Week Hot newz

FIFA World Cup History

South Africa 2010
Winner: Spain
Runners-Up: Netherlands
Third: Germany
Fourth: Uruguay
adidas Golden Ball: Diego FORLAN (URU)
adidas Golden Boot: Thomas MUELLER (GER)
Best Young Player Award: Thomas MUELLER (GER)
adidas Golden Glove: Iker CASILLAS (ESP)
FIFA Fair Play award: Spain

Mwandishi wa BBC amkumbuka Mandela


Mandela aliwagusa watu wengi duniani
Nelson Mandela alijiondoa kutoka maisha ya umma mwaka 2004. Mwandishi wa BBC Richard Hamilton alikuwa mwandishi wa BBC mjini Cape Town wakati huo na anatuletea kumbukumbu zake kuhusu rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini:
"Bwana Mandela, unawezaje kuwa katika hali hii nzuri ya mwili? Aliuliza ripota msichana wa tv, ambaye aligongana jicho na Bwana Mandela.
Tulikuwa katika eneo la gereza la Kisiwa cha Robben ambako Nelson Mandela alitumikia miaka kumi na nane kati ya ishirini na saba aliyofungwa jela.

Struggle giants die within 10 years of each other


In the 1940s Tambo, Sisulu, Mandela and other young intellectuals of the time regularly visited the house of then ANC president Dr AB Xuma. It was there that they came up with a plan to revive the ANC and make it more accessible to ordinary people. In 1944 the three men helped form the ANC Youth League.


Three giants of the struggle -- Oliver Tambo, Walter Sisulu, and former president Nelson Mandela -- died within 10 years of each other.
The first to die was former African National Congress president Oliver Tambo in 1993.
Tambo and Mandela met when they were studying at the University of Fort Hare in the Eastern Cape.
In the 1940s Tambo, Sisulu, Mandela and other young intellectuals of the time regularly visited the house of then ANC president Dr AB Xuma. It was there that they came up with a plan to revive the ANC and make it more accessible to ordinary people. In 1944 the three men helped form the ANC Youth League.
Tambo spent over 30 years in exile. He become acting ANC president in 1967 following the death of Chief Albert Luthuli and in 1985 he was re-elected president of the party.
The same year Tambo returned from exile he was elected ANC chairman. He died on April 24, 1993 at the age of 75 due to complications after a stroke.
During his speech at Tambo's funeral Mandela said: "Here lies before you the body of a man who is tied to me by an umbilical cord which cannot be broken."
In 2003 former ANC secretary general and deputy president of the ANC Walter Sisulu died.
Sisulu, who was born in 1912, the year the ANC was founded, died at his Johannesburg home in the arms of his wife Albertina, herself a legend in her own lifetime.
In a tribute to Sisulu Mandela said: "Xhamela is no more. May he live forever! His absence has carved a void. A part of me is gone."
Mandela's impassioned statement at the time spoke of a 62-year-old friendship.
"Our paths first intersected in 1941. During the past 62 years our lives have been intertwined. We shared the joy of living, and the pain," he said.
"In a sense I feel cheated by Walter. If there be another life beyond this physical world I would have loved to be there first so that I could welcome him. Life has determined otherwise."
On Thursday, 10 years after his old friend's death, Mandela died at the age of 95. He will be buried in his hometown of Qunu in the Eastern Cape next Sunday.

Msiba wa Mandela kuwabeba Tanzanite leo?


