Week Hot newz

South America delivers again


South America delivers again


Regarded by some of its participants as the toughest and most evenly matched of all the qualifying competitions, the South American Zone lived up to all expectations as five contenders battled their way through to the 2014 FIFA World Cup Brazil™.
Their journey to Brazil was lit up by some stellar individual performances and memorable matches, though the tournament will also remain in the memory for other reasons.

Bikira Maria ni Mama wa Matumaini!

Shamrashamra za kufunga Mwaka wa Imani sanjari na Sherehe za Kristo Mfalme zimeanza kutimua vumbi mjini Vatican baada ya Baba Mtakatifu Francisko. Alhamisi tarehe 21 Novemba 2013 kuwatembelea na kusali pamoja na Wamonaki wa Shirika la Wakamadoli mjini Roma. Baba Mtakatifu aliongoza Ibada ya Masifu ya Jioni na baadaye Askofu mkuu Rino Fisichella aliongoza Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu, kama changamoto kwa waamini kumkaribisha Kristo katika hija ya maisha yao ya ndani.

Mihadarati;Wema kunyongwa China,

Akiandika katika ukurasa wake wa Histogram, Wema alisema anachukizwa sana na kitendo hicho, kwani kinamfanya asikae kwa amani na watu walio karibu yake, na wengine wanamtenga kupitia vichwa vya habari tofauti vya magazeti, ambavyo kwa asilimia kubwa anasema vinatumika kuuzia magazeti hayo.
“Hivi karibuni kuna gazeti moja limeandika, ‘Ishu ya dawa za kulevya – Wema kunyongwa China,

Poulsen:Silaha za Chalenji hizi hapa



Kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen ametaja kikosi chake cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27, mwaka huu

Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho 2010 chini ya Kocha Mdenmark, Jan Poulsen, na ambayo imepangwa Kundi B katika michuano ya mwaka huu, itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28, mwaka huu dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos nje kidogo ya Jiji la Nairobi.

Sinema ya msimbazi:Rage kutua Dar kwa Mbwembwe

Wakati  Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage akitarajiwa kutua nchini tarehe 22/11/2013 jioni, bodi ya wadhamini ya klabu hiyo imetangaza kusitisha maamuzi ya kamati yao ya utendaji ya kumwengua katika nafasi uenyekiti.

Jumanne Kamati ya Utendaji ya Simba iliyokutana Jumatatu bila uwapo kwa mwenyekiti (Rage) aliyekuwa Marekani, ilitangaza kumsimamisha Rage na makocha wa timu yao, Abdallah 'King' Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelu 'Julio'.

Kamati hiyo iliamua timu kwa sasa iwe chini ya kocha wa timu ya vijana, Simba B, Seleman Matola  ambaye atakuwa pia Msaidizi wa Kocha Mkuu mpya wa kigeni, Zdravok Logarusic, raia wa Croatia atakayetambulishwa Desemba Mosi, mwaka huu.

DONDOO ZA MAPINDUZI NDANI YA SIMBA

Mapinduzi tata Simba

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibaden �King� na msaidizi wake Jamhuri Kihwelu �Julio�
Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba imefanya mapinduzi yenye utata baada jana kutangaza kumsimamisha kwa muda usiojulikana Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage, lakini uamuzi huo ukionekana kwenda kinyume na Kununi za Shirikisho la Soka nchini, TFF.

Kamati hiyo pia imeamua kuwatimua Kocha Mkuu, Abdallah Kibaden “King” na msaidizi wake Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ na kumtangaza Kocha mpya kwamba atakuwa ni raia wa Croatia, Zdravok Logarusic ambaye atasaidiwa na nahodha wa zamani wa timu hiyo ambaye kwa sasa anainoa Simba B, Selemani Matola.

Katiba ya TFF
Hata hivyo, Katiba ya TFF ambayo ndiyo Katiba mama inayopaswa kufuatwa na vyama vya soka na klabu zote zilizo chini ya shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka nchini, hairuhusu mapinduzi na wajumbe wote wa kamati za utendaji wa kuchaguliwa wanatakiwa wakae madarakani kwa muda wa miaka minne.

