Ni
mara ya kwanza wafanyibiashara wametajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani.
Shirika hili limeongeza kwamba utumizi mbaya wa mamlaka unasababisha
ongezeko la umasikini, na kuwanyima raia mahitaji muhimu.
Watu
wengi ambao ni masikini wamejipata mara kadhaa wakilazimika kulipa hongo
ikilinganishwa na matajiri, inasema "Transparency International".
Nchi ya Liberia imetajwa kama inayoongoza kwa visa vya ufisadi Afrika. Inafuatwa na Cameroon, Nigeria na Sierra leone.Afrika
mashariki Uganda inaongoza kwa visa vya ufisadi, ikifuatwa na Kenya.
Kusini mwa Afrika Zimbabwe na Zambia zinaongoza katika nchi zenye visa
vingi vya ufisadi.
Botswana, Mauritius na Cape Verde, ndiyo
mataifa pekee ya Afrika ambapo visa vya ufisadi ni vya chini zaidi ikiwa
ni asili mia mbili pekee.
Wafanyibiashara
wakubwa wametakwa kuwa miongoni mwa watu wafisadi zaidi sawa na maafisa
wa polisi Barani Afrika. Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa
na shirika la kuchunguza ufisadi duniani "Transparency International".
Wafanyibiashara
wakubwa wametakwa kuwa miongoni mwa watu wafisadi zaidi sawa na maafisa
wa polisi Barani Afrika. Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa
na shirika la kuchunguza ufisadi duniani "Transparency International".
Ni
mara ya kwanza wafanyibiashara wametajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani.
Shirika hili limeongeza kwamba utumizi mbaya wa mamlaka unasababisha
ongezeko la umasikini, na kuwanyima raia mahitaji muhimu.
Watu
wengi ambao ni masikini wamejipata mara kadhaa wakilazimika kulipa hongo
ikilinganishwa na matajiri, inasema "Transparency International". Image caption
Raia wengi wa Kenya wamelalamikia visa vya ufisadi serikalini
Nchi ya Liberia imetajwa kama inayoongoza kwa visa vya ufisadi Afrika. Inafuatwa na Cameroon, Nigeria na Sierra leone.
Afrika
mashariki Uganda inaongoza kwa visa vya ufisadi, ikifuatwa na Kenya.
Kusini mwa Afrika Zimbabwe na Zambia zinaongoza katika nchi zenye visa
vingi vya ufisadi.
Botswana, Mauritius na Cape Verde, ndiyo
mataifa pekee ya Afrika ambapo visa vya ufisadi ni vya chini zaidi ikiwa
ni asili mia mbili pekee.
St. Bibiana, Virgin and Martyr
(Feast day - December 2nd) Other than the name, nothing is known for
certain about this saint. However, we have the following account from a
later tradition.
In the year 363, Julian the Apostate made Apronianus Governor of Rome. St. Bibiana suffered in the persecution
started by him. She was the daughter of Christians, Flavian, a Roman
knight, and Dafrosa, his wife. Flavian was tortured and sent into exile,
where he died of his wounds. Dafrosa was beheaded, and their two
daughters, Bibiana and Demetria, were stripped of their possessions and
left to suffer poverty. However, they remained in their house, spending
their time in fasting and prayer.
Apronianus,
seeing that hunger and want had no effect upon them, summoned them.
Demetria, after confessing her Faith, fell dead at the feet of the
tyrant. St. Bibiana was reserved for greater sufferings. She was placed in the hands of a wicked woman called Rufina, who in vain endeavored to seduce her. She used blows as well as persuasion, but the Christian virgin remained faithful.
Enraged
at the constancy of this saintly virgin, Apronianus ordered her to be
tied to a pillar and beaten with scourges, laden with lead plummets,
until she expired. The saint endured the torments with joy, and died
under the blows inflicted by the hands of the executioner.
Hata katika umaskini wao, waafrika bado ni watu wenye furaha! - OSS_ROM
Baba
Mtakatifu Francisko amerejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija
yake ya kitume Barani Afrika alikotembelea Kenya, Uganda na Jamhuri ya
Watu wa Afrika ya Kati kuanzia tarehe 25 hadi 30 Novemba 2015. Huko
amepata nafasi ya kujionea na kusikiliza kilio cha Familia ya Mungu
kuhusiana na umaskini, ukosefu wa haki msingi na mahitaji muhimu ya
binadamu. Ameguswa na kilio cha vijana wanaotaka saratani ya rushwa na
vitendo vya kigaidi, uharibifu wa mazingira ipewe tiba muafaka; mambo
yote haya yanahatarisha utu na heshima ya binadamu.
Baba Mtakatifu akiwa njiani amepata
fursa ya kujibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari
waliokuwa kwenye msafara wake. Anasema, pale ambapo sera za uchumi na
maendeleo zinajikita katika ubinafsi, utajiri na mali, hapo utu na
heshima ya binadamu viko rehani. Inasikitisha kuona kwamba, kuna watu
wachache sana wanaomiliki utajiri wa dunia wakati ambapo kuna kundi
kubwa la watu bado linaendelea kuogelea katika dimbwi la umaskini na
magonjwa. Baba Mtakatifu anasema, amesikitishwa
sana na mahangaiko ya wananchi wa kitongoji cha Kangemi, Kenya;
ameguswa na mateso ya watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Watoto
Bangui. Amejionea jinsi watoto wanavyoteseka kutokana na utapiamlo
mkubwa, kwa kukosa dawa na vifaa tiba. Yote haya ni kwa sababu watu
wanapenda kuabudu fedha na mali kuliko utu na heshima ya binadamu.
Magonjwa, umaskini na maafa yataendelea kuwaandama wanadamu ikiwa kama
binadamu mwenyewe hataweza kufanya toba na kumwongokea Mungu. Matajiri
wawe na ujasiri wa kugawana rasilimali ya dunia na maskini, ili waweze
wao pia kufurahia Injili ya maisha! Baba Mtakatifu anakiri kwamba,
ameguswa kwa namna ya pekee na ukarimu, furaha na maisha ya Familia ya
Mungu Barani Afrika hata katika umaskini wao, bado wanaweza kufurahia
maisha. Wameonesha ukarimu wa ajabu kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na
kumsikiliza. Kenya inaonekana kuwa na maendeleo; Uganda bado inajikita
katika mashuhuda wa imani; huu ndio utambulisho wao unaowapatia ujasiri
wa kushuhudia imani inayomwilishwa katika matendo! Katika
Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Baba Mtakatifu anakaza kusema, wao
wana kiu ya amani, upatanisho na msamaha wa kweli; udugu, umoja na
mshikamano wa kitaifa kwa kutambua kwamba wao ni ndugu wamoja! Waamini
wanapaswa kuwa wajenzi wa haki, amani na maridhiano kati ya watu na wala
si wachochezi wa kinzani na misigano mambo ambayo yanasigana na imani
wanayoiungama. Serikali ya mpito Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati
isaidie kuwapatia wananchi: haki, amani, msamaha na upatanisho wa
kitaifa. Bara la Afrika lina utajiri na
raslimali nyingi; lina tunu na tamaduni zinazopaswa kuendelezwa. Kwa
bahati mbaya Bara la Afrika linaonekana na wengi kuwa ni uwanja wa fujo
pasi na usalama. Baba Mtakatifu anakaza kusema, Bara la Afrika limekuwa
kama kichwa cha mwendawazimu, watu wengi wanalinyonya kiasi kwamba
limekuwa ni shahidi wa unyonyaji pasi na huruma. Anasema analipenda Bara
la Afrika na kwamba, kuna haja ya kushikamana ili kuliendeleza Bara la
Afrika badala ya kuendelea kunyanyaswa na wenye nguvu wachache duniani! Baba Mtakatifu anawataka waandishi wa
habari kutekeleza dhamana na wajibu wao kwa kuzingatia kanuni, maadili
na sheria kwani hakuna uhuru pasi na mipaka hata katika mapambano dhidi
ya rushwa na ufisadi ambao umeenea sehemu mbali mbali za dunia hata
mjini Vatican. Vyombo vya habari viwe na ujasiri wa kufunua maovu na
vyombo vya sheria vitekeleze wajibu wake barabara.Waandishi
wa habari waseme ukweli pasi na kuuvuruga kwa ajili ya mafao yao
binafsi; waoneshe weledi katika kazi zao kwa kujikita katika ukweli
pamoja na kuheshimu sifa ya mtu! Waandishi wa habari wawe na ujasiri wa
kuomba msamaha pale wanapokosea na kukiuka kanuni maadili za kazi. Katika mapambano dhidi ya vitendo vya
kigaidi na misimamo mikali ya kidini, viongozi wa kidini wanapaswa
kutekeleza dhamana na wito wao kwa kutambua kwamba, wao ni vyombo na
wajenzi wa: umoja, haki, amani,upatanisho na maridhiano. Misimamo mikali
ya kidini ni saratani ambayo iko katika dini zote na inakwenda kinyume
kabisa cha mafundisho msingi ya kidini. Hapa kuna watu wanatumia
misimamo mikali ya kidini kwa ajili ya mafao ya binafsi, ili kujipatia
fedha na utajiri wa haraka haraka. Baba Mtakatifu Francisko anakiri
kwamba, kumekuwepo na tatizo la kumshirikisha Monsinyo Vallejo Balda
pamoja na Francesca Immaculata Chaouqui katika Tume ya Marekebisho ya
masuala ya uchumi na fedha Vatican, ingawa baada ya kumaliza kazi zao
waliondoka na kwamba, watuhumiwa hawa hawakumnyima usingizi hata kidogo
kwani kile kilichochapishwa kwenye vitabu kinaonesha kazi ya mageuzi
iliyofanywa. Rushwa anakaza kusema Baba Mtakatifu ni adui wa haki.
