Week Hot newz

Batarokota: Nje ya muziki mimi ni bonge la mchoraji.

 

Nyota wa muziki wa Bongofleva na mziki wa asili ya Kitanzania, Batarokoa akisoma somo katika kanisa la Mt Patric Morogoro.

Nyota wa muziki wa Bongofleva na mziki wa asili ya Kitanzania, Batarokota, amesema nje ya kazi yake ya sanaa ni mchoraji mzuri wa picha asili na mpambaji wa nyumba kwa mitindo ya kiasili na alikuwa akifanya kazi hiyo tangu akiwa shuleni.
 
Batarokota, ambaye hivi jana alitawala vichwa vya habari vikitaharifu ya kwamba amejiunga na chama cha siasa cha ACT-Wazalendo, amesema hadi sasa bado anaipenda kazi hiyo ya kuchora na anazidi kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu zana za kale  kwa sababu ndiyo mambo anayoyapenda.
Msanii wa Bongo fleva na nyimbo za asili ya Kitanzania Batarokota wa pili kushoto akiwa na meneja wako Alon kwa kushoto na Mr Kwiproducer wakiwa kwa shaga ya amani
 
Alisema wakati alipokuwa shuleni alikuwa maarufu sana kwa uchoraji na mcheza ngoma za kisukuma na alikuwa mwalimu wa  wanafunzi wenzake na watu wengine, na licha ya kwamba alikuwa analipwa ujira mdogo, alikuwa anafurahi kuona watu waliomzunguka wamependeza na michoro yake.
 
"Walikuwa wakinilipa pesa ndogo Sh. 500 tu, lakini nilikuwa napenda kuchora na walikuwa wanapendeza hivyo, hali hiyo iliendelea hata nilipokuwa nyumbani. Kuchora na ngoma ni vipaji vyangu , ndiyo maana najitahidi sana niwe na shule ya sanaa," alisema Batarokota.
 
Batarokota alisema angeweza kuwa na shule ya sanaa za kale na mababu,"Unajua mimi jina langu kwa sasa ni kubwa na thamani yake pia ni kubwa, hivyo siwezi kusema nifungue tu kijishule. Napaswa kufungua shule ya Kimataifa kubwa yenye sifa kama ya jina mababu zetu kwama Mwanamarundi, na wengine wengi, kiasi kwamba hata mtu akiangalia na kuambiwa hii shule ni sanaa za makabila makubwa  akubali na kusema 'yes'

Breaking News; Batarokota ajiunga rasimi na ATC-Wazalendo

Msanii wa bongo fleva na nyimbo za asili ya Kitanzania  Batarokota, majira ya asubuhi leo amejiunga rasmi katika chama cha siasa cha ATC-Wazalendo kupata kadi namba 223643 alikabidhiwa kadi na Afisa wa Chama mkoani Morogoro.

Basata yalitoa kifungoni shindano la Miss Tanzania


 

Dar es Salaam.
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limemfungulia mwandaaji wa shindano la urembo la Miss Tanzania, Lino International Agency baada ya kuomba radhi na kufanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,  Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema  LINO International Agency imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne kwa ajili ya maandalizi ili kukamilisha usajili wa mawakala katika ngazi husika.
Mngereza amesema kuwa mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na kutofuata sheria ,kanuni za uendeshaji matukio ya sanaa nchini ,kutokuwakilisha nyaraka mbalimbali za shindano lake na mikataba ya washirki,kutumia  mawakala ambao hawajasajiliwa na kupewa vibali na Baraza la sanaa la Taifa.
Amesema miongoni mwa mapungufu yaliyofanyiwa kazi na Kampuni ya Lino ni mchakato wa kusajili mawakala  na kufanyia marekebisho kanuni na taratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

