitokea baada ya Rais Kikwete kupewa fursa ya kuzungumza kwenye ibada hiyo ambayo ilianza mapema

EMMANUEL ANORLD OKWI ATUA YANGA!!

Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

Baraka Kizuguto

Afisa Habari – Young Africans SC

Disemba 15, 2013.
Photo: BREEEEEEAKING NEEEEEEWWS!!!!

SASA NI RASMIIIIIIIIIIIIIIIIII!!  EMMANUEL ANORLD OKWI ATUA YANGA!!
>> Kweli mwenye pesa sio mwenzako!!
>> Hiini habari kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto

Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nhcini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.
 
Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.
 
Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku  Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria  klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.
 
Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji  watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.
 
Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.
 
Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.
 
Baraka Kizuguto
 
 Afisa Habari – Young Africans SC
 
Disemba 15, 2013.

Papa Francisko mtu mashuhuri kwa Mwaka 2013

Baba Mtakatifu Francisko ameteuliwa na Gazeti maarufu la TIME kuwa ni mtu mashuhuri kwa Mwaka 2013. Akizungumzia uteuzi huu, Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, Vatican kwa ujumla hakushangazwa na uteuzi huu, kwani kuna vielelezo makini vinavyoonesha mguso na mashiko tangu Baba Mtakatifu Francisko achaguliwe kuliongoza Kanisa Katoliki kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Nelson Mandela amezikwa kimila



Hayati Mandela alikuwa kipenzi cha dunia nzima
Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela amezikwa katika kijiji cha Qunu mkoa wa Cape Mashariki nchini Afrika Kusini.
Mjane wa Mandela Graca Machel pamoja na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma walikuwepo katika hafla ya mazishi iliyohudhuriwa na jamaa za karibu wa familia ya Mandela pamoja na viongozi wengine wakuu.
Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa walihudhuria mazishi hayo ambayo yalikuwa ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya

Safari ya Mandela yaishia Kijiji cha Qunu!


Mandela daima alisema anataka kuzikwa nyumbani alikozaliwa Qunu
Kijiji cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo cha shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela.
Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.

Udugu ni silaha dhidi ya umaskini, rushwa na ufisadi;

Udugu ni msingi na njia ya amani; ndiyo kauli mbiu inayoongoza Maadhimisho ya Siku ya 47 ya Kuombea Amani Duniani, itakayofanyika tarehe Mosi, Januari 2014 sanjari na Maadhimisho ya Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu. Huu ni ujumbe unaochota utajiri wake kutoka katika Maandiko Matakatifu pamoja na mang'amuzi ya mshikamano wa kidugu kati ya watu.

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Majilio

Tafakari masomo Dominika, ninafurahi tena kuwa nawe katika safari yetu ya Majilio tukijiandaa kwa ajili ya ujio wa Mwana wa Mungu. Ni wakati huu tunapoimba kwa furaha Masiha wetu njoo, ukatuokoe.
Tuko sasa Dominika ya tatu ya Kipindi cha Majilio ambapo Neno la Mungu linatualika kutambua kwa njia ya imani alama zinazomtambulisha Masiha. Tunapata kutafakari katika Injili juu ya wasiwasi wa Yohane Mbatizaji juu ya Masiha, kiasi kwamba anatuma wafuasi wake tokea gerezani wakamwulize Bwana wakisema, eti wewe ndiye Masiha tuliyemtarajia au tumngojee mwingine?
Yohane Mbatizaji anaingiwa na wasiwasi kwa sababu aliweka matumaini yake katika alama zisizo za kweli! Kwetu sisi yaweza tokea na inatokea mara kadhaa kutumaini katika bwana asiye mwenyewe! Kumbe leo mwaliko ni huo, yaani kuwa makini ili tusianguke katika mtego kama huo!
Mpendwa msikilizaji, alama ambazo zilisadikika na Yohane Mbatizaji na wafuasi wake ni kuwa Masiha ajaye atakuwa hakimu mkali atakayewapatiliza mbali wadhambi. Kinyume chake Masiha hafanyi hilo isipokuwa upendo kwao akitafuta kuwaokoa katika taabu yao hiyo. Mpendwa msikilizaji, kazi na wajibu wetu mkuu, ni kutambua wakati huo tukijiuliza daima, ni alama zipi zinazomtambulisha Masiha ambaye tunaimba kwa furaha tukisema uje kutuokoa!
Ndiyo kusema, alama za kweli tunazipata katika Somo la kwanza toka kitabu cha Nabii Isaya 35:1-6,10 akisema ndipo vipofu na viziwi watakapoona na kusikia, mwenye kupooza atarukaruka tena na bubu kuimba kwa furaha. Mara moja toka katika alama hizi tunagundua kuwa Masiha anakuja kwa ajili ya kuwaondoa walio katika taabu na kuwaweka huru. Taabu kwa kawaida ni tokeo la dhambi, yawezekana dhambi ya mtu binafsi lakini hasa dhambi kwa ujumla.
Mpendwa msikilizaji, katika hili tunaalikwa kuingia katika safari ya toba na uaminifu kwa Injili kama tusomavyo katika Injili ya Marko. 1:15. Katika toba na kuishi Injili tunafikia kwa namna ya pekee kabisa hatua ya kutambua alama zinazomtambulisha Masiha.
Jukumu la kuishi alama hizi linatuweka katika mazingira ya furaha na linatuonesha waziwazi kwamba utawala wa Masiha unaanza kukolea katika maisha yetu.
Mpendwa mwana wa Mungu, inawezekana ikajitokeza kukawa na kuchelewa katika utekelezaji, yaani kuishi toba na hivi tukaweza kukata tamaa, basi Mtume Yakobo anatutia moyo na tumaini akisema, kuweni na subira mpaka Bwana atakapokuja. Katika subira tunataka polepole kutenganisha uovu na ubaya ulio katika jumuiya na katika mtu awaye yote katika ubinafsi wake.
Katika subira Mtume Yakobo anatuonya daima kuachana na tabia ya kuhukumiana maana hakimu mwaminifu ni mmoja yaani Mfalme Masiha. Mtume Yakobo anatuonya katika subira kutambua kuwa safari ya wokovu lazima itazamwe kama mkulima anavyongojea mvua za masika na za vuli.
Mpendwa msikilizaji, kipindi cha Majilio ni kipindi cha neema, ni kipindi cha kupanda ili kujipatia mavuno hapo baadaye, na kwa hakika mavuno ni furaha ya moyo inayokamilishwa katika Yesu Kristu mfufuka ambaye atatufufua siku ya mwisho na kukaa naye katika kiti cha enzi pamoja na Baba mbinguni.
Nikikutakia majilio njema napenda kusema fikiria zaidi kuwalisha maskini na kuwahudumia wagonjwa katika jumuiya yako na jitahidi kuwa adui wa dhambi kila siku ya maisha yako. Mpendwa, hiyo ndiyo namna ya kuishi Majilio ya mwaka huu. Nakukumbusha tena hapo jirani kwako kuna mtoto ambaye amekosa ada ya shule msaidie na mfundishe namna ya kuitumia na zawadi yako kwa hakika ni mbinguni. Tumsifu Yesu Kristo na Bikira Maria.