Mapambano dhidi ya rushwa mjini Vatican ni mchakato ulioanzishwa na
Kardinali Joseph Ratzinger wakati alipotoa tafakari ya Njia ya Msalaba,
siku chache kabla ya kifo cha Papa Yohane Paulo II, akachaguliwa na
Makardinali kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro ili kuendeleza mchakato wa
mageuzi. Kumbe, wizi wa nyaraka za siri kutoka
Vatican ni tendo la jinai na kwamba, Baba Mtakatifu angependa kesi hii
iwe imekamilika na kutolewa hukumu kabla ya kuanza maadhimisho ya Mwaka
Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu, hapo tarehe 8 Desemba 2015,
pengine jambo hili halitawezekana anasikitika kusema Baba Mtakatifu
Francisko na kwamba kwa kushirikiana na Makardinali wataendelea kufanya
mageuzi kadiri ya maelekezo yaliyotolewa na Makardinali katika mikutano
yao kabla ya uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro kunako mwaka 2013. Kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi ambao bado
unaendelea kusababisha vifo vingi miongoni mwa vijana wa kizazi kipya,
Baba Mtakatifu anakaza kusema, Kanisa litaendelea kuhimiza kanuni
maadili na utu wema; kwa kusimama kidete kutangaza na kushuhudia Injili
ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo. Matumizi ya kondomu si dawa ya
kuzuia matatizo na majanga yanayoliandama Bara la Afrika. Kuna ukosefu
wa haki msingi za binadamu; uharibifu mkubwa wa mazingira; baa la njaa
na utapiamlo; ukosefu wa maji safi na salama; bado kuna biashara kubwa
ya silaha, unyonyaji na udhalilishaji wa binadamu; watu hawana makazi
bora na salama. Matatizo na changamoto hizi zikipewa ufumbuzi muafaka
hata Ukimwi utatoweka. Baba Mtakatifu anasema aliwaahidia
Mapatriaki wa Armenia kushiriki katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka
101 ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Armenia. Lakini ikumbukwe
kwamba, vita ni kiwanda kinachozalisha silaha na utajiri kwa watu
wachache, hata katika nchi zile ambazo uchumi wake unachechemea, bado
utakuta wananunua silaha za mapambano! Vita
ni dhambi dhidi ya ubinadamu na madhara yake ni makubwa licha ya vifo
na maafa; vita inasababisha pia biashara haramu ya binadamu,
udhalilishaji wa utu na heshima ya binadamu bila kusahau unyonyaji. Kuna
haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kusimama kidete ili kuhakikisha kwamba,
vita inasitishwa ili amani iweze kutawala katika akili na mioyo ya watu.
Mwenyezi Mungu ndiye asili ya amani changamoto kwa watu wote kuwa ni
vyombo na wajenzi wa amani. Baba Mtakatifu Francisko akizungumzia
kuhusu mazingira anakaza kusema, viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa
wanaoshiriki katiki katika mkutano wa athari za mabadiliko ya tabianchi,
Cop21 huko Paris, Ufaransa wanao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba
kunakuwepo na udhibiti wa athari za mabadiliko ya tabianchi vinginevyo,
dunia itaendelea kushuhudia maafa makubwa kwa watu na mali zao. Baba
Mtakatifu anasema, ana imani na matumaini kwa viongozi wa Jumuiya ya
Kimataifa kwamba, wataweza kutoa majibu muafaka kuhusiana na athari za
mabadiliko ya tabianchi. Dini ya Kiislam ina tunu msingi za
maisha ya kiroho zinazoweza kutumika katika mchakato wa majadiliano ya
kidini katika ujenzi wa udugu na urafiki; maisha ya kiroho yanayojika
katika mambo msingi badala ya kushabikia misimamo mikali ya kidini
ambayo inapatikana katika dini zote. Hii ni changamoto kwa waamini
kutubu, kuongoka na kuomba msamaha, ili dunia iweze kuwa ni mahali
pazuri zaidi pa kuishi. Baba Mtakatifu anasema katika umri
wake, safari ndefu ni taabu na shida anatarajia kwenda nchini Mexico ili
kutoa heshima yake kwa Bikira Maria pamoja na kutembelea baadhi ya
maeneo ambayo hayajawahi kutembelewa na Mapapa. Kunako mwaka 2017 tayari
amekwisha kupata mwaliko wa kutembelea baadhi ya nchi za Amerika ya
Kusini. Mwishoni, Baba Mtakatifu amewashukuru waandishi wa habari wote
waliokuwa kwenye msafara wake Barani Afrika kwa kazi kubwa waliyoifanya
ili kuwahabarisha watu. Amewashukuru kwa maswali yao na kwamba,
ameyajibu kadiri anavyofahamu pale ambapo haja jibu amewaambia wazi wazi
na wala si sehemu ya utamaduni wake kuficha mambo!
Kardinali Pietro Parolin Katibu mkuu wa Vatican katika mahojiano maalum na Gazeti la Avvenire linalomilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Italia anasema, Jumuiya ya Kimataifa pamoja na wapenda amani wote wameshtushwa na mashambulizi ya kigaidi yaliyojitokeza nchini Ufaransa na kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Hakuna mtu au taifa ambalo linaweza kujihakikishia usalama wake kwa asilimia mia moja, jambo la msingi ni watu kuwa waangalifu zaidi na kamwe wasimezwe na woga na hofu zisizo na mvuto wala mashiko!
Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko Barani Afrika kuanzia tarehe 25- 30 Novemba 2015 kwa kutembelea Kenya, Uganda na Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati inatarajiwa kutekelezwa kama ilivyopangwa na kwamba, kwa sasa hakuna mabadiliko yoyote. Kuna changamoto ya ulinzi na usalama Afrika ya Kati, lakini Baba Mtakatifu ameipatia kipaumbele cha kwanza kwani anataka kuwaimarisha ndugu zake katika imani, mapendo na matumaini, tayari kujikita katika majadiliano na ujenzi wa madaraja ya watu kukutana na kusaidiana.