Rais huchaguliwa kwa kura, si maandamano

mafuriko
MAANDALIZI ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu ni ya kipekee kutokana na kupambwa na mbwembwe nyingi ikiwamo misafara na maandamano makubwa ya wagombea urais. Ni jambo la kujivunia kuona kwamba wananchi wengi wameonyesha mwamko mkubwa wa ushabiki wa kisiasa.
 Hadi sasa dalili za awali zinaonyesha kwamba ushindani mkubwa wa kinyang’anyiro cha urais utakuwa kati ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 Misafara na maandamano makubwa ya wagombea urais hao vinazidi kuteka akili za wananchi wengi waliogawanyika katika makundi mawili yanayoelekea kulingana; kundi linalomshabikia Lowassa na jingine linalomuunga mkono Dk. Magufuli.
Kutokana na misukumo mikubwa ya hisia za kisiasa, kuna wananchi ambao ukiwambia kuwa Dk. Magufuli ndiye rais ajaye wanaweza kukutoa roho! Vivyo hivyo, wapo wengine ambao wakikusikia unasema njia ya Lowassa kuelekea Ikulu ni nyeupe wanaweza kukutenga katika jamii.
Ukiuliza sababu za wanaoamini kwamba Lowassa atashinda urais watakwambia ni misafara na maandamano makubwa ya watu wanaoonekana kumshabikia. Hata kwa upande wa Dk. Magufuli jibu ni hilo hilo!
Lakini kwa upande mwingine, wapambe wa Lowassa wanamuelezea kwamba ni mwajibikaji na mwenye uamuzi mgumu katika masuala ya umma, hivyo anafaa kukabidhiwa uongozi wa nchi kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania kiuchumi na kijamii.
Wengine wanaamini kwamba Dk. Magufuli ndiye anafaa kukabidhiwa mikoba ya Ikulu ya Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete. Kwamba mgombea huyo ni msafi asiye na kashfa za ufisadi, lakini pia hayumbishwi katika kusimamia misingi ya uwajibikaji kwa umma na kutetea maslahi ya Taifa.
Kimsingi hakuna wa kuwalaumu mashabiki wa pande hizo mbili maana wanatekeleza haki yao ya kikatiba na kidemokrasia ilmradi hawavunji sheria za nchi.
Lakini pamoja na haki hiyo, mashabiki hawa wanapaswa kutafakari vizuri juu ya misimamo yao ya kuamini kwamba misafara ya kifahari na maandamano makubwa ya watu ni kielelezo tosha cha ushindi kwa mgombea urais.
Si sahihi kutumia takwimu za idadi kubwa ya watu katika misafara na maandamano kuwa ndiyo kigezo cha ushindi kwa mgombea, maana mbwembwe za aina hiyo hazimchagui rais. Kinachomchagua rais ni kura zinazopigwa kwa utaratibu uliowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), si vinginevyo.
Tukumbuke kwamba mtu yeyote ana uhuru wa kushiriki maandamano ya wagombea urais, ubunge na udiwani bila kuulizwa kitambulisho. Lakini haruhusiwi kupiga kura za kuchagua viongozi wa nafasi hizo kama hana kitambulisho husika na iwapo atakiuka maelekezo ya NEC.
Hii ni sawa na kusema kwamba katika Tanzania hii, kila mtu, yaani mwenye kitambulisho cha kupiga kura, asiye nacho, mtoto na hata mgonjwa wa akili, wote wana uhuru wa kushiriki maandamano ya wagombea, jambo ambalo ni tofauti na utaratibu wa kupiga kura za kuchagua viongozi wa kisiasa.
 Ikumbukwe hata wakati wa ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani hapa Tanzania Julai 2013 maelfu ya watu walijitokeza kumlaki, kumwona na kusikia anachosema, ingawa si kweli kwamba wote walikuwa wanampenda wala kumkubali na kumfurahia. Miongoni mwao walikuwapo wanafiki waliochukizwa na ziara hiyo wakiamini kimakosa kwamba alikuja kusaini mikataba ya kuuziwa nchi yetu!
Misafara na maandamano ya wagombea ni sawa na kokoro ambalo wakati mwingine hubeba viumbe wasiohitajika. Kuna watu wanashiriki misafara na maandamano ya aina hiyo wakiwa na dhmira ya kweli ya kuwaunga mkono wagombea, lakini wengine wanakwenda kufanya kazi zisizo za kisiasa kama vile kulinda usalama, kupiga picha, kurekodi video na sauti.
 Kwa hiyo, kuamini au kujitumainisha kwamba idadi kubwa ya watu kwenye misafara na maandamano ya wagombea ndiyo kigezo cha ushindi, ni sawa na ndoto za mchana kweupe ambazo daima hazitimii.
Itakuwa jambo la maana kama mashabiki na wapambe wa kisiasa watazingatia umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kupiga kuza za kuwachagua wagombea wanaowataka kuliko kujiridhisha na wingi wa watu katika maandamano ambayo hayana nafasi ya kuchagua viongozi.
Kuamini kwamba idadi kubwa ya watu kwenye misafara na maandamano ya wagombea ndiyo kigezo cha ushindi ni dhana potofu na matokeo yake mwisho wa siku upande unaoshindwa katika uchaguzi hudhani umeibiwa kura, na wakati mwingine hugeuka kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani usiyo wa lazima.
Jambo la msingi zaidi kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ni kuongeza juhudi za kuhamasishana (kwa wenye vitambulisho waliojiandikisha kwenye dafrari la kudumu la wapigakura) kujitokeza kwa wingi kupiga kura za kuchagua viongozi tunaowataka siku ya Jumapili Oktoba 25, mwaka huu.
Sambamba na hilo, wananchi wote tunapaswa kushiriki mikutano ya kampeni za wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa ili kuwachuja na kubaini wanaofaa kutuongoza baada kusikia sera na ilani za vyama vyao.
Ingawa baadhi ya wananchi imani zao zimejikita kwenye vyama, lakini ni vizuri zaidi kuchagua mtu kwanza, chama baadaye kwa sababu maendeleo na mabadiliko tunayoyataka yataletwa na viongozi watu, siyo vyama ambavyo daima haviwezi kufanya chochote.
 Lakini pia, tushirikiane kuuombea Uchaguzi Mkuu ujao baraka za Mungu ili ufanyike kwa uhuru na haki. Tuombe tukitambua kwamba mshindi wa uchaguzi huo atakuwa ni yule aliyepigiwa kura nyingi kwa utaratibu halali, si vinginevyo. Mungu ubariki Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015.

Nani akinusuru Chuo cha Ualimu Korogwe?