Ibara ya 31 (6) cha Katiba hiyo kinaeleza kwa tafsiri isiyo rasmi; “Mjumbe wa kamati ya utendaji anaweza kuondolewa baada ya yeye mwenyewe kuandika barua ya kujiondoa, kutohudhuria vikao vinne mfululizo vya kamati ya utendaji, kushindwa kufanya kazi za kamati ya utendaji kutokana na kuugua hadi kufikia hatua ya mgonjwa mahututi ndani ya kipindi cha miezi 12 na kupatikana na hatia ya kutenda kosa la jinai au kufungwa pasi na dhamana.”

Babu Seya sasa kufia jela


Nguza Viking na mtoto wake Papii wakitoka mahakamani
Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania imetupilia mbali ombi la warufani wawili Nguza Viking na mwanaye, ambao waliomba mahakama hiyo kufanya marejeo ya uamuzi wake wa awali wa kuwapata na hatia kama ambavyo hukumu dhidi yao ilivyotolewa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004.
Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto.

Askofu: Mtandao umemuua Mvungi

Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Marehemu Dk. Sengondo Mvungi
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi, alizikwa jana katika Kijiji cha Chanjale Juu, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro huku Askofu Rogath Kimario wa Kanisa Katoliki Jimbo la Same, akiwaeleza waombolezaji kwamba marehemu amekufa kwa kifo cha fedheha kilichotokana na kile alichokiita mauaji ya kimtandao.

20 wauawa kwa shambulio

Moja ya mashambulio nchini Somalia
Karibu watu ishirini wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga kwenye kituo cha polisi nchini Somalia.
Shambulio hilo limetokea katika mji wa Beledweyne karibu na mpaka na Ethiopia. Mashuhuda wameiambia BBC kuwa gari lilipiga lango kuu la kuingia kwenye jengo la polisi na kulipuka kabla ya watu wenye silaha kushuka na kushambulia jengo hilo kwa risasi. Taarifa zinasema wengi waliofariki katika shambulio hilo ni maafisa wa polisi.

Cameroon yazifuata Nigeria, Ivory Coast


Cameroon imekuwa nchi ya tatu kutoka barani Afrika kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Brazil mwaka kesho 2014 baada ya kuifunga Tunisia siku ya jumapili kwa magoli 4 - 1 katika mechi iliyopigwa mjini Younde Cameroon.
Cameroon itashiriki fainali hizo za Kombe la Dunia kwa mara ya sita tangu mashindano hayo yalipoanza ambapo sasa itaungana na Nigeria na Ivory Coast ambazo nazo zimefuzu kushiriki mashindano hayo

Tarehe 24 Novemba 2013 Papa kukabidhi Waraka wa "Furaha ya Injili"

Baba Mtakatifu Francisko katika kilele cha Maadhimisho ya Mwaka wa Imani sanjari na Siku kuu ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu anatarajiwa kuwakabidhi waamini Waraka Mpya wa Kichungaji, "Evangelii Gaudium" Yaani "Furaha ya Injili" kama alama ya kudumu ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani. Ibada ya Misa inatarajiwa kuanza saa 4:30 kwa saa za Ulaya.

Hayo yamesemwa na Askofu mkuu Rino Fisichella, Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji mpya alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari mjini Vatican siku ya Jumatatu, tarehe 18 Novemba 2013. Mkutano huu umehudhuriwa pia na viongozi waandamizi kutoka Baraza hili.

Ufoo Saro: Niliokoka kufa kutokana na miujiza ya Mungu

Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro akisoma somo kwenye biblia wakati wa ibada maalumu ya shukrani kwenye Kanisa la (KKKT ) Usharika wa Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dare Salaam jana. Picha na Sanjito Msafiri.


Baba Mtakatifu atoa dawa ya maisha ya kiroho



Jumapili iliyopita tarehe 17 Novemba 2013 wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, waamini na mahujaji waliokusanyika ili kuungana na Baba Mtakatifu Francisko kwa Tafakari na Sala ya Mchana, walipewa tiba ya maisha ya kiroho, itakayowasaidia katika kumwilisha mafanikio ya Mwaka wa Imani.

