Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Kim Poulsen, amesema timu yake mesto wa yosso na wazoefu, iko tayari kuikabili Zambia (Chipolopolo) katika mechi yake ya kwanza ya kuwania ubingwa wa mashindano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Nyayo jijini hapa.
Akizungumza jana, Poulsen alisema wachezaji wake wote wako tayari na wamejiandaa kufanya vizuri katika mechi hiyo ya kwanza ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele.
Poulsen alisema mechi dhidi ya Chipolopolo inatarajiwa kuwa ngumu kwa sababu wachezaji wengi wa Zambia ni wauzoefu tofauti na kikosi chake ambacho mwaka huu ni mseto kutokana na kujumuisha yosso wengi aliowaita kwa mara ya kwanza, lakini anaamini watafanya vizuri.
"Tuko tayari, tumejiandaa kwa mashindano na tunaamini tutaanza vyema mechi yetu," alisema Kocha huyo raia wa Denmark.
Aliongeza kuwa, katika kundi lao ambalo linajumuisha timu ya Somalia na Burundi, hakuna mechi nyepesi kwa sababu kila moja imekuja kushindana na si kushiriki.
Naye mshambuliaji mahiri wa timu hiyo, Mrisho Ngasa, aliliambia blogu hili kuwa wamekuja Nairobi kushindana na watajituma ili kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania Bara.
Ngassa alisema anajua Watanzania wamewatuma kuiwakilisha vyema na hicho ndicho wamepanga kukitekeleza.
"Tunajua jukumu letu na tunamuomba Mungu tufanye vizuri, tuombeeni ili tufanye kile ambacho kocha ametuelekeza," alisema Ngasa.
Kilimanjaro Stars iliyoko Kundi B, ilitua jijini hapa juzi usiku na itacheza mechi yake ya pili Desemba Mosi dhidi ya Somalia huku ikimaliza hatua ya makundi kwa kuivaa Burundi hapo Desemba 4, mwaka huu.
Uganda ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka kwa kushirikisha nchi wanachama wa Cecafa na timu alikwa.

Mashindano ya Cecafa Senior
Challange yanaanza kesho jumatano huku timu 12 zikishiriki
kwenye mashindano hayo yanayo husisha timu kutoka kanda ya za Afrika
Mashariki na Kati.
Makocha wa timu zote wamewaita kambini wachezaji
wao bora wakiwemo wale wanaocheza ugenini ili kuongeza nafasi zao za
kushinda kombe hilo.Mechi zitachezwa katika miji ya Nairobi, Kisumu, Nairobi na Machakos huku serikali za wilaya zikitoa udhamini na kushawishi kumbi ambapo mechi hiyo itaandaliwa- kwa kurejelea mashindano ya vilabu bingwa ya mwaka huu yalioandaliwa katika miji ya darfur na kusini mwa kordofan nchini sudan.
Mashindano ya cecafa yamesalia kuwa chanzo cha furaha katika soka haswa kwa mashabiki wa eneo la afrika magharibi na kati haswa ikizingatiwa kuwa timu kutoka eneo hili hazijapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa kutokana na viwango duni vya soka nchini.
Ukosefu wa wadhamini umesababisha kubadilishwa kwa jina la mashindano ya mechi za cecafa mara kwa mara kwa heshma za wadhamini.
Tanzania wamewaita washambulizi wa TP mazembe Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata ili kuonyesha uzito wa mashindano ya mwaka huu.
Mashindano ya klabu bingwa yameitwa baada ya rais wa Rwanda Paul Kagame huku Senior Challenge yakipewa jina la bwenyenye wa Ethiopia Sheikh Mohammed al Amoud kati ya 2005 na 2006.
Mashindano ya mwaka huu yatakayoisha tarehe 5 Disemba yanajumuisha timu 11 za kanda na Zambia ambao ni wageni.
Kundi A ni Kenya, Ethiopia, Sudan kusini na Zanzibar,
kundi B ni Tanzania, Zambia, Burundi na Somalia,
kundi C linahusisha mabingwa watetezi Uganda, Rwanda, Sudan na Eritrea.
Ni timu 4 pekee zimeweza kufuzu kwa kombe la Afrika katika mda wa miaka 10 huku 1 pekee ikishiriki hatua ya makundi.
Rwanda na Kenya zilifika Tunisia 2004, Sudan ilishiriki fainali Ghana 2008 na 2012 huko Equitorial Guinea huku Ethiopia ikishiriki Afrika Kusini 2013.
Cecafa ilianzishwa mwaka 1926 wakati huo ikijulikana kama Kombe la Gossage wa utawala wa ukoloni Kenya, Uganda,Tanganyika na Zanzibar, lakini mwaka wa 1967 ilibadilishwa jina na kuwa senior challenge cup na imekua ikiandaliwa mara kwa mara lakini imeshindwa kuhamasisha ushindani jambo ambalo limechochea mjadala kulifanya shindano hili kuwa la kuendeleza timu za vijana.