Kuhusu hali ya ulinzi na usalama mjini Vatican anasema, wasi wasi na hofu ipo, lakini mambo haya yanapaswa kukabiliwa kwa ujasiri pasi na kukata wala kukatishwa tamaa, jambo ambalo linaendelea kuoneshwa na Ufaransa pamoja na mataifa mengine. Lengo la magaidi ni kupandikiza mbegu ya hofu na wasi wasi miongoni mwa watu. Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kuwa na ujasiri na mbinu mpya za kupambana na vitendo vya kigaidi.
Kardinali Pietro Parolin anasema, safari ya kikazi iliyokuwa imepangwa na Rais Hassan Rohan wa Iran ili kutembelea Vatican ilifutwa kutokana na sababu za ulinzi na usalama na kwamba, malango ya Vatican yako wazi, anaweza kuja Vatican wakati atakapoona kwamba, inafaa zaidi. Vatican inapenda kuonesha mshikamano na majadiliano na nchi ya Iran kwa ajili ya mafao ya wengi.
Jumuiya ya Kimataifa anasema Kardinali Parolin inaweza kupambana na vitendo vya kigaidi kwa kushirikiana kwa dhati na kwamba, kila serikali inawajibu wa kulinda amani na usalama wa raia wake sanjari na kuhakikisha kwamba, inatumia njia muafaka ili kutekeleza lengo hili msingi na muhimu katika mchakato wa maendeleo na ustawi wa jamii. Kuna haja ya kuendeleza mchakato wa majadiliano kati ya watu, ili kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano; mambo ambayo yanaweza kuchukua muda mrefu kutekelezwa, lakini hatima yake ni amani, utulivu na upatanisho.
Ni wajibu wa Jumuiya ya Kimataifa kufikia maamuzi msingi katika mapambano dhidi ya vitendo vya kigaidi, kwa kuzingatia sheria za kimataifa, haki msingi za binadamu kwa kuendelea kushirikiana pamoja na kudumisha majadiliano kati ya watu, ili kweli maamuzi yanayofikiwa yaweze kutekelezwa na watu wengi zaidi. Viongozi wa kidini wanayo dhamana mahususi katika kusaidia majiundo ya dhamiri za watu ili kusimama kidete kulinda, kutetea na kushuhudia haki, amani na maridhiano ya kweli.
Kardinali Parolin anakaza kusema, maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu yaliyotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko yatazinduliwa rasmi hapo tarehe 8 Desemba 2015 yataendelea kama yalivyopangwa na wala hakuna sababu ya msingi ya kutaka kufuta wala kuhailishwa kwa maadhimisho haya. Hiki ni kipindi cha kuendelea kuhimiza umuhimu wa majadiliano, haki, amani na upatanisho. Maadhimisho ya Jubilei ya huruma ya Mungu iwe ni fursa ya kujikita katika majadiliano ya kidini kama anavyokazia Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa kichungaji juu ya maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu, “Misericordiae vultus” Uso wa huruma.
Mwaka Mtakatifu iwe ni fursa muhimu ya kuwaunganisha waamini wa dini mbali mbali ili kwa pamoja waweze kuondokana na nyanyaso, ubaguzi na vurugu zinazosababishwa na waamini wenye misimamo mikali ya kidini. Dini zote hizi zinaonesha utajiri mkubwa katika dhana ya huruma ya Mungu kwa mwanadamu, katika maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei yahuruma ya Mungu waamini wa dini hizi wanaweza kukutana kama sehemu ya majadiliano ya kidini!
Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya kwa kushirikiana na Serikali
linaendelea kuwahamasisha wananchi wa Kenya na Afrika kwa ujumla kujitokeza kwa wingi
kumpokea na kusali pamoja na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hija
yake nchini Kenya kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 27 Novemba 2015.
Zambia na Vatican zinaadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia. - ANSA
17/11/2015 08:19
Mitandao ya kijamii:
Askofu
mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na
ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican kuanzia tarehe 7 hadi tarehe 12
Novemba 2015 amekuwa na ziara ya kikazi nchini Zambia kama sehemu ya
maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya Uhuru wa Zambia sanjari na Miaka
50 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Vatican na Zambia. Mahusiano haya
yalianzishwa na Mwenyeheri Paulo VI kunako tarehe 27 Oktoba 1965 katika
Waraka wake wa kitume “Africae gentes”.
Akiwa nchini Zambia, Askofu mkuu Gallagher amepata nafasi ya kukutana
na kuzungumza na viongozi wa Kanisa, Serikali ya Zambia chini ya
uongozi wa Rais Edgar Chagwa Lungu pamoja na Mabalozi na wawakilishi wa
Jumuiya ya Kimataifa nchini Zambia. Askofu mkuu Gallagher amebahatika
kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Makanisa kadhaa kwa kukazia
umuhimu wa Zambia kuendelea kuwa ni udongo mzuri kwa ajili ya
kupandikiza Habari Njema ya Wokovu. Akiadhimisha
Ibada ya Misa Takatifu kwa Majandokasisi wa Seminari kuu ya Mtakatifu
Dominiko, Askofu mkuu Gallagher amewataka Waseminari hao kufanya
tafakari ya kina kuhusu maisha na wito wao, daima wakilenga juu zaidi
kwa kuonesha upendo na uaminifu.
Akizungumza na Rais Edgar Chagwa Lungu, wakati wa kumbu kumbu ya
Jubilei ya Miaka 50 ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Zambia na
Vatican, Askofu mkuu Galagher amepongeza mahusiano mazuri ya
kidiplomasia kati ya Vatican na Zambia pamoja na mchango mkubwa
unaotolewa na Kanisa katika ustawi na maendeleo ya wananchi wote wa
Zambia. Kanisa kwa namna ya pekee, limekuwa mstari wa mbele katika
huduma kwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.
Mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili yanalenga kwa namna ya
pekee kudumisha na kuimarisha huduma kwa familia ya binadamu, kwa
kujikita katika mchakato wa maendeleo endelevu, haki na amani. Serikali
ya Zambia kwa namna ya pekee, inalipongeza Kanisa Katoliki kwa mchango
wake katika maendeleo ya wananchi wengi wa Zambia, lakini zaidi katika
sekta ya elimu na afya. Askofu mkuu Gallagher, amepata pia nafasi ya kutembelea nchini Malawi,
huku akiongozana na Askofu mkuu Julio Murat, Balozi wa Vatican nchini
Zambia na Malawi, ambako amepokelewa na viongozi wa Kanisa na Serikali
ya Malawi. Viongozi hawa katika mazungumzo yao wamegusia kwa namna ya
pekee, mambo msingi katika mchakato wa maendeleo endelevu ya wananchi wa
Malawi, ambao kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi, lakini kwa
namna ya pekee baa la njaa na umaskini.
Askofu mkuu Tarcisius Zizaye, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Zambia, amemshukuru kwa namna ya pekee kabisa Baba Mtakatifu Francisko
kwa kuijali Familia ya Mungu nchini Malawi katika shida na mahangaiko
yake; wakati wa raha na machungu. Kwa
upande wake, Askofu mkuu Richard Paul Gallagher amewasilisha salam za
Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuonesha moyo wake wa upendo na sala
kwa wale wote walioathirika kutokana na mafuriko pamoja na ukame wa
kutisha nchini Malawi. Askofu mkuu Gallagher katika Ibada ya Misa
Takatifu, akiwa Malawi, amewataka waamini kuwa ni mashuhuda wa mwanga wa
Injili ya Kristo, kwa kuonesha mshikamano na huduma kwa maskini na
wagonjwa, hasa wale wanaoteseka kutokana na ukimwi. Maaskofu wa Malawi
wamemshirikisha Askofu mkuu Gallagher maisha na utume wa Kanisa nchini
Malawi pamoja na changamoto wanazoendelea kukabiliana nazo.
Askofu mkuu Gallagher akiwa nchini Malawi amekutana na kuzungumza na
Rais Peter Mutharika wa Malawi aliyekuwa ameambatana na viongozi wa
Serikali pamoja na Kanisa. Kwa muda wa miaka arobaini na tisa, Malawi
imekuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Vatican. Katika kipindi cha miaka
yote hii, Kanisa limekuwa mdau wa pekee kabisa katika ustawi na
maendeleo ya wananchi wa Malawi: kiroho na kimwili. Kanisa limesaidia
kudumisha mchakato wa utawala bora na demokrasia nchini Malawi.
