Miaka ya Mapema
1952
Rolihlahla Mandela, mwanawe chifu, alizaliwa katika kijiji
kimoja kiitwacho, Mvezo katika mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini
tarehe 18 Julai mwaka 1918. Alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake
kwenda shule. Mwalimu ambaye hata hangeweza kutaja jina lake vyema,
alizoea kumuita Nelson. Alitoroka mjini Johannesburg mwaka 1941 ili
kuepuka kulazimishwa kuoa mapema. Alikutana na Walter Sisulu
aliyemsaidia kupata kazi katika kampuni ya ya Witkin Sidelsky na
Eidelma. Pia alijiunga na chama cha (ANC)
Kesi ya Uhaini
1956
Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza
ya sheria inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa
ushirikiano na Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao
walikosa uwakilishi. Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi
wa rangi, ANC ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza
kuendesha harakati zake kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na
kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi
yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958,
Mandela alimuoa Winnie Madikizela.
Huru hatimaye
1990
Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya
ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa
mwaka 1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De
Klerk akakiondolea marufuku chama cha ANC. Tarehe 11 Februari, Mandela
aliachiliwa baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku
yeye pamoja na mkewe wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza
wa chama cha ANC mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa
chama .Mazungumzo yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika
weusi na wazungu.
Tuzo ya amani ya Nobel
1993
Mnamo mwaka 1993, Mandela na rais wa nchi hiyo wakati huo,
walituzwa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi za kuleta uthabiti Afrika
Kusini. Akikubali tuzo hiyo, Mandela alisema kuwa '' tutafanya kila
tuwezalo kuweza kuleta mageuzi duniani.''
Rais mpya
1994
Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika
Kusini, watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa
kidemokrasia. Mandela alichaguliwa. Akihutubia umma, katika sherehe ya
kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: "uhuru
utawale, Mungu aibariki Afrika!'' Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa
nyumba za kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea
kuongezeka.Thabo Mbeki alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza
sera za nchi hiyo kimataifa.
Akitoka Robbben
1995
Kuadhimisha miaka mitano baada ya kuachiliwa kwake, Nelson
Mandela alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa
kwa miaka 18. Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na
wafungwa wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu.
Mapafu ya Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi
katika machimbo ya mawe.
Usiniite''
2004
Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama
kiongozi wa chama tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka
1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji,
akiwa na miaka 80. Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo
kuanza matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa
anataka maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha
aliwaambia wandishi wa habari wasimpigie simu.
Sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake
2008
Wanamuziki, waigizaji na wanasiasa waliungana na Mandela
katika sherehe kubwa uwanja wa Hyde Park mjini London kusherehekea miaka
90 ya kuzaliwa kwake. Akiongea na wale waliofika, aliwaambia, ''ni
wakati kwa kizazi kipya kuchukua uongozi, kibarua kwenu sasa.''
Kuugua
2010
Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya
kustaafu. Ingawa alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la
kombe la dunia mwaka 2010 nchini humo. Januari mwaka 2011, alilazwa
hospitalini kwa ukaguzi maalum, huku serikali ikiwakumbusha watu kuwa
aliwahi kupata matatizo ya kupumua. Alipokea matibabu ya ugonjwa wa
mapafu mwaka 2012 na pia mwaka 2013 .