Chuo cha Ualimu Korogwe
S.L.P. 533, Korogwe
NDUGU Mhariri,
Sisi ni watumishi wazalendo katika Chuo cha Ualimu Korogwe, mkoani Tanga. Tunasikitishwa na uendeshaji mbovu wa chuo chetu.
Uongozi wa juu wa chuo umekuwa dhaifu katika kuchukua uamuzi wa kiutawala ili kulinda hadhi ya chuo hiki kitaifa na kimataifa. Tumejitahidi bila mafanikio kukabili uzembe wa kiuongozi chuoni hapa.
Juhudi zetu ni pamoja kuripoti katika mamkala husika, ikiwamo ngazi ya wizara. Tunaamini kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha za chuo, kuanzia fedha za michango, miradi ya chuo na hata zile zinazoletwa chuoni kutoka wizarani.
Wapo wenzetu waliodiriki kuhoji hadharani, kumuandikia nyaraka mbalimbali na hata kushauri uongozi wa juu wa chuo bila mafanikio. Maarifa yote ya kiutaratibu na kikanuni yalifuatwa bila mafanikio na wengine ilibidi siku moja kumfungia mkuu wa chuo ofisini kama hatua ya kumshinikiza aondoe uozo chuoni.
Hatua zote hizo zimekuwa zikilenga kuwezesha mabadiliko ya kimfumo chuoni na kujibu hoja za msingi, ikiwamo kuitishwa kwa vikao vya ripoti za mapato na matumizi.
Athari za uongozi mbovu chuoni zimeanza kujitokeza ambazo ni pamoja na kuporomoka kwa kiwango cha taaluma chuoni. Kwa mfano, matokeo ya watahiniwa wa mtihani wa taifa kwa mwaka 2012 ni mabaya, zaidi ya watahiniwa 310 wanatakiwa kukariri masomo waliyofeli hapo mwakani wakati wenzao watakapokuwa wanafanya mtihani mingine, pia wapo wanachuo 67 waliofeli kabisa hivyo hawana sifa za kuwa walimu popote pale.
Gharama serikali inazoingia kumsomesha mwanachuo mmoja kwa miaka miwili si chini ya milioni sita (ukijumuisha mishahara ya watumishi, na gharama nyingine za uendeshaji).
Wakufunzi wamekuwa wakiomba vikao vya kujadili hali ya kitaaluma, kwa mfano, kujadili matokeo hayo mabovu lakini kutokana na maovu ya uongozi, imekuwa vigumu vikao hivyo kufanyika.
Tunaamini vikao haviitishwi kwa sababu uongozi utabanwa kuhusu mwenendo wake mbovu. Kero mbalimbali zimekithiri chuoni, kuanzia hali duni ya maktaba ambayo huchangiwa Sh. 10,000 na kila mwanachuo tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi leo lakini hali ya jengo la maktaba si ya kuridhisha.
Hakuna vitabu vya kutosha maktaba, chumba cha maktaba kilichopo hali yake ni mbaya, maabara ya kompyuta si ya kuridhisha. Kuna madai kwamba fedha zinazotoka wizarani kwa ajili ya ukarabati zimekuwa zikitafunwa sambamba na fedha za michango ya Sh. 10,000 kila mwaka ya wanafunzi.
Mashine za kudurufu ni tatizo, wino kwa ajili ya mashine hizo hakuna na wanafunzi hujigharimia ili angalau kujitafutia elimu bora. Inafikia mahali hata barua za mkuu wa chuo zinakaa kwa karani wake zaidi ya wiki mbili bila kuchapwa kisa eti wino hakuna! Hii ni aibu kwa chuo kikubwa kama hiki.
Ndugu mhariri, chuo kina miradi na huduma kadhaa ambazo ni sehemu ya vyanzo vya mapato bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini. Baadhi ya vyanzo vya mapato vya chuo ni pamoja na fedha zinazotokana na huduma ya chakula kupitia mradi wa “Domestic Science” (DS).
Mradi huu unaendeshwa zaidi wakati wa kazi mbalimbali maalumu zinazofanyika eneo la chuo, kwa mfano shughuli za Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) au shughuli nyingine kama semina.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi mikubwa inayokiingizia chuo fedha nyingi lakini hali ya chuo haiendani na mamilioni ya shilingi yanayopatikana kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.
Upo mradi wa mnara wa simu, mradi mdogo wa kantini ya chakula, mradi wa huduma ya mafunzo ya muda mfupi kwa wanafunzi wa sekondari maarufu kwa jina la TAI (Teachers Academic Initiatives) na wale wa elimu ya awali ambao nao unaingiza fedha. Tunaamini mapato ya miradi hii hayafanani na taarifa zilizopo na kwa kweli tunashangazwa na wakaguzi wa hesabu wanaofika chuo hapa na kuondoka kimya kimya bila kuwapo na ripoti kuhusu hali halisi.
Chuo chetu kimepoteza mvuto kwa sababu ya uongozi mbovu, miaka ya nyuma chuo kilikuwa kikipokea wanafunzi zaidi ya 1500 lakini leo hii hata 200 ni vigumu kuwapata. Wakati mwingine tunadhani ni njama zinazohusisha hata vyuo binafsi ili wanafunzi wakasome huko badala ya chuo hiki chenye sifa ya kipekee nchini.
Haturidhiki na mbinu zinazotumiwa na uongozi wa chuo katika kukabili matatizo haya kwa sababu uongozi ni sehemu ya matatizo haya.
Uongozi wenye tuhuma katika miradi ya chuo ukiwamo mradi wa majoho kwa ajili ya mahafali ya wanachuo haupaswi kuaminika kuongoza chuo cha kitaaluma, tena taaluma nyeti ya ualimu. Uongozi unaojihusisha na michango ya fedha za wanafunzi katika hali ya shaka kubwa haupaswi kuongoza chuo hiki.