the TanzaniteMKUU wa msafara wa timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini chini ya miaka 20, Peter Manchonyane, ameelezea wasiwasi wa kikosi chake kuathiriwa na msiba wa Rais wa zamani wa nchi yake, Nelson Mandela, katika mechi ya leo dhidi ya Tanzania ‘Tanzanite’.
Bara la Afrika na dunia kwa jumla, inaomboleza msiba wa Mandela, aliyefariki juzi usiku, saa chache baada ya kikosi cha vijana cha nchi hiyo kutua nchini kwa mechi ya mchujo kuwania kufuzu fainali za dunia kwa wanawake chini ya umri huo, zitakazochezwa nchini Canada mwakani.
Manchonyane alisema kuwa kikosi chake kinachojulikana kwa jina la ‘Basetsana’, kimekumbwa na simanzi miongoni mwa wachezaji na viongozi, baada ya kifo cha Mandela na kwamba anahisi kitaathiri harakati zao leo.
Pamoja na hofu hiyo, kiongozi huyo alisisitiza kuwa lengo lililowaleta ni kupigana kusaka ushindi, ili kujiwekea mazingira mazuri kuelekea mechi ijayo kuwania tiketi ya kufuzu raundi ya tatu na ya mwisho ya mchujo huo wa fainali za mwakani huko Canada.
“Tumeshtushwa na kifo cha Mzee Mandela, kambi imejaa simanzi. Licha ya kutarajia ugumu kucheza tukiwa katika hali hiyo, lakini tunaamini tutashinda changamoto hiyo na kuibuka na ushindi ili kuondoa presha katika mechi ya marudiano nyumbani,” alisema Manchonyane.
Kwa upande wake kocha wa Tanzanite, Rogasian Kaijage, alisema, kauli ya kiongozi huyo ni ‘danganya toto’ iliyobeba mantiki ya kuwahadaa na kuvimbisha kichwa na kwamba ameligundua hilo na kikosi chake kitacheza kwa tahadhari dhidi ya Basetsana.
Alisema, anakitambua kikosi cha Basetsana ni kizuri, imara na bora, hivyo kazi ya nyota wake itakuwa kupigania matokeo mazuri nyumbani kama ilivyokuwa dhidi ya Msumbiji na wala hawatobweteka kwa alichokiongea kiongozi huyo.

“Basetsana kama jina lao lilivyo ni wasichana wadogo, ambao ni vigumu kushikwa na simanzi kubwa juu ya msiba wa kiongozi ambaye wakati anatawala wengine walikuwa wadogo, wengine hawajazaliwa. Watoto mara nyingi hawaguswi sana na vifo,” alifafanua Kaijage.
Aliongeza kuwa, nia yao kama timu ni kupigania matokeo mazuri na kuwataka Watanzania kumiminika kwa wingi kuwasapoti mabinti hao, ili kuwapa nguvu ya kushinda na kujiweka pazuri kuelekea raundi ya tatu ya michuano hiyo.
Kwa upande wake nahodha wa Tanzanite, Fatuma Issa, alisema, morali katika kikosi chake iko juu na kwamba, Watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa ili kuwashangilia kuwaongezea nguvu na Mungu akipenda wataibuka na ushindi.
Viingilio katika mechi ya leo itakayopigwa kuanzia saa 10:00 alasiri, vitakuwa ni sh 1,000, sh 2000, sh 5,000 na sh 10,000, ambako tiketi zitauzwa uwanjani hapo leo.

Papa Francisko aomboleza kifo cha Mzee Madiba!



Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambirambi kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini na wananchi wa Afrika ya Kusini kwa ujumla wao kutokana na kifo cha Mzee Nelson Mandela. Anaiombea roho ya Mzee Mandela iweze kupata huruma ya Mungu pamoja na kuendelea kuwaimarisha wote walioguswa na msiba huu mzito!

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Mzee Nelson Mandela alisimama kidete kulinda na kutetea utu na heshima ya raia wake; akajenga na kuimarisha umoja wa wananchi wa Afrika ya Kusini pasi na vita, wakitembea katika njia ya upatanisho na ukweli. 



Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, mchango wa Mzee Mandela utakuwa ni changamoto kwa wananchi wa Afrika ya Kusini kusimama kidete kulinda haki na mafao ya wengi; wanasiasa wakiwa mstari wa mbele. Baba Mtakatifu anawapatia wananchi wote wa Afrika ya Kusini baraka zake za kitume, wakati huu wa maombolezo ya kitaifa!