Rais Mutharika amelishukuru kwa namna ya pekee kabisa Kanisa Katoliki
kwa msaada mkubwa lililotoa kwa wananchi wa Malawi walipokumbwa na
mafuriko pamoja na ukame wa kutisha. Askofu mkuu Gallagher ametumia
nafasi hii kuwasilisha pia salam na matashi mema kutoka kwa Baba
Mtakatifu Francisko kwa wananchi wa Malawi. Kabla
ya kuondoka kutoka Malawi, Askofu mkuu Gallagher alipata nafasi ya
kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa Watawa wa ndani wa Mtakatifu
Clara kwa kuwataka kuwa kweli ni mashuhuda amini wa maisha ya kuwekwa
wakfu, kwa kufuata mfano wa karama na moyo wa Mtakatifu Clara wa Assisi.
Askofu mkuu Paul Richard Gallagher tayari amerejea mjini Vatican na
anaendelea “kudunda mzigo kama kawa”.
RAIS John Magufuli amewasili mkoani Dodoma kwa mara ya kwanza tangu
achaguliwe kuongoza Tanzania akiwa ametumia njia ya barabara huku akiwa
na siri moyoni ya nani atakuwa Waziri Mkuu wake. Njia aliyotumia kufika
Dodoma imewashangaza wengi kutokana na ukweli kwamba marais
waliotangulia wamekuwa wakitumia usafiri wa ndege.
Baada ya kuwasili Ikulu Ndogo ya Rais iliyopo Wilaya ya Chamwino
mkoani Dodoma akitokea jijini Dar es Salaam, alipokewa na viongozi
mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Chamwino Ikulu, Joseph
Seganje, wananchi wamefarijika kuona Rais huyo akiishi kwenye Ikulu hiyo
kama alivyokuwa ameahidi. “Tayari tumempokea Rais wetu na wananchi wana
furaha isiyo na kifani,” alisema Seganje.
Wakizungumza mapema wiki iliyopita, baadhi ya wakazi wa Chamwino
Ikulu walisema itakuwa ni faraja kubwa kwa Rais kuishi kijijini hapo.
Alice Chidong’oi alisema Dk Magufuli ni kiongozi anayeonesha nia ya
dhati ya kuwatumikia watu wake kwa kujali zaidi wanyonge kama ilivyokuwa
kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
“Tunaamini akiishi hapa atakuwa sehemu ya jamii ya Wana Chamwino na
hilo litasaidia hata kuboreshwa kwa huduma za jamii ikiwemo maji,”
alisema Chidong’oi. Alisema hiyo itakuwa fursa nzuri kwa wakazi wa eneo
hilo kufanya biashara, kwani uwepo wake ndani ya wilaya hiyo utaongeza
idadi ya wageni.
Mkazi mwingine, Stanley Richard, alisema vijana wa Chamwino wanapenda
kazi na Dk Magufuli akiwa hapo itakuwa ni kazi tu. “Ni mtu ambaye
anapenda kazi na sisi vijana tunapenda kufanya kazi, tutampa ushirikiano
mkubwa katika kipindi chote atakachokuwa madarakani,” alisema.
Alisema alifurahi alipochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwani alijua nchi imepata kiongozi ambaye yuko tayari kuwaletea
wananchi wake mabadiliko. Tayari Serikali mkoani hapa imepiga marufuku
kufanyika kwa mikutano ya hadhara na maandamano wakati wa vikao vya
Bunge vikiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, alisema amri hiyo ya kuzuia
mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa bado inaendelea ili
kuweka utulivu muda wote wa vikao vya Bunge.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Bunge, kesho Alhamisi, Bunge
litapokea na kuthibitisha kwa kupiga kura jina la Waziri Mkuu wa 11 wa
Tanzania ambalo Dk Magufuli atakuwa ameliwasilisha kwa Spika Job Ndugai.
Kwa hiyo, Dk Magufuli atakuwa ametua mjini hapa akiwa na siri yake
moyoni ya nani atakuwa Waziri Mkuu wake kwa miaka ya mwanzo ya utawala
wake inayokoma mwaka 2020.
Mbali ya kutoa jina la Waziri Mkuu, Dk Magufuli anatarajia
kulihutubia Bunge, Ijumaa alasiri baada ya kuwa amemwapisha Waziri Mkuu
asubuhi. Hotuba yake itakuwa dira ya utawala wake kwa miaka mitano
ijayo.
Pichani juu msanii wa nyimbo za asili ya Kitanzania Batarokota akiwa katika Hoteli ya Misana aliyofikia jijini Mwanza..
MSANII wa nyimbo za asili ya Kitanzania Batarokota siku ya jumatatu ijayo saa 11:30 jioni anatarajia kuongea kwa njia ya simu live kutoka Mwanza katika kipindi cha Africa Sana kinachorushwa na radio Bahari FM kutoka Zanzibari. Msanii Batarokota atakuwa na maojiano na mwandishi wa Bahari FM Joan Donisya Thimas maharufu saut ya Black Sugar ndani ya mawimbi ya 97.3 Bahari FM. Jumatatu hiyo Batarokota ataongea moja kwa moja kutoka Jijini Mwanza aliko kwa sasa kwa maandalizi ya sikuu za mwishoni mwa mwaka 2015 kaa mkao wa kula kupata habari za Batarokota na ujio wa mwaka 2016.
PAMBANO la kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi
mwaka 2018 kati ya timu ya soka ya Tanzania `Taifa Stars’ dhidi ya
Algeria, linalotarajiwa kupigwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
limekuwa gumzo miongoni mwa mashabiki wa soka ndani na nje ya nchi.
Aidha, idadi kubwa ya mashabiki katika `vijiwe’ vya soka, wameonesha
dhamira ya dhati ya kutaka kuiunga mkono Stars. Ujio wa Mbwana Samatta
na Thomas Ulimwengu wa Stars wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na pia taarifa za Rais, Dk John Magufuli
kuwa atajitokeza kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania `Mwanzo Mwisho’,
kwa pamoja vimechangia kuongeza hamasa ya mchezo huo.
Samatta na Ulimwengu wametoka kuweka historia ya kuwa wa wanasoka wa
kwanza wa Tanzania kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya
klabu yao kufanya hivyo mwishoni mwa wiki, huku Samatta akiongeza taji
jingine la ufungaji bora.
Aidha, kwa Magufuli, hilo litakuwa pambano lake la kwanza kushuhudia
akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu alipoapishwa
kuchukua nafasi ya Rais Jakaya Kikwete, mwanamichezo aliyeondoka
madarakani baada ya kumaliza muda wake wa uongozi kwa mujibu wa Katiba
ya nchi.
Tayari waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Mali, Keita Mahamadou,
Diarra Bala, Niare Drissa Kamory na mwamuzi wa akiba Coulibaly Harouna
wameshawasili nchini tangu jana asubuhi, huku mtathimini wa waamuzi
Attama Ibrahim Boureima kutoka nchini Niger naye akiwa tayari nchini
tangu juzi usiku.
Reading 1, First Kings 17:10-1610 So he went off to Sidon. And when he reached the city gate, there was a widow gathering sticks. Addressing her he said, 'Please bring a little water in a pitcher for me to drink.' 11 She was on her way to fetch it when he called after her. 'Please', he said, 'bring me a scrap of bread in your hand.' 12 'As Yahweh your God
lives,' she replied, 'I have no baked bread, but only a handful of meal
in a jar and a little oil in a jug; I am just gathering a stick or two
to go and prepare this for myself and my son to eat, and then we shall
die.' 13 But Elijah
said to her, 'Do not be afraid, go and do as you have said; but first
make a little scone of it for me and bring it to me, and then make some
for yourself and for your son. 14 For Yahweh, God of Israel, says this: Jar of meal shall not be spent, jug of oil shall not be emptied, before the day when Yahweh sends rain on the face of the earth.' 15 The woman went and did as Elijah told her and they ate the food, she, himself and her son. 16 The jar of meal was not spent nor the jug of oil emptied, just as Yahweh had foretold through Elijah.