Batarokota akerwa na Uadui Kwenye Sanaa


Staa wa Bongo fleva na mziki wa asili ya Kitanzania Batarokota



Staa wa Bongo fleva na mziki wa asili ya Kitanzania  ambae mwaka jana aliingia katika kinyanganyiro cha KTMA 2014 katika katengo ya Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya kitanzania ambao wimbo wake wa kwejanga nyangisha uliingia na kuambulia patupu  , Paskal Linda Mgundu  ‘Batarokota ’ambaye hivi karibuni ameweka wazi juu ya kukerwa na namna ushabiki  wa sanaa nchini unavyopelekwa kwenye uadui na sio ushindani  kama ilivyokuwa miaka michache iliyopita.
“Kiukweli kwenye sanaa tumeanza kwenda kwenye njia mbaya sana,aina hii ya ushabiki wa mtindo wa uadui itatupeleka pabaya sana..Mashabiki wa Ali Kiba , Wema sepetu na Diamond  wanapaswa kuliona mapema tatizo hili,” alisema mkali huyo wa bongo fleva na nyimbo asili Batarokota.
Aidha , Batarokota amewaomba mashabiki wake kujiandaa kuipokea nyimbo yake mpya ya  ccm ju ambapo ndani ya songi hiyo amewashirikisha  na wasanii  L.L. J kutoka Rwanda na Castol kutoka DRS, “Ni songi kali sana itakayowavunja mbavu na kuwafundisha  naomba muinunue itakapotoka”.

BATAROKOTA:KWEJAGA-NYANGISHA MWAKA JANA ILINIPAISHA KIMATAIFA

MWANAMUZIKI aliyeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya Kilimanajaro Tanzania  Music Award 2014 Batarokota amedai video ya wimbo wake wa Kwejaga-nyangisha ndio ulioweza kumpaisha kimataifa mwaka jana na kufikia hatua hiyo ambapo sasa atazidisha juhudi ili aweze kufahamika.

Batarokota amedai wimbo wake huo umebeba maudhui halisi ya utamaduni wa Kitanzania kwa Lugha ya kisukuma na ambao umechangia kumweka hapo halipo, Batarokota amesema kuwa mbali na kuanza muziki muda mrefu na kufanikiwa kuingiza nyimbo kwenye Tuzo za kili kwa mara ya kwanza lakini ataendelea na mapambano.

Hata hivyo msanii huyo ameamua rasmi kuimba muziki wenye vionjo vya asili na kuachana na muziki wa kutumia sapo ya beat za magharibi ambao alikuwa akiufanya hapo kwanza, ' kwejanga nyangisha ni nyimbo yangu ya pili nilitoka na Kamle Balongo nikiwa na Mama Nyamoko na nikaona ni vizuri nami nianze na hii, na tana nimekuja na Irombo rise, ila nimeshawahi kutoa songi  nyingi zenye mahadhi ya kizazi kipya ukiwemo upendo kwa mama, ogopa 666, kiama sasa, vita vya wenyewe kwa wenyewe , ni mzuri tu we, total balaa, vichwa vya kale, tumerudi, ', alisema na kuongeza.

Mwenyeheri Sr. Irene Stefani alikuwa ni Mama mwenye huruma na mapendo


Mwenyeheri Irene Stefani: Mama mwenye huruma na mapendo. - RV

Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Tanzania kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko, Leo Jumamosi, tarehe 23 Mei 2015 anatarajiwa kumtangaza Mtumishi wa Mungu Sr. Irene Stefani kuwa Mwenyeheri, katika Ibada ya Misa Takatifu itakayofanyika Jimbo Katoliki la Nyeri, Kenya. Sr. Irene Stefani ni mtawa aliyejitahidi kumwilisha upendo katika maisha yake kwa watu aliokutana nao. Huu ni upendo ambao uliwagusa na kuacha chapa ya kudumu katika maisha ya watu.

Hivi ndivyo anashuhudia Sr. Salesia Mugaya wa Shirika la Consolata katika mahojiano maalum na Radio Vatican, kutoka Jimbo Katoliki la Nyeri ambako, tayari Kanisa linajiandaa kwa ajili ya kumtangaza Mtumishi wa Mungu Sr. Irene kuwa Mwenyeheri. Ni mtawa ambaye ubinafsi hakuwa na nafasi hata kidogo katika maisha yake, akaonesha mshikamano wa umoja na upendo kwa watu wote pasi na ubaguzi, hii ndiyo changamoto kwa watu katika ulimwengu mamboleo.
Mwenyeheri mtarajiwa Irene alijisadaka kama muuguzi, akawahudumia watu kwa mapendo, kiasi cha kuyamimina maisha yake kwa kuambukizwa na ugonjwa wa Tauni wakati akimhudumia Mwalimu Julius Ngalya. Alikuwa ni mpishi mzuri, kiasi kwamba, wengi walifurahia chakula chake; alikuwa ni Mwalimu bora aliyefundisha kwa mfano wa maisha yake, akasimama kidete kuimarisha tunu msingi za maisha ya kifamilia kwa kukazia mawasiliano kati ya wazazi na watoto wao waliokuwa wanaishi Nairobi.Wengi wanamkumbuka kuwa ni Katibu muhtasi wa maskini na wale wasiojua kusoma wala kuandika. Sr. Irene Stefani alikuwa ni Mama mwenye upendo na huruma kama walivyomwita “Nyaatha”.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Askari simameni kidete kulinda amani, sheria, demokrasia na haki msingi