Ni kisasi leo Kili Stars vs Cranes


Kili na CranesKIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’, kinatarajiwa kushuka dimbani leo kuwakabili Uganda ‘The Cranes’ katika mechi ngumu ya robo fainali ya michuano ya Chalenji iliyoanza kutimua vumbi Novemba 27.
Mechi kati ya Stars na Cranes ambao ndio mabingwa watetezi, inafananishwa na fainali kutokana na upinzani wa timu hizo. Itachezwa saa 8:00 mchana kisha kufuatiwa na mchezo mwingine wa hatua hiyo saa 10:00 jioni kati ya wenyeji Kenya ‘Harambee Stars’ na Rwanda.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen, alisema ana imani ya kufanya vema kutokana na ubora wa kikosi chake, hasa baada ya kuwasili kwa nyota wa kimataifa, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Poulsen alisema siku mbili tangu walipotoka kucheza na Burundi, amehakikisha anarekebisha matatizo aliyoyaona katika mchezo huo, hasa safu ya ulinzi ambayo ilionekana kulegalega.
Naye kipa wa Stars, Ivo Mapunda, alisema hakuna timu ambayo wanaihofia katika michuano hiyo, bali cha muhimu ni dakika 90 za uwanjani ndizo zitaamua nani anasonga mbele na nani anafungasha virago.
Alisema ana imani kubwa ya kufanya vema katika mchezo wa leo, huku akiwataka wachezaji wenzake kutulia na kucheza mpira, kwani kuwafunga Uganda kuko pale pale ila cha muhimu Watanzania ni dua zao.
“Unajua hakuna mtu aliyetegemea kama tutafika hapa tulipo sasa, hivyo basi kwanini mbele tushindwe? Uganda ni timu ya kawaida tu kama timu nyingine, nina imani tutashinda,” alisema Mapunda.
Naye Kocha wa Uganda, Milutin Micho aliyewahi kuifundisha Yanga, alisema anauhofia mchezo wa leo, baada ya kuwaona Samatta na Ulimwengu wakiwemo katika kikosi cha Kili Stars.
Micho alisema lolote linaweza kutokea katika mchezo huo, cha muhimu ni kusubiri dakika 90 za mwamuzi uwanjani ila Tanzania ni timu nzuri.
“Mechi hiyo itakuwa ngumu, kwa kuwa nimefuatilia mechi za Tanzania, ni wazuri, lakini vijana wangu pia watapambana ili kuhakikisha wanashinda,” alisema Micho.