Responsorial Psalm, Psalms 146:7, 8-9, 9-10
7 gives justice to the oppressed, gives food to the hungry; Yahweh sets prisoners free. 8 Yahweh gives sight to the blind, lifts up those who are bowed down. 9 Yahweh protects the stranger, he sustains the orphan and the widow. Yahweh loves the upright,but he frustrates the wicked. 10 Yahweh reigns for ever, your God, Zion, from age to age.
Gospel, Mark 12:38-44
38 In his teaching he said, 'Beware of the scribes who like to walk about in long robes, to be greeted respectfully in the market squares, 39 to take the front seats in the synagogues and the places of honour at banquets; 40 these are the men who devour the property of widows and for show offer long prayers. The more severe will be the sentence they receive.' 41
He sat down opposite the treasury and watched the people putting money
into the treasury, and many of the rich put in a great deal. 42 A poor widow came and put in two small coins, the equivalent of a penny. 43 Then he called his disciples and said to them, 'In truth I tell you, this poor widow has put more in than all who have contributed to the treasury; 44 for they have all put in money they could spare, but she in her poverty has put in everything she possessed, all she had to live on.'
Reading 2, Hebrews 9:24-28
24 It is not as though Christ had entered a man-made sanctuary which was merely a model of the real one; he entered heaven itself, so that he now appears in the presence of God on our behalf. 25 And he does not have to offer himself again and again, as the high priest goes into the sanctuary year after year with the blood that is not his own, 26
or else he would have had to suffer over and over again since the world
began. As it is, he has made his appearance once and for all, at the
end of the last age, to do away with sin by sacrificing himself. 27 Since human beings die only once, after which comes judgement, 28 so Christ too, having offered himself only once to bear the sin of many, will manifest himself a second time, sin being no more, to those who are waiting for him, to bring them salvation.
Feastday: November 6 Patron of political prisoners, imprisoned people, prisoners of war, and captives, women in labour, as well as horses
Death: 559
According to unreliable sources, he was a Frank courtier
who was converted by St. Remigius, refused the offer of a See from his
godfather, King Clovis I, and became a monk at Micy. He lived as a hermit at Limoges
and was rewarded by the king with all the land he could ride around on a
donkey in a day for his prayers, which were believed to have brought
the Queen through a difficult delivery safely. He founded Noblac
monastery on the land so granted him, and it grew into the town of
Saint-Leonard. He remained there evangelizing the surrounding area until
his death. He is invoked by women in labor and by prisoners of war because of the legend that Clovis promised to release every captive Leonard visited. His feast day is November 6.
Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili ya 32 ya Mwaka B wa Kanisa. - EPA
Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican,
ninakuleteeni tafakari Neno la Mungu lililo taa na mwanga wa maisha
yetu. Tayari tuko ukingoni mwa mwaka wa Kanisa, ni Dominika ya 32 ya
mwaka B wa Kanisa. Mama Kanisa ametuwekea Neno likitualika kujitoa na
kujiaminisha katika Bwana bila kujibakiza, tukiwa na matumaini na kwa
namna hiyo tutajaliwa yale yote mema yatokayo kwa Mungu. Ujumbe huu
tunaupata kwa mifano hai ya wajane wawili wanaokubali mpango wa Mungu na
kutoa kile chote walichokuwanacho, kinyume na matajiri. Matokeo ya
tendo lao jema wanakirimiwa baraka tele katika maisha yao.
Katika Somo la kwanza tunamwona Nabii Eliya akimkimbia mfalme Ahab
ambaye alitaka kumwangamiza. Nabii anapokimbia anakutana na mama mjane
ambaye yuko katika taabu ya njaa! Nabii akitambua taabu ya mama huyu
lakini pia akiwa na tumaini katika Bwana, anamwomba maji na kipande cha
mkate. Mama huyu alikuwa na unga kidogo kiasi cha kutosheleza siku moja
kwa ajili yake na mwanaye, na baada ya hapo kadiri ya mjane huyo basi
wangekufa! Lakini kwa sababu ya tumaini kuu na akisikiliza sala ya
msisitizo ya Nabii Eliya anakubali kutoa kila kitu. Kwa ufadhili huu
alioufanya kwa Nabii wa Mungu, mjane huyu anapata chakula cha
kutosheleza maisha yake mpaka njaa itakapoisha katika nchi ile.
Mpendwa mwana wa Mungu, ukarimu na tumaini la mjane huyu ndio unaozaa
matunda mema. Matunda haya ni baraka na amani itokayo kwa Mungu. Ni
alama ya kwamba Mungu huwajali walio maskini ambao wanamkimbilia na
kumtumaini daima katika maisha yao. Mungu huwajali wale wote ambao
wanakubali kushirikisha vipaji vyao na kugawana mali zao na wengine
walio wahitaji. Jaribu kuwa mkarimu kwa Mungu utaona matunda yake!
Ewe ndugu msikilizaji, bado tunaendelea na sehemu ya barua kwa
Waebrania ambayo leo yatufundisha kwa msisitizo, tofauti iliyopo kati ya
Kuhani mkuu wa kweli yaani Yesu Kristo na makuhani wengine. Yesu Kristu
anatolea sadaka yake si katika madhabahu yaliyotengenezwa kwa mawe bali
ukuhani wake ni wa madhabahu ya mbinguni ambayo hayakujengwa kwa mikono
ya wanadamu. Kuhani Mkuu Yesu Kristo hutolea sadaka mara moja na
hutosheleza maisha yote kwa kuondoa dhambi na kutakasa mioyo ya watu,
tofauti na sadaka za makuhani wa Agano la Kale ambazo hazikumaliza
shughuli ya kuwatakasa watu, kumbe iliwapasa kurudia kila mwaka! Basi
mwaliko kwetu ni kumfuasa Bwana kwa kushiriki sadaka ya Misa kwa ajili
ya wokovu wetu.
Katika Injili, Mtakatifu Marko akinukuu mafundisho ya Bwana anakazia
kujitoa bila kujibakiza kama mama mjane aliyetoa sadaka senti mbili
ambazo ilikuwa ndiyo hazina yake! Anatoa yote bila kuogopa kwa maana
analo tumaini katika Bwana ambaye ni mgawaji wa mapaji yote. Mjane huyu
ni kinyume na watu wengine ambao hutoa ziada na si mali hasa inayotoka
katika mioyo yao! Mpendwa yafaa kujitazama moyoni wapi ulipo katika
makundi haya mawili! Kama uko katika kundi la mjane basi unayo heri ya
milele na uishikilie kwa furaha maana ni zawadi toka kwa Bwana.
Basi mpendwa ndugu unayetafakari nami, jaribu kujikuza katika sala
ukiomba fadhila ya ukarimu katika maisha yako. Kula, ishi, cheka na
zungumza na wengine kwa furaha daima.
Tumsifu Yesu Kristo. Tafakari hii imeletwa kwako na Pd Richard Tiganya C.PP.S.
Tatizo la vifo vya wajawazito na watoto wachanga
linasababisha majonzi makubwa kwa jamii lakini pia linaleta ongezeko la
watoto waliodumaa, wagonjwa, watoto wa mitaani kupunguza nguvu kazi ya
taifa.
Ili taifa lisonge mbele kimaendeleo halina budi kuimarisha huduma
za afya kwa wananchi , ili kupunguza vifo vya wajawazito, wazazi na
watoto wachanga kwa lengo la kuepusha matatizo hayo.
Takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii za mwaka 2014
zinaonyesha kwamba Tanzania ni nchi ya saba duniani kwa idadi kubwa ya
vifo vitokanavyo na uzazi, ikikadiriwa kuwa wajawazito karibu 7,900
hufa kila mwaka, huku wastani wa watoto wachanga 40,000 wakipoteza
maisha kila mwaka kabla ya kutimiza mwezi mmoja baada ya kuzaliwa.