Baba Mtakatifu Francisko akizungumza na Jeshi la Polisi Italia. - OSS_ROM
21/05/2015 15:07
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 21 Mei 2015 amekutana na kuzungumza na ndugu na jamaa ya Askari waliopoteza maisha yao wakati wakitoa huduma kwa nchi yao ya Italia. Amewashukuru kwa ushuhuda wa matumaini ya Kikristo yanayowasaidia katika utekelezaji wa dhamana yao kama Askari, huku wakitekeleza wajibu wao katika uaminifu unaolenga mafao ya wengi; ujasiri unaosaidia makuzi ya mtu na jamii inayomzunguka pamoja na kuunza mazingira yanayowawezesha watu kuishi katika uhuru na kwa kuheshimiana

About the Show Machachari


Machachari

Machachari is a children comedy/ adventure series that depicts the friendship between Govi, Baha and Stella who live in the ghetto neighbouring the suburban estate where their friends Almasi, Joy and Fatso live in.Theirs is a friendship that transcends society's divide of the rich and poor.The story also follows the adventures of our main heroes as they tackle their respective school and home lives with occasional assistance from their 'go- to' adults; Ma dvd- the ghetto clown and Sofia- Almasi's home house help and Ma dvd's girlfriend.Through their adventures we get to see children's impact on family and society as a whole.  

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya tatu ya Kipindi cha Majilio


Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican kipindi cha tafakari, ninakuleteeni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya tatu ya Majilio. Masomo ya Dominika ya tatu daima hutupa ujumbe wa FURAHA. Ndiyo kusema tunaalikwa kufurahi daima katika kuishi imani yetu. RealAudioMP3

Wimbo wa kwanza katika litrujia ya Misa Takatifu unaoimbwa hivi, furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini Bwana yu karibu ni ufupisho kamili wa ujumbe wa Neno la Mungu katika Dominka hii. Basi mpendwa, fungua moyo wako ukaianze siku na Dominika hii kwa uchangamfu wa moyo katika Bwana.

Katika masomo tukianza na lile la kwanza Nabii Isaya anawaalika wana wa Israeli katika furaha hiyo kwa maneno ya kutia moyo, maneno ya kuwatia nguvu ili kujenga tumaini yakwamba siku moja wataondolewa utumwani Babeli, watarudi nyumbani. Ujumbe wa tumaini anawapeni kwa maneno ya furaha akisema Roho wa Bwana amenitia mafuta niwahubirie maskini habari njema, niwagange waliovunjika moyo na kisha kuwatangazia mateka uhuru na zaidi kutangaza mwaka wa Bwana, mwaka wa furaha.

Kama wewe na mimi tungekuwa katika utumwa huo tungefurahi na kurukaruka kama Waisraeli. Leo hii tuko katika utumwa gani? Tuko katika vifungo vya dhambi kiroho, na hivi Masiya anakuja na kutangaza ukombozi toka mikasa hiyo, kwa nini tusifurahi? Tunapaswa na tunaalikwa kurukaruka na kuchangamka. Kuchangamka hakutakuja kama tutaiweka mbali nasi sacramenti ya Kitubio mlango safi, mlango mwembamba kwa ajili ya Ekaristia, umisionari na maisha ya uzima wa milele.

Nabii Isaya anasema tena “nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu, maana amenivika vazi la wokovu. Furaha hii ya Nabii Isaya ni furaha ya kweli kwa maana anaondolewa katika dhiki ya dhambi. Nasi twaweza kufurahi lakini ili tuweze kupata furaha ambayo Masiya atatuletea inatupasa kuwa na moyo wa subira, matumaini, majitoleo toba na uwajibikaji kiroho na kimwili. Ndiyo kusema kuwa na moyo mnyoofu ambao hupokea yote kwa uchaji na furaha.

Kwa namna ileile ambayo Nabii Isaya anawaimarisheni Wana wa Israeli, Mtume Paulo anapowaandikia Watesalonike anawashauri daima waweni watu wa furaha na matumaini. Ndiyo kusema wanapomgonja Bwana wamngoje kwa furaha na wala si kwa kununa na kusikitika daima. Anawataka wapate furaha katika maisha ya sala, shukrani kwa Mungu na daima kumkaribisha Roho Mtakatifu ndani mwao. Kumkaribisha Roho Mtakatifu ni kujitenga na dhambi na kila aina ya ubaya katika maisha ya kila siku. Ni katika kuishi furaha hiyo Mama Kanisa katika mwaka huu anatualika kuungana na Watawa kuwa chachu ya Injili, tukiifanya ipenye katika jumuiya tunamoishi kwa njia ya unabii wetu na hivi kwa namna hiyo itaweza kuzaa matumaini mapya.