Nelson Mandela kuzikwa Desemba 15 siku ya Jumapili


Nelson Rolihlahla MandelaSIKU moja baada ya kifo cha  Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela (95), mazishi yake yanatarajiwa kufanyika wiki moja kuanzia sasa, Desemba 15, siku ya Jumapili.
Mazishi hayo ya kihistoria na ya aina yake, yatafanyika katika kijiji chake cha Qunu, mahala alipopachagua mwenyewe kabla ya kifo chake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Mzee Madiba atazikwa katika eneo hilo la Mashariki ya Cape kwa heshima zote.
Zuma alisema mazishi ya kitaifa, ikiwamo utoaji wa heshima za mwisho, yatafanyika jijini Pretoria ambapo baadaye mwili wake utasafirishwa kwenda Mkoa wa Cape Mashariki hadi katika Kijiji cha Qunu ambako ndiko  Mzee Madiba alipozaliwa na kukulia.
Aidha, taarifa hiyo ilieleza kuwa  Mzee Madiba  atazikwa kwa sherehe maalumu za kimila karibu na makaburi ya watoto wake watatu.
Kutokana na msiba huo ulioikumba dunia, wakuu wa nchi mbalimbali duniani, akiwemo Rais wa Marekani, Barack Obama, Oprah Winfrey na Hillary Clinton wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo mbali ya viongozi wengine kutuma salamu za rambirambi kwa Rais Zuma na kwa familia ya Mzee Madiba.
Viongozi duniani wanena
Miongoni mwa marais waliotuma salamu za rambirambi kwa Rais Zuma na kwa mjane  wa Mzee Madiba, Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika Kusini ni pamoja na Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye pia ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia jana hadi Desemba 8  na kuagiza bendera kupepea nusu mlingoti kwa siku hizo.
Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa,  Ban Kin Moon alisema Mandela alikuwa kielelezo cha  Umoja wa Mataifa  kwani alikuwa mtu wa heshima na mtetezi wa haki za binadamu,  aliyepinga ubaguzi wa rangi na mpigania usawa.
“Kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, natoa rambirambi zangu kwa watu wa Afrika Kusini na hasa kwa familia ya Nelson Mandela na wapendwa,” alisema.
Aidha, Moon alieleza kuwa inashangaza, kuona Mandela alitoka kizuizini bila uadui baada ya kifungo cha miaka 27, ambapo nia yake ilikuwa kujenga nchi yake katika misingi bora kwa kutumia akili.
Salamu za Rais Kikwete kwa Zuma
Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Zuma, wanafamilia na wananchi wote wa Afrika Kusini kutokana na kifo cha Mzee Mandela.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwandishi wa habari wa rais msaidizi, Ikulu Premi Kibanga, Rais Kikwete ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia jana Desemba 6 hadi 8 mwaka huu.
Aidha, Rais Kikwete alisema kuwa katika siku hizo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Rais Kikwete alisema kuwa msiba huo ni wa bara zima la Afrika na dunia.
“Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa karne ya 20 na 21. Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwanamapinduzi na mstahamilivu,” alisema.
Rais Kikwete alimuelezea Mzee Mandela kuwa ni  kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha  kuwaunganisha wananchi wa Afrika Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
“Mandela ni mfano bora kwa wanadamu, wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa. Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake, hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake.”
Alisema ni muhimu kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake  mahali pema peponi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idhaa za Kiafrika katika DW, Claus Stäcker alisema kuwa vyombo vya habari na wanasiasa duniani kote wanaendelea kushindana katika kuonyesha heshima zao kwa Mandela, ambaye yeye mwenyewe hakupenda kuchukuliwa kama Mungu.
Stäcker alisema Mandela hakuwa mtakatifu, hata ingawa hivyo ndivyo vyombo vya habari vinavyomwelezea. Kila kichwa cha habari kinamfanya aonekane kama mtu aliyefanya maajabu na hasa kuonekana kama kuiabudu sanamu.
“Mandela mwenyewe hakupenda kuabudiwa. Alikuwa akikubali tu shingo upande barabara, shule na taasisi kuitwa jina lake, kuruhusu sanamu za shaba na majumba ya makumbusho ya Mandela kujengwa, mtindo ambao bila shaka utaendelea kukua,” alibainisha  Stäcker.