Kama vile haitoshi inakadiriwa kwamba watoto 100,000 hufa kila
mwaka kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano.Kadhalika wengine 50,000
huzaliwa wakiwa wafu kutokana na sababu mbalimbali ambazo iwapo jitihada
za makusudi zingechukuliwa mapema, zaidi ya asilimia 45 ya vifo hivyo
visingezuiliwa.
Pia asilimia 44 ya wasichana wanaofikisha umri wa miaka 19 nchini wanapata ujauzito, haijalishi wapo shuleni au nje ya masomo.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 asilimia 54 ya
Watanzania ni watu walio chini ya miaka 20 na hii inatafsirika kuwa
takribani miaka 15 hadi 20 ijayo idadi kubwa ya vijana wataingia katika
umri wa uzalishaji mali na kuwa nguzo ya kiuchumi.
Kutokana na hali hiyo makala hii inawapa changamoto wateule wa
nafasi za urais na ubunge kuweka wazi namna watakavyo lishughulikie
tatizo kubwa la vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
Ukweli ni kwamba viongozi hawa wanakwenda kufunga mkataba kati yao
na raia kwa miaka mitano ijayo hivyo kazi yao ni kutafuta ufumbuzi wa
kumaliza tatizo hili.
Waliochaguliwa wafahamu kuwa afya ya mama ni muhimu kama ilivyo ya
mtoto wajue kuwa tangu mwanzo suala hili halijapewa kipaumbele cha
kutosha kutokana na kutokuwapo mfumo bora wa kutoa huduma kikamilifu.
Ni vyema sasa wabunge na mawaziri watakaounda serikali ya awamu ya
tano wakatueleza kwa kina namna gani watakavyosimamia na kuhakikisha
uzazi salama wa mpango unavyosimamiwa ili kuhakisha kuwa adha ya kufa
wakati wa kujifungua inamalizika ama kuondoka.
Aidha viongozi waieleze jamii vipaumbele vyao kwenye afya ya mama
na mtoto ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali kuona suala hilo kuwa na
umuhimu wa kipekee na kulipa kipaumbele zaidi ikilinganishwa na masuala
mengine.
Tafiti mbalimbali zilizofanywa na mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali ya DSW, Marie Stopes Tanzania, Pathfinder International,
Chama cha Maelezi Bora (Umati) na HDT zinabainisha kuwa tatizo la uzazi
wa mpango ni kubwa.
Tafiti za mashirika hayo zinaonyesha kuwa mimba zisizotarajiwa
husababisha uwezekano mkubwa wa vifo vya mama na mtoto kwa asilimia tisa
ya vifo vinavyotokea nchini.
Angalizo linatolewa kuwa kiwango hicho kinaweza kuongezeka zaidi
iwapo hatua za makusudi hazitatolewa katika jamii kwa hiyo ni suala
ambalo wabunge wanatakiwa kulitizama na kulipa umuhimu wa kipekee.
Uzazi wa mpango ni mkakati muhimu wa kuwasaidia wanawake kupanga
muda wa kutosha kati ya kizazi kimoja na kingine, kuzuia mimba katika
umri mdogo na kuepuka mimba zisizotarajiwa.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, (WHO) gharama za kuzuia
ujauzito ni za chini zaidi kuliko za matibabu yanapotokea wakati wa
kujifungua.
Kwa hiyo uzazi wa mpango unazipa familia au mtu binafsi uwezo wa
kuchagua ukubwa wa familia ambayo anaimudu, kuwekeza katika elimu na
makuzi ya kila mtoto na kubaki na fedha za ziada hatua inayoweza
kuchangia kukuza uchumi wa taifa.
Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake Moke Magoma, anasema kuna
uwezekano mkubwa wa Tanzania kupiga hatua za haraka kimaendeleo iwapo
jamii itapata uelewa wa kutosha kuhusu uzazi wa mpango.
“Ni muhimu sana kuwepo kwa huduma za afya ya mjamzito na mtoto
mchanga, ambayo katika uhalisia wake inajidhihirisha kwa kila aliye hai
sasa amepatikana kupitia mama yake kuwa mjamzito” anasema Dk. Magoma.
“Uzazi wa mpango ni muhumu kwa kuwa wanaweza kudhibiti na kupanga
idadi ya watoto, kuendeleza na kutunza familia kitaaluma, lishe na
wakati huo wakafanya kazi wanazozitaka na kushiriki katika maamuzi ya
kiuchumi na kisiasa”
Daktari Magoma anasema uzazi wa mpango ni njia bora zaidi katika
afya ya mama na mtoto na kwamba mbinu za kitaalamu za uzazi wa mpango
hazina madhara kama baadhi ya watu wanazovumisha na kuwatia hofu
wananchi.
Naye Dk. Msiima Mushumba,kutoka shirika la Marie Stopes
Tanzania,anasema jamii inapaswa kutambua kuwa kuzaa watoto wengi bila
mpangilio ni kuhatarisha maisha ya mama, watoto na kudumaza uchumi wa
taifa.
Anasema kwa wastani familia inapaswa kuzaa watoto wasiozidi watano
na kwamba kuanzia mimba ya sita na kuendelea huitwa mimba hatarishi
ambapo anaitaka jamii kufuata njia za uzazi wa mpango.
Kadhalika anabainisha kuwa wananchi ambao hawakusoma wanazaa zaidi
kuliko waliosoma kwa kuwa wengi wao hutambua umuhimu wa kuzaa kwa mpango
kuliko ambao hawakusoma.
Dk. Mushumba, anasema jitihada za makusudi zinahitajika kupitia
serikali, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na jamii kwa ujumla
kuhakikisha huduma za uzazi wa mpango zinawafikia wanawake wote nchini.
RAIS John Magufuli, aliyeanza kazi juzi kwa kumteua Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, George Masaju, baada ya kumuapisha jana amefanya ziara ya
kushtukiza katika ofisi za Wizara ya Fedha, Hazina.
Tofauti na ziara za viongozi wengine wakiwemo mawaziri waliowahi
kuongoza ofisi hiyo, ambao huingia katika vyumba vya mikutano au ofisi
za viongozi, Dk Magufuli yeye alianza kuingia katika ofisi za watumishi
wa kawaida.
Dk Magufuli aligeuka kivutio kwa wananchi, pale alipotoka katika
lango kuu la Ikulu Dar es Salaam kwa miguu kwenda wizarani hapo kupitia
njia ambayo imekuwa ikitumiwa zaidi na wananchi.
Wizara hiyo mbali na kuwa karibu na Ikulu, lakini imezungukwa na
ofisi nyingi, ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Ofisi Ndogo ya
Bunge na mara kwa mara nje kuna kawaida ya kuwa na wananchi na magari
mengi yenye madereva wa maofisa wanaofika wizarani hapo na wengine
katika ofisi nyingine kwa shughuli mbalimbali.
Baada ya kuingia katika ofisi hizo, Dk Magufuli alianza kufungua
milango ya ofisi za watumishi hao na kuwasalimia aliowakuta na kuhoji
pale alipokuta meza haina mtendaji.
Katika hatua hiyo, Dk Magufuli alishangazwa kukuta meza sita kati ya
nane katika moja ya ofisi hizo, hazina watumishi akalazimika kuuliza
majina ya watumishi husika na alipoambiwa walikuwepo, akahoji
walikokwenda akajibiwa walikwenda kunywa chai. Huku akionekana
kutoridhishwa na majibu hayo, Dk Magufuli alitikisa kichwa huku akisema
“wameenda kunywa chai eee!” na kuondoka ofisini hapo kwenda kwenye ofisi
za viongozi wa wizara hiyo.