Mwinjili Yohane anatupatia namna nyingine ya kujipatia furaha, nayo ni kuwa ushuhuda kwa nuru, na nuru hii ni Kristo Mwana wa Mungu aliye katikati yetu ambaye mara kadhaa hatumfahamu vema. Ni kujishusha kama Yohane Mbatizaji ambaye mbele ya Mwana wa Mungu anaona yeye si kitu, ananyenyekea mbele ya mwumba wake. Yeye ni chombo cha Mungu, sauti iliayo nyikani- itengenenezeni njia ya Bwana. Hili ni fundisho kubwa kwa wanaojikweza ili waweze kuiga mfano wa Yohane mbatizaji na watakatifu wengine kama Mt Yosefu na zaidi sana Mama Mtukuka, Mama wa Mungu anayesema daima “mimi ni mtumishi wa Bwana nitendewe kama ulivyonena”. Ni fundisho na mwanga kwa wale wanyenyekevu ambao wanaalikwa kupiga hatua nyingine katika maisha yao ya kiroho wakikumbuka fundisho la Mt Paulo asemaye “siyo kwamba nimekwishakamilika bali nakaza mwendo ili niweze kulifikia lile taji”.

Habari nzima iliyo ya furaha imelala katika wokovu wetu ambao unakuja kwa njia ya Kristo, Mwana wa Mungu. Kumbe kazi ya kufurahi ni kushikamana na wokovu huo siku zote. Ni kujitahidi kugundua huyu Kristo anakuja namna gani kwetu na anataka tufanye nini, yaani tuishi mapendo. Tusome Neno lake, tupokee sakramenti na tushikamane na uongozi wa Kanisa takatifu. Tumsifu Yesu Kristo.

Tafakari hii imeletwa kwako na Padre Richard Tiganya, C.PP.S.

Kanisa si Mapadre au Maaskofu, bali wabatizwa wote


Baba Mtakatifu Francisco, katika mafundisho yake kwa mahujaji na wageni walio kusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican, ameendelea kulizungumzia Kanisa, katika asili yake kuonekana na maana yake ya kiroho. Fumbo la mwili wa Kristo, uliojengwa ndani ya Roho Mtakatifu na pia uhalisi wa kanisa unao onekana kupitia jumuiya zake, Parokia na majimbo yake katika asili ya muundo wake wa kitaasisi wenye kuwaunganisha waumini kwa pamoja.

Papa amesema, uhalisi huu wa kuonekana wenyewe peke yake, ni fumbo linaonyesha upendo na fadhila nyingi za Mungu zilizofichika ndani mwake ambazo hutekelezwa na waumini wa Kanisa duniani kote. Na ili kuelewa uhusiano kati ya yale yanayoonekana na yale yanayofanyika katika kipimo cha kiroho ndani ya mwili wa Kristo, yaani Kanisa, tunahitaji kumtazama Yesu mwenyewe, kama Mungu na Mwanadamu.

Katika ubinadamu, Kristo anatimiza Mpango Mtakatifu wa Mungu wa kumkomboa binadamu. Na hivyo katika macho ya imani , tunaweza kuelewa jinsi Kanisa linavyo onekana katika mwelekeo wake wa kuzamisha ukweli kamili wa kiroho. Na kwa njia ya sakramenti zake na ushuhuda wake kwa Kristo, katika dunia yetu, Kanisa hutafuta kutangaza upendo wa Mungu na huruma yake kwa watu wote, hasa kwa maskini na wahitaji.

Katika mafundisho yake Papa, amesema, kwa mara nyingi tunasikia watu wakilalamikia Kanisa halijafanya hiki, halijafanya kile. Lakini, Papa akahoji , Kanisa ni nani hasa? , Je ni Mapadre au Maaskofu au Papa? Hapana , Kanisa ni wabatizwa wote. Waamini wote wa Kristo huunda Kanisa. Kanisa linaloonekana si tu la Mapadre, Maaskofu au Watawa, au Papa, bali ni mjumuiko wa waamini wote wabatizwa, wake kwa waume wa pande zote za dunia , ambao hutangaza kwa vitendo upendo wa Mungu usiokuwa na kipimo. Ni familia zilizo simama imara katika imani , ni wazazi wanaoieneza imani kwa watoto wao , ni wagonjwa wanao yatolea mateso yao kwa Bwana wa Kanisa. Huo ndiyo ulikuwa ujumbe wa Papa katika Katekesi hii.

Nakaaya azindua albamu ya Blessing


Nakaaya azindua albamu ya BlessingMSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nakaaya Sumari alikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa albam yake ya pili iitwayo ‘Blessing’ ambayo ameitoa kama zawadi kwa mtoto wake.
Albam hiyo iliyobeba nyimbo 12 ilizinduliwa siku ya Idd Al- Haji katika ukumbi wa Hock Up, jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashabiki lukuki kutoka ndani ya Nchi na Nchi jirani ya Kenya.
Katika uzinduzi huo Nakaaya alisindikizwa na wasanii mbalimbali akiwemo Naaziz kutoka Kenya, G Nako, Hisia, TID, Chid Benz na wengine.
Akizungumza na Tanzania Daima, Naakaya alisema sababu iliyofanya atoe albam hiyo kama zawadi kwa mtoto wake, ni kwa kuwa yeye ni Baraka kwake hata kama akiwa yupo mbali nae atakuwa na matumaini pamoja na faraja.
“Nawashukuru sana watu wa Arusha, wamenisapoti sana tofauti na nilivyotegemea, walijitokeza kwa wingi sana, nimefurahi nimeanza vizuri, ninaomba waendelee kunisapoti,” alisema.
Nakaaya ni dada wa mshindi wa taji la mrembo wa Afrika kwenye mashindano ya dunia ‘Miss World Africa’ na Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari.