Jijini Dar es Salaam, vilio, simanzi na majonzi  vilitawala katika Ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo nchini baada ya raia wa mataifa mbalimbali wakiwemo Waafrika Kusini wanaoishi nchini, kufika kwa ajili ya kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Mandela.
Raia hao ambao wengi ni wa kigeni walifika katika ubalozi huo kuanzia majira ya saa moja asubuhi, huku wakibeba mashada ya maua na kuyaweka katika picha kubwa ya Mandela iliyowekwa mbele ya ofisi za kuingilia za ubalozi huo.
Raia wa Canada anayeishi hapa nchini aliyejitambulisha kwa jina moja la Jeff, alisema ameguswa na kifo hicho kutokana na Mzee Mandela kuwa mfano bora kwa jamii hasa katika harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi.
“Nimeamua kuambatana na familia yangu kuja kutoa pole kwa kifo hicho kimetugusa sana kwani tumekuwa tukimuangalia Mandela kama mfano wa kuigwa kwa dunia nzima,” alisema.
Akizungumzia kifo hicho, Balozi wa Afrika Kusini nchini, Thanduyise Henry Chiliza alisema ni huzuni kubwa na majuto kuwajulisha kuwa rais wa zamani na nembo ya kitaifa, Nelson Rolihlahla Mandela, amefariki dunia juzi Desemba 5, mwaka huu, majira ya saa 2:50 usiku akiwa na umri wa miaka 95.
“Ingawa sisi tulijua kwamba siku hii itakuja, lakini hakuna kitu kinachoweza kupunguza hisia zetu na hasara kubwa tuliyopata na ya kudumu kwa kumpoteza kiongozi huyo,” alisema.
Alisema kutokana na msiba huo bendera ya taifa hilo itapepea nusu mlingoti hadi mazishi ya Mzee Mandela yatakapofanyika.
“Kitabu cha maombolezo kimefunguliwa katika ubalozi wetu plot 1338/9, barabara ya Mwaya, Masaki, Dar es Salaam kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi saa 3:30 hadi saa 9:30 na Ijumaa saa 3:30 hadi saa 6:30 mchana kasoro siku za sikukuu,” alisema.
Chiliza alisema Serikali ya Afrika Kusini inaendelea na mipango ya mazishi na Waafrika Kusini kila pembe ya dunia watajulishwa suala hilo.
Maisha ya Mandela
Mandela alikuwa mtu aliyezaliwa kuwa kiongozi.
Kama rafiki yake waliyefungwa naye pamoja, Ahmed Kathrada, alivyosema hivi karibuni, Mandela alizaliwa katika familia ya kifalme na ilikuwa kawaida kwake kuwa alizaliwa kuwa kiongozi.
Mandela alijibeba vyema sana alipokuwa kiongozi wa chama cha ANC na kwamba hakuna hata nusu ya imani yake iliwahi kumuondoka miaka yote 27 aliyokuwa gerezani.
Ingawa Mandela alijitaja mwenyewe kuwa kama sehemu tu ya uongozi wa ANC, hapakuwa na shaka kuwa alikuwa kiongozi mkuu wa chama hicho kwa kizazi chake wakati huo nchini Afrika Kusini.
Kwa dunia nzima Mandela alikuwa ishara ya mambo mengi, sio kiongozi tu, lakini mfano wa viongozi ambao dunia inastahili kuwa nao enzi hizo.
Wengi wanamfahamu Mandela kwa kuwa na moyo mwepesi wa kusamehe na wengi wanamkumbuka hivyo kwani baadhi walimshangaa sana miaka ya tisini, aliposema kuwa hana chuki na mtu na kuwa amewasamehe waliomtendea ubaya na hata kumfunga.
Alizaliwa mwaka 1918, katika Rolihlahla Dalibhunga, na kulelewa katika Kijiji cha Mvezo Mashariki mwa Mkoa wa Cape.
Alikuwa na ndugu zake 13 katika familia iliyokuwa na uhusiano wa karibu na familia ya kifalme ya Thembu.
Mandela alienziwa na wengi kwa sababu ya vita aliyopigana dhidi ya utawala wa wazungu.
Baba yake alifariki Mandela akiwa na miaka tisa. Alimtaja baba yake kama mtu mkali mwenye kutaka watu kufuata maadili mema.
Lakini alimsifu sana baba yake kwa kumsisitizia kuwa na maadili mema kwani yeye ndiye alimfanya kuwa mtu mwema maishani.
Ilikua muhimu kwake kupata elimu. Na hivyo akasomea katika shule ya kimethodisti na kisha mwaka 1939 akaenda katika Chuo Kikuu cha Fort Hare.
MAISHA YAKE KWA UFUPI
1943: Alijiunga na chama cha ANC.
1956: Alifunguliwa kesi ya uhaini, lakini baada ya miaka minne ikatupiliwa mbali.
1962: Alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la uchochezi na kufungwa jela miaka mitano.
1964: Alishitakiwa kwa kosa la kuhujumu serikali na kufungwa maisha jela.
1990: Aliachiliwa kutoka gerezani.
1993: Alishinda tuzo ya Amani ya Nobel.
1994: Alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini.
1999: Aling’atuka madarakani.
2001: Aligundulika kuwa na saratani ya tezi kibofu.
2004: Alistaafu.
2005: Alitangaza kuwa mwanawe alifariki kwa maradhi ya ukimwi.