Alipoingia ndani, alifanya kikao cha muda mfupi na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha, Dk Servacius Likwelile pamoja na makamishna wa fedha na
alipotoka taarifa za wizara hiyo zilieleza kuwa Dk Magufuli ameagiza
watumishi wa Wizara hiyo inayosimamia Mamlaka ya Mapato (TRA),
kuhakikisha wanaongeza kasi ya ukusanyaji mapato, na akaelekeza hasa kwa
wafanyabiashara wakubwa.
Mbinu aliyotumia Dk Magufuli, ni ya kitawala ambapo viongozi
husimamia wizara kwa kufanya ziara za ghafla, au kutembelea maeneo ya
watumishi bila kutoa taarifa, tena bila kufuata utaratibu wowote. Lengo
lake mara nyingi ni kujulia hali ya watumishi na matunda yake ni
kuongeza ari ya kufanya kazi, kuhimiza na kusisitiza malengo ya taasisi.
*Kuapishwa kwa Masaju
Awali kabla ya kufanya ziara hiyo, Dk Magufuli alimuapisha Masaju
kuendelea kushikilia nafasi hiyo, ambapo Mwanasheria Mkuu huyo aliahidi
kuendelea kusimamia kesi mbalimbali dhidi ya Serikali ili kuokoa fedha
za umma.
Uapisho huo ulifanyika Ikulu na kuhudhuriwa na watu mbalimbali
akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Othman Chande,
Spika wa Bunge, Anna Makinda na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest
Mangu.
Masaju alisema ni tumaini lake kuwa wananchi wataendelea kutii sheria
za nchi, ili kudumisha amani na mshikamano kama ilivyokuwa wakati wote
huku Serikali ikiendelea kuimarisha utii wa sheria.
“Serikali shughuli yake ya msingi ni kusimamia utekelezaji wa sheria
na yenyewe ina jukumu la kusimamia amani. Nashauri ushirikiano
uliotolewa wakati wa Uchaguzi Mkuu uendelee kudumishwa,” alisema Masaju.
Masaju alisema Serikali inaokoa fedha nyingi za umma kwa kushinda
kesi dhidi yake na kwamba inajitahidi kuendesha kesi zake kwa weledi,
huku akitoa mfano wa mashauri 34 ya kesi za uchaguzi ya kupinga matokeo
zilizofunguliwa mwaka 2010, ambazo Serikali ilizishinda zote.
Alishukuru kupatikana kwa Serikali mpya kwa amani na kwa kuzingatia
maelekezo ya sheria na kuomba hali hiyo iendelee ili shughuli mbalimbali
ziendelee hasa zile za kujenga uchumi na za kijamii. Alitaka amani ya
nchi ipewe kipaumbele na kuonya kuwa ikivurugika hakuna kazi
itakayofanyika na kusisitiza amani ndiyo itakayodumisha uchumi wa nchi.
Most faithful St. Dymphna, you remained true to your baptismal promises to the very end. You are, therefore, honored, known, and loved after 1,400 years by people you have aided all over the world. We do not know how long or short atimeis left to us of thislifehere, but help us in any case to be faithful toGodto the end. Please gain for us thegraceto live one day at atimeas if each were to be our last. Amen.
Feastday: November 4 Patron of learning and the arts.
Death: 1584
Charles was the son of Count Gilbert Borromeo and Margaret Medici, sister of Pope Pius IV. He was born at the family castle of Arona on Lake Maggiore, Italy on October 2. He received the clerical tonsure when he was twelve and was sent to the Benedictine abbey of SS. Gratian and Felinus at Arona for his education.
In 1559 his uncle was elected Pope Pius IV and the following year, named him his Secretary of State and created him a cardinal and administrator of the see of Milan. He served as Pius' legate
on numerous diplomatic missions and in 1562, was instrumental in having
Pius reconvene the Council of Trent, which had been suspended in 1552.
Charles played a leading role in guiding and in fashioning the decrees
of the third and last group of sessions. He refused the headship of the
Borromeo family on the death of Count Frederick Borromeo, was ordained a priest in 1563, and was consecrated bishop of Milan the same year. Before being allowed to take possession of his see, he oversaw the catechism, missal, and breviary called for by the Council of Trent. When he finally did arrive at Trent (which had been without a resident bishop
for eighty years) in 1556, he instituted radical reforms despite great
opposition, with such effectiveness that it became a model see. He put
into effect, measures to improve the morals and manners of the clergy
and laity, raised the effectiveness of the diocesan operation,
established seminaries for the education of the clergy, founded a Confraternity of Christian Doctrine for the religious instruction of children
and encouraged the Jesuits in his see. He increased the systems to the
poor and the needy, was most generous in his help to the English college at Douai, and during his bishopric held eleven diocesan synods and six provincial councils. He founded a society of secular priests, Oblates of St. Ambrose
(now Oblates of St. Charles) in 1578, and was active in preaching,
resisting the inroads of protestantism, and bringing back lapsed
Catholics to the Church. He encountered opposition from many sources in
his efforts to reform people and institutions.
He died at Milan on the night of November 3-4, and was canonized in 1610. He was one of the towering figures of the Catholic
Reformation, a patron of learning and the arts, and though he achieved a
position of great power, he used it with humility, personal sanctity,
and unselfishness to reform the Church, of the evils and abuses so
prevalent among the clergy and the nobles of the times. His feast day is November 4th.
Ninakualika
katika tafakari yetu tukiwakumbuka marehemu wote. Kila mwaka tarehe 2
Novemba na zaidi sana mwezi Novemba ni siku na wakati ambao Mama Kanisa
anatualika kwa ajili ya kuwaombea marehemu walioko toharani. Kwa kawaida
siku zote mama Kanisa anasali kwa ajili ya marehemu mmoja mmoja au
kikundi lakini leo anasali kwa ajili ya Kanisa zima la wateswa lililoko
toharani. Huo ndio utajiri wa Kanisa linapogawa mastahili ya Msalaba wa
Kristu kwa wahitaji walioko safarini kuelekea mbinguni.
Picha juu ni Mwandishi wa habari Paskal Linda wa www.batarokota.blogspot.com
Siku ya Marehemu wote!
Mwanafalsafa John Mbiti alisema “Niko
kwa sababu tuko na kwa vile tuko, kwa hiyo niko ” Sentesi hii
yanitafakarisha na kunisaidia kuhisi uwapo wa mwingine pembeni mwangu
aliye mhitaji na hivi yaonesha hitaji la jumuiya. Katika siku ya leo
Kanisa lahisi uwapo wa wahitaji ndio marehemu wote, ndio waliolala
toharani wakitakaswa ili waingie mbinguni. Kanisa lahisi na kutekeleza
ule muunganiko uliopo kati ya marehemu (kanisa la wateswa), watakatifu
wa mbinguni (kanisa la washindi) na kanisa la wapiganaji ndio sisi na
hivi kwa pamoja ni kanisa moja familia ya Mungu. Fundisho tulilolisikia juu ya
muunganiko wa kanisa shindi, kanisa la wateswa na kanisa la mahujaji
linawekwa mbele yetu na Papa Paulo VI akisema “sisi twasadiki ushirika
wa waamini wote wa Kristo, wa wale walio bado safarini duniani, wa wale
waliokufa ambao wanapata utakaso, wa wale wenye heri ya mbingu, wote
pamoja hufanya Kanisa moja tu. Nasi twasadiki kwamba katika umoja huu,
mapendo ya huruma ya Mungu na ya watakatifu wake yasikiliza daima sala
zetu” (KKK 962) Ndiyo kusema kuwaombea marehemu ni sehemu ya imani yetu,
ni upendo kwa jirani tukiitikia injili ya Bwana ya kumsaidia aliye
katika taabu, aliyemhitaji. Kuwaombea marehemu ni kielelezo
kimojawapo cha imani yetu katika ufufuko, kwa maana kama hatusadiki
yakuwa Kristu alikufa na kufufuka imani yetu ni bure. Ni kutokana na
msingi huo twaamini kwamba wale waliolala usingizi katika Yesu Kristo
mfufuka, parapanda ya Mungu ikilia watafufuliwa kwanza nasi tuliosalia
tutanyakuliwa kwa kuwafuata wao.