Papa ashukuru mapokezi mazuri ya Tirana Albania.

Katekesi ya Papa kwa mahujaji wageni kwa Jumatano hii mjini Vatican, imetafakari safari yake ya kitume katika Mji Mkuu wa Tirana Albania. Ziara ya siku moja lakini aliyoitaja kwamba, ilijaa utajiri mkubwa wa upendo na mshikamano kati ya Jimbo Takatifu na nchi ya Albania.

Katika Maelezo, Papa Francisco amesema, alikwenda Albania, kuonyesha mshikamano wake wa karibu na Kanisa zima na watu wa Albania, taifa ambalo kwa muda wa miaka mingi, liliteswa na kushamiri kwa ukana Mungu , na unyama wa serikali isiyojali uwepo wa Mungu. Baada ya kuangushwa kwa mamlaka hayo, sasa taifa linahitaji kupewa moyo, kwa ajili ya ufanikishaji wa kazi nyingi za kuijenga upya jamii, ili iwe ni jamii yenye kupenda amani na kuheshimiana na kushirikiana katika huduma, kwa ajili ya manufaa ya wote.

Papa ameonyesha kufurahi na kumshukuru Mungu, kwa uwepo wa roho ya mshikamano na mazungumzo kati ya jamii Albania licha ya tofauti za kidini na kitamaduni. Anamwoba Bwana, ili taifa hili lisonge mbela na roho huyo, na kamwe lisirudishwe nyuma katika mateso makali ya ukana Mungu. Papa alieleza kwa kuurejea Mkutano wake na viongozi wa dini mbalimbali, ambamo aliweza mwenyewe kuushuhudia moyo huo wa kuheshimiana na kushirikiana, uliojengwa juu ya utambulisho wa kila mmoja.

Daily Reading for Saturday, September 20th, 2014

Reading 1, First Corinthians 15:35-37, 42-49

35 Someone may ask: How are dead people raised, and what sort of body do they have when they come?
36 How foolish! What you sow must die before it is given new life;
37 and what you sow is not the body that is to be, but only a bare grain, of wheat I dare say, or some other kind;
42 It is the same too with the resurrection of the dead: what is sown is perishable, but what is raised is imperishable;
43 what is sown is contemptible but what is raised is glorious; what is sown is weak, but what is raised is powerful;
44 what is sown is a natural body, and what is raised is a spiritual body. If there is a natural body, there is a spiritual body too.
45 So the first man, Adam, as scripture says, became a living soul; and the last Adam has become a life-giving spirit.
46 But first came the natural body, not the spiritual one; that came only afterwards.
47 The first man, being made of earth, is earthly by nature; the second man is from heaven.
48 The earthly man is the pattern for earthly people, the heavenly man for heavenly ones.
49 And as we have borne the likeness of the earthly man, so we shall bear the likeness of the heavenly one.

Responsorial Psalm, Psalms 56:10-12, 13-14

10 In God whose word I praise, in Yahweh whose word I praise,
11 in God I put my trust and have no fear; what can mortal man do to me?
12 I am bound by the vows I have made, God, I will pay you the debt of thanks,
13 for you have saved my life from death to walk in the presence of God, in the light of the living.

Gospel, Luke 8:4-15

4 With a large crowd gathering and people from every town finding their way to him, he told this parable:
5 'A sower went out to sow his seed. Now as he sowed, some fell on the edge of the path and was trampled on; and the birds of the air ate it up.
6 Some seed fell on rock, and when it came up it withered away, having no moisture.
7 Some seed fell in the middle of thorns and the thorns grew with it and choked it.
8 And some seed fell into good soil and grew and produced its crop a hundredfold.' Saying this he cried, 'Anyone who has ears for listening should listen!'
9 His disciples asked him what this parable might mean,
10 and he said, 'To you is granted to understand the secrets of the kingdom of God; for the rest it remains in parables, so that they may look but not perceive, listen but not understand.
11 'This, then, is what the parable means: the seed is the word of God.
12 Those on the edge of the path are people who have heard it, and then the devil comes and carries away the word from their hearts in case they should believe and be saved.
13 Those on the rock are people who, when they first hear it, welcome the word with joy. But these have no root; they believe for a while, and in time of trial they give up.
14 As for the part that fell into thorns, this is people who have heard, but as they go on their way they are choked by the worries and riches and pleasures of life and never produce any crops.
15 As for the part in the rich soil, this is people with a noble and generous heart who have heard the word and take it to themselves and yield a harvest through their perseverance.