Tafakari hii imeletwa kwako na Padre Richard Tiganya, C.PP.S.

Teacher handed 3 life sentences for rape

Colonel Jay Naicker said Nkosingiphile Hlekwayo, 50, raped the 11-year-old girl on three occasions in 2009. The court sentenced him on Wednesday.
 

A KwaZulu-Natal school teacher has been handed three life sentences by the Empangeni Regional Court for the rape of an 11-year-old pupil, police said on Friday.
Colonel Jay Naicker said Nkosingiphile Hlekwayo, 50, raped the 11-year-old girl on three occasions in 2009. The court sentenced him on Wednesday.
"The victim reported the matter to her parents and a case was opened at the Empangeni police station," he said.
"The Empangeni family, child protection and sexual offences unit took over the investigation that led to the arrest of the accused on the same day that the offence was reported."
He said Hlekwayo's family allegedly approached the girl's family and promised to pay them or give them cattle if they withdrew the case.
"The victim's parents refused to do so and they... allegedly received death threats. The victim was taken to a place of safety until the case was finalised."
Provincial police commissioner, Lt-Gen Mmamonnye Ngobeni welcomed the sentence and expressed her confidence in the judicial system.

Robin van Persie hatachezea Manchester United kipindi hiki

Robin van Persie 




Robin van Persie hatachezea Manchester United kipindi hiki cha mechi nyingi baada ya kupata jeraha la paja ambalo litamuweka nje mwezi mmoja, meneja David Moyes alisema Ijumaa.
"Robin Van Persie atakuwa nje mwezi mmoja. Alipata jeraha kwenye paja akipiga kona ambayo ilizaa goli (dhidi ya Shakhtar Donetsk on Tuesday)," Moyes aliambia kikao cha wanahabari kabla ya mechi yao ya Jumapili Aston Villa.
Mholanzi huyo, ambaye amefunga mabao saba katika mechi 11 za Ligi ya Premia msimu huu, alirejea baada ya kuuguza jeraha la mtoki wikendi iliyopita wakati wa

Arsenal ya lala kwa Man City 6-3

a
Man City
Manchester City, wametoa ujumbe mkali kwa mahasimu wao kwenye ligi ya Premier Arsenal baada ya kuwacharaza mabao sita kwa matatu.
Upande wa Manuel Pellegrini uliwacharaza Arsenal na kuziba pengo la pointi tatu.
Arsenal walilalamika wakitaka kupewa penalty moja ingawa kwa kweli Man City walikuwa wamejiandaa vilivyo dhidi ya Arsenal, huu ulikuwa kama upepo kwao.

Safari ya Mandela mwisho Kijiji cha Qunu


Jeneza la Mandela
Mwili wa hayati Nelson Mandela umepelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa safari ya mwisho kabla ya kuzikwa siku ya Jumapili kijijini Qunu.
Idadi kubwa ya watu walifurika barabara angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa heshima zao za mwisho.
Mandela aliyefariki tarehe 5/12/2013 atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili tarehe 15/12/2013,