Kuwaombea marehemu ni jambo la thamani na la imani ambalo si la leo
bali limekuwepo katika safari ya wokovu. Tunasoma daima katika kitabu
cha pili cha Wamakabayo kuwa Yuda kiongozi wa Wayahudi alichanga fedha
kwa kila mtu jumla drakma mbili elfu, akazipeleka Yerusalemu kutoa
sadaka ya dhambi. Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki kwa kuwa
aliukumbuka ufufuo wa wafu. Alifanya hili kwa sababu ya imani na kama
asingekuwa na imani kuwa wafu watafufuliwa ingekuwa upumbavu na kazi
bure kuwaombea marehemu. (Rej. 2Wak. 12: 43-45). Basi ndugu yangu mpendwa ninakualika
katika msingi uleule wa imani katika ufufuko, kusali daima sala hii
“raha ya milele uwape Ee Bwana na mwanga wa milele uwaangazie wapumzike
kwa amani, amina”. Ni Sala ya kujenga urafiki na marehemu walioko
toharani na hatimaye watakatifu wa mbinguni. Ni sala ambayo yatukumbusha
wapendwa wetu ambao wengine tuliwafahamu kwa karibu na hivi yatudai
wajibu wa kuomba huruma ya Mungu kwa ajili yao pasipo kukoma. Mama Kanisa ametuwekea Misa tatu kwa
ajili ya marehemu wote ili kwa njia hiyo marehemu wapate msaada wa
masitahili ya Kristo kwa njia sadaka yake ya msalabani. Anataka asiwepo
hata mmoja atakayekosa huruma na msaada wa Mungu. Katika Misa hizi tatu
injili zagusa Heri Nane njia ya utakatifu na habari ya ufufuko wa wafu
lililotumaini letu na imani yetu tunaposafiri kuelekea ukamilifu yaani
uzima wa milele ambao huja baada ya kifo. Tunasali na kutumaini kuwa,
kwa kifo maisha hayaondolewi ila hugeuzwa na kuwa maisha mapya, maisha
makamilifu. Basi mpendwa mwanatafakari, leo ni
wakati wa kusali na kuwatembelea waliolala kule makaburini ili
muunganiko katika sala ukamilishwe katika upendo unaoonekana katika
maisha ya watu. Yafaa pia kufunga kidogo kwa ajili ya wapendwa wetu ili
kuisimika sala yetu katika majitoleo ya Kristo mteswa na hatimaye uibuke
na ushindi wa Kristu mfufuka. Kumbukeni pia kujiombea wewe mwenyewe kwa
maana kwakukumbusha kujitayarisha kwa ajili ya safari ya kugeuzwa na
kuingia maisha mapya, maisha ya mbinguni.
Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea Makardinali na Maaskofu marehemu. - OSS_ROM
Jumanne
tarehe 3 Novemba 2015 majira ya saa tano katika Kanisa Kuu la
Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko, aliongoza Ibada ya Misa kwa
nia ya kuwakumbuka na kuwaombea Makardinali na Maaskofu wote waliofariki
mwaka huu. Katika kipindi hiki, Kanisa liliondokewa na Makardinali 15
, Patriaki I na Maaskofu 99 kwa idadi ya jumla. Barani Afrika Kanisa
limepoteza maaskofu 10 wakiwemo watatu kutoka Shirikisho la Baraza la
Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA.
Akitoa homilia kwa ajili ya Marehemu hao, Papa Francisco alisema leo
hii tunawakumbuka na kuwaombea ndugu hawa ambao walilipenda Kanisa kama
mchumba wao, na sasa tunamwomba Mungu wa huruma , awapokee katika
furaha kamili na umoja na Watakatifu. Papa
aliendelea kuwakumbuka marehemu akisema kuwa ni wajibu kutoa shukrani
kwa ukarimu wao wa kuitikia wito Mtakatifu, kama ilivyotajwa katika neno
la Injili na hasa kwanza kabisa kwa ajili ya uongozi wao na huduma yao.
Na kwamba katika wakati huo wa kutolea sala na maombi kwa ajili ya
ujira wao walioahidiwa kama "watumishi wema na waminifu" kama
ilivyoandikwa katika Injili (Mathayo, 25,14-30), pia sisi tulio bado hai
tumeitwa kufanya upya uchaguzi wetu katika kulitumikia Kanisa.
Papa alieleza na kusisitiza juu ya kutumikia na si kutumikiwa,
akirejea tukio la Yesu kuwaosha miguu wanafunzi wake . Amesema Yesu
mwenyewe alionyesha wazi kwamba, kuwa kiongozi si kuwa myapala lakini
ni kutumikia (Marko 10:45), na kwamba mtu hawezi kuwa mchungaji mwema
kama hayuko tayari kutoa hata uhai wake kwa ajili ya kondoo wake.
Anayekubali kutumikia anakuwa mtu wa kutoa, si katika vitu tu lakini
hata nafsi yake. Papa aliendelea katika macho ya kidunia mtu huyo
huonekana kama mtu anayepoteza, lakini kwa undani wake, kwa
anayeyapoteza maisha kwa ajili ya upendo wake Kristo, huwa na nguvu za
kukishinda kifo na kuupa ulimwengu uzima. Anayetumikia huokoa. Kinyume
chake, asiyeishi kwa ajili ya kutumikia wengine huyo hajiwekei dhamana
kwa maisha ya baadaye.
Papa Francisco aliendelea kuzungumzia upendo wa Mungu, kwamba "Mungu
aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae pekee ili ulimwengu uweze
kukombolewa naye. Na viongozi wa Kanisa na waamini wakiongozwa na upendo
huo hupata hamu ya kutenda kama alivyo fanya Bwana wao, kuyaokoa maisha
ya wengine. Upendo wa Mungu usiokuwa na kipimo wala mwisho, upendo
unaoendelea kuwepo hata miisho ya dunia. Na kama inavyo dhihirishwa
katika Mkate wa Ekaristi unaotolewa kwa ajili ya wokovu wetu ,
uliopatikana kutoka katika kifo na kutupatia maisha yaliyojazwa na
matumaini.
Na kwamba wakati huo wa matoleo ya Misa kwa ajili ya Wapendwa
Makardinali na Maaskofu,pia inakuwa ni wakati wa kujiombea hata sisi
tulio bado hai, kuomba neema ya kuimarishwa, kama Mtume Paulo
anavyohimiza: kuyageuza mawazo yetu kwa mambo yaliyo ya juu na siyo kwa
yaliyo ya chini (Colosai 3.2); kwa ajili ya upendo wa Mungu na jirani,
badala ya kujali tu mahitaji yetu.
Papa amesisitiza na kutoa mwaliko kwa watu wote, kutojiwekea hazina
hapa duniani lakini juu mbinguni. Asema huo ndiyo msingi wa kuyafuata
maisha ya Pasaka ya Bwana, yaliyo leta ukombozi na kutuweka huru dhidi
ya mashaka na wasiwasi unaoletwa mambo ya kidunia, ambayo hupita na
kuteketea kabisa ndani ya hewa nyembamba. Na kwamba maisha hayo hayadai
zaidi , ila kwenda kwake tu, ambako kuna maisha, wokovu, ufufuo na
furaha. Huko ndiko tutakuwa watumishi wake kulingana na mapenzi yake, si
kama watwana lakini kama wana wake wapendwa walioyatoa maisha yao kwa
ajili ya wokovu wa dunia.
Na siku ya Jumatatu jioni Papa Francisco alitembea eneo la makaburi
lililoko chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ambako alitolewa sala
zake binafsi kwa ajili ya Roho za marehemu watangulizi wake katika Kiti
cha Askofu wa Rome . Imekuwa ni kama utamaduni wa Mapapa katika siku hii
ya kuwakumbuka na kuwaombea marehemu, Papa huteremka chini katika eneo
la Makaburi ya watangulizi wake kutolea sala zake binafsi, kuomba huruma
ya Mungu