Nyimbo hapo juu ni ya kisukuma iliyopitwa na Mama Nyamoko akiwa na Msanii Batarokota.
Mwazirishi wa blogu hii ni Paskal Linda Mgundu maharufu Batarokota Pichani kushoto alizaliwa 1974 Kijiji cha Kigamboni katika Hospitali Teule ya Kigamboni Mkoa wa Temeke jijini Dar es salaam.
Batarokota kabila ni Msukuma kutoka kijiji cha Nyashigwe kilomita 35 kutoka jijini Mwanza kaskazini mwa nchi ya Tanzania.

Batarokota ana mke na watoto wanne na alifunga ndoa Jumamosi ya
tarehe 5/Machi/2011 katika kanisa Katoriki la Mtakatifu Partic la mjini
Morogoro,Batarokota alifunga ndoa na Sara Abed Linda.Na kabla ya
ndoa alifanikiwa kupata watoto wawili na wawili baada ya kufunga
ndoa.
Watoto wanne wa Batarokota wakwanza alizaa na mchumba wake wa
kwanza Saula Athony Kapama ambae kwa sasa ni marehemu aliyefariki tarehe
9/Agosti/2005 Sumve Matare kwa ajali ya Treni ya abiria iliyokuwa ikienda Dar essalaam, Saula Kapama alimwachia
Batarokota mtoto mmoja jina Ng`wibis Linda ambae alizaliwa Agosti 2000
katika Dispensary ya St Michael mtoto wa pili wa
Batarokota ni Shija Paskal ambae alizaliwa Desemba 2006 katika Hospital
ya Bugando jijini Mwanza, Batarokota alizaa mtoto na rafiki wake wa kike
Ruti Fidel Kanuti na Mtoto wa tatu wa Batarokota ni mtoto wa kike
Makrina Juliana ambae alizawa Novemba/ 2011 mjini Morogoro katika
Hospital ya Morogoro amezaa na mke wake Sarah Dile Linda na wanne ni
Telezia wa Yesu aliye zaliwa Desemba,2013
.
.
ELIMU
Batarokota amesoma shule ya msingi Igoma, nakumaliza shule 1990 na alifanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari 1991 katika shule ya sekondari Buswelu na kufanikiwa kumaliza mwaka 1994, baada kidato cha tano na sita Mweli Sekondari 1997.
Na mwaka 2010 Batarokota akufanikiwa kujiunga na chuo cha Powercomputer kilichopo jijini Mwanza- Tanzania na kuahitimu masomo kutengeneza computer, tovuti, blogu, grafics, Logo design, video editing and production baada ya kumaliza masomo ya computer Batarokota aliendelea na masomo ya Computer Nchini - Kenya katika chuo cha Moi na kumaliza masomo ya Diploma miaka 3, 2013.
Na picha chini Batarokota akiwa ofisini kwake anakofanyia shunguli za design na kutengeneza matangazo.
Batarokota amesoma shule ya msingi Igoma, nakumaliza shule 1990 na alifanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari 1991 katika shule ya sekondari Buswelu na kufanikiwa kumaliza mwaka 1994, baada kidato cha tano na sita Mweli Sekondari 1997.
Na mwaka 2010 Batarokota akufanikiwa kujiunga na chuo cha Powercomputer kilichopo jijini Mwanza- Tanzania na kuahitimu masomo kutengeneza computer, tovuti, blogu, grafics, Logo design, video editing and production baada ya kumaliza masomo ya computer Batarokota aliendelea na masomo ya Computer Nchini - Kenya katika chuo cha Moi na kumaliza masomo ya Diploma miaka 3, 2013.
Na picha chini Batarokota akiwa ofisini kwake anakofanyia shunguli za design na kutengeneza matangazo.
BATAROKOTA AMEFANYA SHOW MAENEO MENGI
Mwaka Novemba/1994 Batarokota alifanya show ya kuwaanga kidato cha nne
katika shule ya Buswelu Sekondari na Mgeni rasmi alikuwa Hayati Paulo
Bomani.Mwaka.
Julai/1996 Batarokota alialikwa katika show ya kusaka
mrembo wa
Kigamboni Miss Kigamboni katika ukumbi wa CCM kivukoni .Katika show
alikuwa wamealikwa wasanii Fune with Sanse kiongozi wao J- Mtambo na
kundi lake la POSOJU.
Mwaka Agosti/1998 ,Batarokota alikalibishwa na
kundi lake la G tha Dunia
katika ukumbi wa Liberty Hall jijini Mwanza, siku hiyo walikuwa
wanazindua singo ya wimbo wao 'upendo kwa mama' wasanii walio alikwa ni
Mr 2, Dr KB, BWV, Makamanda wa Gola, Daz P, na wengine wengi.
Mwaka, 2004
Batarokota akiwa na kungi la G THA Dunia alialikwa pamoja na
wasaniii H- Baba, J- Mo, Mr Paulo, Solo Thang, Vick Kamata na BWV.
katika kufanya show kubwa iliyo fanyika katika uwanja wa Ally Hassan
Mwinyi mjini Tabora show hii iliandaliwa na Zizou Entertnment.
Mwaka2004 ,
25,Desemba. Batarokota alialikwa yeye pamoja na msanii wa
nyimbo za kiasili Mama Nyamoko (Suzana Nyamoko), kwenye show ya
kuwaburudisha watu wa Geita siku ya kristimasi katika ukumbi wa Lake
View Hotel .
