MAKAO Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani, yamekanusha vikali uvumi
ulioenea kwamba Baba Mtakatifu, Francis, yuko hatarini kwa kuwa kundi la
kimafia linamuwinda kumfanyia uhalifu kwa kile kilichoelezwa kuhusu
uamuzi wake wa kufanya mageuzi katika kanisa hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari wa Vatican, Frederico Kardinali
Lombard, alikiambia kituo cha habari cha ABC kwamba hakuna sababu za
wazi zinazoweza kuwafanya kuwa na wasiwasi.