Yatakayojiri wakati wa kufunga Mwaka wa Imani:

Mama Kanisa anajiandaa kufunga rasmi Mwaka wa Imani, uliotangazwa na kuzinduliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita na kuendelezwa kwa ari na moyo mkuu na Papa Francisko hapo tarehe 24 Novemba 2013, wakati wa Sherehe ya Kristo Mfalme. Ibada hii inatarajiwa kuongozwa na Baba Mtakatifu Francisko, kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya. Maadhimisho ya kufunga Mwaka wa Imani yataanza rasmi kwa

Blessing of a New House


Translated by Most Reverend J. H. Schlarman Bishop of Peoria

Mandela hoi awezi kuongea!

Picha ya kale ya Nelson Mandela na Winnie kabla ya kuachana
Mke wa zamani wa Nelson Mandela, amesema rais huyo wa zamani awezi kuzungumza, lakini anatumia uso kuwasiliana na watu.
Winnie Madikizela-Mandela alieleza kuwa Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 95, ni mgonjwa kweli kweli ,lakini alikanusha tetesi kuwa mashini ndio inamsaidia kupumua.
Mwezi wa Septemba Bwana Mandela alirudi nyumbani baada ya kulazwa hospitali mjini Pretoria kwa karibu miezi mitatu akitibiwa ugonjwa wa mapafu.
Serikali ya Afrika Kusini imesema hali yake bado ni ya kutia wasi-wasi na wakati mwengine hubadilika.

Samatta wawania tuzo Mchezaji bora wa Afrika

Mbwana Samatta  na Victor Wanyama (kulia) 
Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limetangaza majina ya wachezaji wa kiafrika watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2013 na Mchezaji bora wa Afrika anayechezea vilabu vya ndani ya Afrika mwaka 2013.
Katika majina hayo yapo majina mawili ya wachezaji wanaotoka Afrika Mashariki ambao ni Victor Wanyama raia wa Kenya anachezea

GARAMA ZA MATIBABU KUWA JUU: Bacteria sugu ni tishio kubwa


Dawa za antibiotics zinazouzwa Afghanistan
Tume ya wataalamu wa afya imeonya kuwa aina sugu ya vidudu vya bacteria ni moja kati ya tishio kubwa kabisa katika matibabu.
Katika taarifa iliyoandikwa kwenye jarida la kisayansi, The Lancet, wataalamu wanatoa wito mataifa yashirikiane ili kupambana na tishio hilo.

Taasisi ya Kiislamu yachangia damu salama

TAASISI ya Bilal Muslim Mission of Tanzania imewashauri Watanzania kujitolea damu salama ili kuokoa maisha ya wengi wanaohitaji damu hospitalini.
Ombi hilo limetolewa juzi na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sibtain Meghji, alipozungumza wakati wa utoaji damu salama, tukio lililofadhiliwa na taasisi hiyo jijini Mwanza.

NDOA: habithi katika Uislamu

Mzee wa miaka 80 alirudi nyumbani kutoka msikitini, akabisha mlango wa nyumba yake lakini hakufunguliwa, akasimama kwa mda mpaka akazirai na kuanguka chini, Mke wake akaona mume wake amechelewa, akafunguwa mlango kwenda kumtafuta, akampata amezirai mbele ya mlango, akamwagia maji mpaka akapata fahamu, mke akamuomba msamaha mume wake kwa kuchelewa kumfungulia mlango kwa kuwa hakusikia mlango ukibishwa na akaona yeye ndie sababu ya mumewe kuzirai..
Mume akamwambia mke wake sikuzirai kwa sababu hiyo bali niliposimama mbele ya mlango wangu na nikaona umefungwa, nikawa nafikiria jee kama ningekuwa nimesimama mbele ya Mlango wa Allah subhanahu wata'ala na Allah subhanahu wata'ala hakunifungulia ningekuwaje?
Katika ile hali ya kufikiria hivyo nikajipata sina fahamu;);););)