Kifo cha Mandela:Dunia waomboleza


Nelson Mandela kuzikwa tarehe 15 Desemba
Raia wa Afrika Kusini wako kwenye maombolezo kwa siku ya pili hii leo wakiwa kwenye mkesha kwa usiku nzima kwa ajili ya kuomboleza mpendwa wao Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela, aliyeaga dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Watu wamekuwa wakikumbuka mema yake , wakicheza na kuimba Mbele ya makazi yake ya zamani mjini Soweto.
Katika mkutano na Waandishi wa habari , Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliainisha matukio ya juma zima kwa ajili ya maombolezo ambapo ametangaza kuwa siku ya jumapili siku maalum ya maombi na ibada maalum.
Siku ya Jumanne, itakuwa ni siku ya shughuli maalum za maombolezo ya kitaifa ambapo shughuli hizo zitafanyika katika uwanja wenye uwezo wa kukusanya watu 95,000 ulio nje kidogo ya mji wa Johannesburg.
Raia wa Afrika kusini wakiwa kwenye maombolezo
Mwili wa Mandela utalala Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria kuanzia siku ya jumatano mpaka siku ya ijumaa.
Mazishi ya Mandela yatafayika jumapili ijayo tarehe 15 kijijini kwake alikokulia,Qunu.
Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 kabla ya kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.
Serikali yake iliondoa utawala wa kibaguzi wa watu weupe ambao ulikuwa na sera za kuwagawa watu wenye asili ya weupe na weusi.
Raia wa Afrika Kusini nchi nzima wamekuwa wakisali, wakiimba nyimbo za kupinga ubaguzi wa rangi na kuwasha mishumaa, wakikumbuka maisha ya Kiongozi wao na namna alivyo wavuta kwa mtindo wa maisha yake.

Kesho ni Basetsana na Tanzanite

  1. Kila mmoja wetu anafahamu kwamba Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Rolihlahla Mandela
    amefariki dunia jana December 6, 2013. Rais JM Kikwete pia akatangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo Dec 6 mpaka Dec 8 na bendera ya Tanzania itapepea nusu mlingoti siku zote hizo.
    Lakini kesho jumamosi Dec 7, 2013 ile timu yetu ya Wadada iliyowabugiza Msumbiji bao KUMI BILA uwanja wa Taifa inatakiwa kucheza na wadada wenzao wa Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 katika Uwanja wa Taifa.

KOMBE LA DUNIA || BRAZIL 2014 MAKUNDI KAMILI.



Makundi yamejulikana , na pia imejulikana nani atamenyana na nani.
Hapana shaka wapenzi wa soka barani Afrika pamoja na kuomboleza kifo cha Nelson Mandela wamekuwa wanafuatilia Droo ya kombe la dunia kufahamu nani wapinzani wa timu tano zinazowakilisha bara hilo.
Cameroon wamejikuta katika kundi gumu la A pamoja na wenyeji Brazil, Mexico na Croatia.
Mabingwa watetezi Uhispania watakuwa katika kundi B pamoja na Netherlands waliokutana nayo fainali kombe lililopita, na timu zingine ni Chile na Australia.
Dua ya Ivory Coast ya kuepuka kundi gumu sana wakati huu inaonekana imesikika, wako katika kundi C pamoja na Colomboa, Japan na Ugiriki.England watakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi D ambapo wapinzani wao ni Italia, Uruguay na Costa Rica.
Kwenye kundi E Ufaransa inacheka usiku huu kwani imepangwa pamoja na Uswizi, Ecuador na Honduras.Mabingwa wa Afrika Nigeria wako katika kundi F pamoja na Argentina Iran na Bosnia Harcegovinia, ambayo inashiriki kombe la dunia mara ya kwanza.
Ghana ndiyo inayoonekana kuwa matatizoni miongoni mwa timu za Afrika. Wamejikuta katika kundi G ambapo watapamaba na na Ujerumani, Marekani na Ureno.Timu ya tano ya Afrika Algeria itakuwa kwenye kundi H na wapinzani hapo ni Ubelgji, Korea Kusini na Urusi.