Tafakari ya Neno la Mungu Domonika ya 25 ya Mwaka A,



Mpendwa, tunatafakari masomo ya Jumapili ya 25 ya mwaka wa A wa Kanisa, tukialikwa kuwa na matumaini daima katika kumtafuta Bwana na kutambua kuwa wema wa Mungu ni wa milele kwa watu wote na fikra zake ni tofauti na fikra za kibinadamu. Katika somo la kwanza Waisraeli wako utumwani Babeli kwa sababu hawakutii mausia ya Bwana na zaidi wanaona hawawezi kusamehewa dhambi zao, wamepoteza tumaini na wanaona kana kwamba Mungu amewatupa na kuwaacha kabisa. Zaidi ya hilo wanaongeza kosa jingine tena la kumwona Mungu anayefikiri kama wao, wanafikiri hawezi kuwasamehe tena.


Mpendwa, katika shida yao hiyo Mungu anamtuma Nabii Isaya awaambie kuwa fikra na njia za Mungu ni za juu mno ni tofauti na fikira za kibinadamu kiasi kwamba si rahisi kuzielewa. Zaidi ya hilo Isaya anawakumbusha kuacha njia zao mbaya na kumrudia Bwana. Kumrudia Bwana si tu kuacha dhambi, bali pia kubadili namna ya kumtazama Mungu, Mungu aliye haki na mkamilifu. Mawazo haya yatajitokeza waziwazi katika Injili ambapo tunaona Mungu anayewapenda wote wadhambi kwa wema.

TB Joshua awakosoa waandishi walioandika ghorofa 6 za kanisa lake zimeporomoka, aeleza kilichotokea



Kanisa la mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua linalojulikana kama The Synagogue Church of All Nations limetoa tamko rasmi kuhusu tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa sita la kanisa hilo, tukio lililoripotiwa kuua watu kadhaa na kujeruhi, Ijumaa.
Katika tamko hilo lililowekwa kwenye ukurasa wao wa Facebook, wamewakosoa waandishi walioripoti kuwa kanisa zima limeporomoka na kwamba sio kanisa wanalotumia kwa ibada bali ni jengo.
“Hili ni tamko rasmi kutoka The Synagogue, Church Of All Nations kuhusu habari zinazoripotiwa hivi sasa na vyombo vya habari kufuatia tukio lililotekea leo. Ni jengo na sio kanisa (tunalotumia kwa ibada) kama ilivyoripotiwa. Watu wachache waliokuwa mule wameokolewa. Unachotaka kitokee kwa wenzako, Mungu anakutakia wewe. Hakuna kinachotufanya sisi kumpenda mtu kama kumuombea. Kadiri navyokupenda, ndivyo kadiri nitakavyokuombea.” Limesomeka tamko hilo.
Ingawa hawakuzungumzia kabisa kuhusu watu kupoteza maisha au la..taarifa za awali zimeeleza kuwa watu makumi wamepoteza maisha. Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa wameona miili ya watu waliopoteza maisha ikitolewa katika jengo hilo.
Hata hivyo bado hakuna uthibitisho wa daktari kuhusu taarifa hizo za watu kupoteza maisha.
Inaelezwa kuwa zaidi magari ya wagonjwa (ambulance) 20 yalionekana yakitoka katika eneo hilo yakiwa na majeruhi.


Daily Reading for Thursday, September 4th, 2014

18 There is no room for self-delusion. Any one of you who thinks he is wise by worldly standards must learn to be a fool in order to be really wise.
19 For the wisdom of the world is folly to God. As scripture says: He traps the crafty in the snare of their own cunning
20 and again: The Lord knows the plans of the wise and how insipid they are.
21 So there is to be no boasting about human beings: everything belongs to you,
22 whether it is Paul, or Apollos, or Cephas, the world, life or death, the present or the future -- all belong to you;
23 but you belong to Christ and Christ belongs to God.

Responsorial Psalm, Psalms 24:1-2, 3-4, 5-6

1 [Psalm Of David] To Yahweh belong the earth and all it contains, the world and all who live there;
2 it is he who laid its foundations on the seas, on the flowing waters fixed it firm.
3 Who shall go up to the mountain of Yahweh? Who shall take a stand in his holy place?
4 The clean of hands and pure of heart, whose heart is not set on vanities, who does not swear an oath in order to deceive.
5 Such a one will receive blessing from Yahweh, saving justice from the God of his salvation.
6 Such is the people that seeks him, that seeks your presence, God of Jacob.Pause

Gospel, Luke 5:1-11

1 Now it happened that he was standing one day by the Lake of Gennesaret, with the crowd pressing round him listening to the word of God,
2 when he caught sight of two boats at the water's edge. The fishermen had got out of them and were washing their nets.
3 He got into one of the boats -- it was Simon's -- and asked him to put out a little from the shore. Then he sat down and taught the crowds from the boat.
4 When he had finished speaking he said to Simon, 'Put out into deep water and pay out your nets for a catch.'
5 Simon replied, 'Master, we worked hard all night long and caught nothing, but if you say so, I will pay out the nets.'
6 And when they had done this they netted such a huge number of fish that their nets began to tear,
7 so they signalled to their companions in the other boat to come and help them; when these came, they filled both boats to sinking point.
8 When Simon Peter saw this he fell at the knees of Jesus saying, 'Leave me, Lord; I am a sinful man.'
9 For he and all his companions were completely awestruck at the catch they had made;
10 so also were James and John, sons of Zebedee, who were Simon's partners. ButJesus said to Simon, 'Do not be afraid; from now on it is people you will be catching.'
11 Then, bringing their boats back to land they left everything and followed him.