Hakika Muujiza mkubwa
kuliko yote wa Bwana Mtume S.A.W ni hii Quraan
tukufu ambayo haibadiliki kama vitabu vyinginevyo na kila zama
zikenda ndio inafahamisha zaidi kinyume na vitabu
viandikwavyo na mwanadamu ambavyo kila siku zikipita
hubidi kufanyiwa marekibisho fulani ili viweze kwenda
na wakati.
Muujiza mkubwa wa
Bwana Mtume Muhammad S.A.W ni
Quraan tukufu lakini kuna Miujiza
mengi aliifanya ingawa hayadhukuriwi lakini hayo aliyoyatenda
yalikuwa ni Miujiza hata kwa
kule kusema kutakuwa na jambo
fulani litakuja kutokea huo nao
ni Miujiza, kwani utapoangalia Taarifu nilisema Miujiza hudhihiri katika baadhi ya
mikono ya
Mitume, hiyo ni sawa na
hata kule kutabiri kuelezea kitachotokea nako huko kunakuwa Miujiza.
Wasomi mbali mbali waliweza kuyanukulu hayo akiwemo Ibn Taymiyyah, Al-Jawab as-Sahih li man Baddala Din al Masih iliyoelezwa na Ibn Kathir, Tarikh na Adh-Dhahabi, Tarikh al-Islam , Ibn Hajar Fathul Bari {6/582). Vile vile rudia Khayru-d-Din Wanili, Mujazat al-Mustapha
(kopi ya 3, iliyochapishwa Maktaba as-Sawadi Jeddah).
Vitabu vingi vimeelezea juu ya Miujiza ya
Bwana Mtume Muhammad S.A.W na baadhi ya miujiza ni kama ifuatayo:
·
Kupasuka kwa mwezi
·
Maji
kuchuruzika katika pacha ya vidole
vyake
·
Kuongeza chakula kidogo kuwa chingi
·
Jiwe
kumsalimu
·
Kuzungumza kwa mguu wa kondoo aliyona
sumu
·
Mti
kutembea na kumfikia yeye Bwana Mtume
·
Kondoo tasa kumfanya atoe maziwa
· Kulirejesha jicho la Qatidah bin an-Numan kwa mkono baada
ya kudondoka na kurejea jicho
hilo hali ya
kawaida
· Alilitemea mate jicho la Syd
Ali baada ya kuvimba na jicho
hilo kurudia hali
yake ya kawaida
· Kubashiri kabla ya tokeo la vita vya Badr kwa kusema
hapa ndipo watapokufa wanaomshirikisha
"Allah" na kuwataja
baadhi yao kwa majina
·
Alibashiri kuwa utajiri wa Chosroes utaangukia
mikononi mwa waislam na utajiri
huo utatumiwa kwa manufaa ya
waislam, pamoja na kusema kuwa
Wa-Farsy na Wa-Roma mali zao zitaangukia
mikononi mwa waislam na Suraqah
bin Malik atavaa kivazi cha Chosroes
·
Alifahamisha kuwa Hassan
bin Ali atapatanisha makundi
yaliokuwa yaki talifiana baina ya waislam
·
Alieleza kuwa Sa’d bin Abi Waqqas ataishi
na hivyo vikundi vilivyokuwa viki talifiana na baadhi yao watafaidika na wengineo watadhurika
·
Alibashiri siku aliyokufa Najash wa Ethopia
na siku ya
kuuwawa kwa al-Aswad al-Ansi akiwa
yupo Yemen
·
Alibashiri kutekwa kwa Turks,
kutekwa kwa Iraq na Syria
·
Alieleza kuwa Ammar bin Yassir atauwawa na wavamizi na
hapo taifa la kiislam litagawanyika katika makundi (madheheb) na kupigana
baina yao
·
Alibashiri kuwa Ruwayfi bin Thabit kuwa ataishi
umri mrefu na ikawa hivyo
·
Alibashiri kuanza kwa moto mkubwa kutokea
sehemu za Hijjaz yakawa hayo
·
Alifahamisha kuwa Thabit
bin Qays, kuwa ataheshimika na kusifiwa na atakufa
kama shahidi yakawa
hayo kwani alisifika na kuuwawa
sehemu ikijulikana kama al-Yamamah
·
Alibashiri juu ya misukosuko ya Sayyidna
Uthman RA na yakatokea
·
Aliwaeleza wakeze kuwa "Aliyemwepesi wa
kutoa sadaka kati yenu ndio
atayenifwata mwanzo, baada ya kufa
kwangu". Aliyekufa mwanzo akawa ni
Zaynab bint Jahsh (ra) huyu
ndio kati ya wake wa Mtume
aliyekuwa mwepesi wa kutasadak na
ndio aliyekufa mara tu baada
ya Bwana Mtume kufariki
·
Mtume
alimuelezea Anas kuwa atakuwa tajiri
na kuwa
na watoto wengi na vile vile
ataishi umri mrefu. Inafahamishwa kuwa Anas aliishi
zaidi ya miaka mia na
ziada, na hakutokea kati ya Ansar aliyekuwa
tajiri zaidi yake na aliwazika
watoto wake wa idadi ya 120 kabla
ya kutokea kwa Hajjaj nchini
Basra (sahih Bukhari
1982)
·
Aliomba moja kati ya Umar asilimu
kwa kuupa nguvu uislam na
Syd Umar Bin Khatab alisimu na uislam kushika
nguvu
·
Baridi ilishtadi na akamtuma Hudhayfa kwenda kufanya upelelezi akiwa hana nguo nzito
za kumzuia baridi na akaomba
awe hahisi baridi, na ikawa katika
kipindi chote alichotumwa baridi inavuma naye kutohisi
kabisa
·
Alimuombea Ibn Abass awe ndio kigingi cha elimu ikawa hivyo
·
Aliomba mvua kunyesha wakati wa
ukame, na wakati anaomba hayo kulikuwa shwari
mawingu kutoenekana na mara alipomaliza
dua yake mawingu yalijikusanya na mvua kuanza
kumiminika.
·
Aliwaombea Abu Talha na mkewe Umm Sulaym waruzukiwe kizazi chema pale walipokutana katika usiku, matokeo
yake alizaliwa Abdullah, na Abu Talha kupata
watoto wengine 9 na wote wakawa
wasomi
·
Alimuombea Umm Qays bint Muhsin dada wa Ukkasha aishi umri
mrefu haiaminiki kuwa alitokea mwanamke
kuishi umri mrefu au kutaokea mwanamke ataoishi umri mrefu zaidi
ya bibi huyu. Imepatikana kwa msaada wa
http://www.mawaidha.info/muujizawamtume.htm
Tunamuomba "Allah" atufanikishe
na haya
"Amin"