Mwaka 2013,Machi, Batarokota amefanya show aliyo alikwa
jijini Nairobi
katika ukumbi wa Brokriny uliopo Gethorai 44 onyesho hili lilifadhiriwa
na Princess Studio.
MAISHA
Kipaji cha Batarokota kilianza kuonekana toka akiwa shule ya msingi
Igoma mwaka 1987, Akiwa shuleni alikuwa akicheaza ngoma za asilia kwenye
kundi la shule na alikuwa akifundishwa na Mwalimu Matongo ambae
nimarehemu na Mwalimu Mayuyu ambae kwa sasa ni mwana kwaya wa Mtakatifu
Bakita katika kanisa la Romani Katoriki Igoma.
Wanafunzi ambao Batarokota
anakumbuka walio kuwa wanacheza wote ngoma ni Tasi Kosinatantine,
Paskal Makaka, Peter Makuke,Frimat Lyimo na wengine wengi.
Tarehe 9/Januari/1998, Batarokota alianziha kundi la mziki wa kurap
jijini Mwanza kwa jina G THA Dunia, kundi hili G Tha Dunia lilikuwa ni
moto wa kuotea mbali ambalo lilitikisha kanda ya Ziwa na lilikuwa
likiundwa na Paskal linda a.k.a Batarokota, Juma Hassani a.k.a Big D na
Danny Ngollo a.k.a Ngollo 2. Kundi hili lilifanikiwa kurekodi albamu
nchini Kenya ambayo ilikuwa ikiitwa '' ONE DAY'' ambayo ilirekodiwa
Agosti/1998 mjini Nairobi, Kenya katika studio ya SYNC SOUND STUDIO
chini ya Producer Mahamud Omari a.k.a Mr M O .Album hii ya ''One Day''
ilikuwa imajazwa na nyimbo kumi ambazo ni 'one day' jina la
albam, 'upendo kwa mama', 'kiama','ogopa 666' , 'nimzuri tu', 'baby
shake', 'wenyewe kwa wenyewe', 'watoto kwanza' , 'total balaa' na
'majonzi'.
Baada ya kukaa nalo kundi hilo Batarokota aliondoka na
kuachana na kundi hili 2004 na kwenda Dermank kwa ajili ya kufundisha
ngoma Wadenish.Tarehe15/,februari/2006 Batarokota alirejea kutoka Dermank na kuanzihsa
kundi jipya liitwalo Watu wa Gola liliko jijini Mwanza, alianzisha kundi
hili akiwa na Juma Hassani a.k.a Big D, Kundi hili Watu wa Gola
walifanikiwa kurekodi nyimbo mbili 'Tumerudi' na 'vichwa vya kale'
nyimbo hizi zimerekodiwa katika studio ya M.O. Record iliyopo Pasiasi
jijini Mwanza chini ya mtayarishaji Q the Don na Dj Zari.
TUZO KATIKA SANAA
Mwaka 2001 tarehe 4/Machi msanii Batarokota akiwa na kundi lake la G THA
Dunia,Kundi hili walifanikiwa kupata zawadi ya cheti cha ushindi wa
best single rap katika wimbo wa -upendo kwa mama- cheti hicho kilitolewa
na Gloryhood Music Award ya jijini Mwanza .
Mwaka 2004,Octoba 22-23, Batarokota alifanikiwakupta cheti cha kuudhulia
na kushiriki Music Crossroads Tanzania Workshops jijini Mwanza.
Mwaka 2014 msanii Batarokota alifanikiwa kuingia kwenye tuzo za
Kilimanjaro Tanzania Music Award 2014 (KTMA 2014) kama nominiss katika
kategori ya Wimbo bora wenye Vionjo vya Asili ya Kitanzania na wimbo wa
kisukuma uitwao `Kwejaga Nyangisha`
NYIMBO MPYA AKIWA NJE YA KUNDI
Batarokota kwa sasa ana nyimbo saba ambazo amesha kamilliza kwa
ajili ya maandalizi ya albamu yake mpya atakayo zindua hivi karibuni yenye nyimbo sita ambazo ziko tiyari ni
` hongera mama` na `amani` nyimbo
hizi zimerekodiwa Mwaka 2003 Januari katika studio Mushroom Studio
jijini Nairobi Kenya chini ya mtayarishaji Teddy Karanda Harrison na Dj
Zari.
Nyimbo vingine ni `Sukurubu` ambayo imerekodiwa Multimedia Studio
jijini Mwanza mtayarishaji Alon Mikomangwa wasanii
walioshiriki kwenye nyimbo hii ni Ceni na Castro kutoka DRC, Kongo na
nyimbo nyingineni `sauti ya haki` na `kwejaga Nyangisha` zimerekodiwa
Januari,2012 studio ya Sky Studio iliyopo Kihonda Morogoro watayarishaji
Orecy Owden na Julius Chares.
Nyimbo nyingine ni ya kisukuma ihitwayo
`irombo rise`iliyo rekodiwa 6/Decemba/2012 katika studio za Sunlight
Records Mazimbu road -Kihonda Morogoro mtayarishaji King Maroh.
KUINGIA KATIKA SIASA
18/08/2015 katika chama cha ATC-Wazalendo na kupata kadi namba 223643 alikabidhiwa kadi na Afisa wa Chama mkoani Morogoro Mjini-Tanzania