WORLD CUP Afrika Kusini mafanikio ya Mandela


Wanamichezo pia wamemkumbuka Mandela
Wanamichezo mashuhuri, duniani wametoa rambi rambi zao kwa hayati Nelson Mandela, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Mohamedi Ali
alisema: "Maisha ya Mandela yalikuwa na maana kubwa kwa dunia nzima , kwake mwenyewe, kwa taifa lake na dunia nzima.
Alitufanya sisi kugundua kua ni muhimu kumjali mwenzake na kuwa sisi ni ndugu licha ya rangi zetu.''
Mwanasoka mashuhuri Bofya Pele naye amesema "Mandela alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa sana maishani mwake. Ni shujaa wangu.’’
Mwanamasumbwi Bofya Ali aliongeza kusema kua, atamkumbuka Mandela sana kwa kuwa mtu mwenye roho safi na alichukizwa sana na mambo ya ubaguzi wa rangi pamoja chuki na uhasama.
Aliwatia moyo wengine kufikia mambo waliyoyaona kama yasiyowezekana.''
"Bofya Ali amesema kua Mandela alifunza watu umuhimu wa kuwasamehe wenzao, na leo ameweza kuwa huru.’’
Bofya Tiger Woods, naye ambaye ni mchezaji golfu mashuhuri zaidi duniani, alisema daima atamkumbuka Mandela.
Aliyekuwa nahodha wa timu ya Uingereza, Bofya David Beckham alisema kuwa anamlilia sana Mandela na kuwa yuko pamoja na familia yake. ''Tumepoteza mtu muhimu sana na shujaa wetu,’’ Alisema Beckham.
Naye mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA, Bofya Sepp Blatter, amesema kuwa anaomboleza sana na anahisi uchungu mwingi kufuatia kifo cha Mandela.

Nelson Mandela Histori 1918-2013

Miaka ya Mapema

1952

Rolihlahla Mandela, mwanawe chifu, alizaliwa katika kijiji kimoja kiitwacho, Mvezo katika mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini tarehe 18 Julai mwaka 1918. Alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake kwenda shule. Mwalimu ambaye hata hangeweza kutaja jina lake vyema, alizoea kumuita Nelson. Alitoroka mjini Johannesburg mwaka 1941 ili kuepuka kulazimishwa kuoa mapema. Alikutana na Walter Sisulu aliyemsaidia kupata kazi katika kampuni ya ya Witkin Sidelsky na Eidelma. Pia alijiunga na chama cha (ANC)


Kesi ya Uhaini

1956

Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza ya sheria inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano na Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa uwakilishi. Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi, ANC ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha harakati zake kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958, Mandela alimuoa Winnie Madikizela.

Huru hatimaye

1990

Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka 1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De Klerk akakiondolea marufuku chama cha ANC. Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu.

Tuzo ya amani ya Nobel

1993

Mnamo mwaka 1993, Mandela na rais wa nchi hiyo wakati huo, walituzwa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi za kuleta uthabiti Afrika Kusini. Akikubali tuzo hiyo, Mandela alisema kuwa '' tutafanya kila tuwezalo kuweza kuleta mageuzi duniani.''

Rais mpya

1994

Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa kidemokrasia. Mandela alichaguliwa. Akihutubia umma, katika sherehe ya kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: "uhuru utawale, Mungu aibariki Afrika!'' Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa nyumba za kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea kuongezeka.Thabo Mbeki alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza sera za nchi hiyo kimataifa.


Akitoka Robbben

1995

Kuadhimisha miaka mitano baada ya kuachiliwa kwake, Nelson Mandela alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa kwa miaka 18. Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na wafungwa wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu. Mapafu ya Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi katika machimbo ya mawe.

Usiniite''

2004

Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama kiongozi wa chama tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka 1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa na miaka 80. Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo kuanza matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa anataka maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha aliwaambia wandishi wa habari wasimpigie simu.

Sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake

2008

Wanamuziki, waigizaji na wanasiasa waliungana na Mandela katika sherehe kubwa uwanja wa Hyde Park mjini London kusherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake. Akiongea na wale waliofika, aliwaambia, ''ni wakati kwa kizazi kipya kuchukua uongozi, kibarua kwenu sasa.''

Kuugua

2010

Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya kustaafu. Ingawa alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2010 nchini humo. Januari mwaka 2011, alilazwa hospitalini kwa ukaguzi maalum, huku serikali ikiwakumbusha watu kuwa aliwahi kupata matatizo ya kupumua. Alipokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu mwaka 2012 na pia mwaka 2013 .

Mtunis:Kufungia Mwaka 2013 na Who`s Bad

Mtayarishaji na Muigizaji wa filamu za kiswahili nchini Tanzania Nice Mohamed ‘Mtunis’pichani amesema kwamba filamu yake ya Who’s Bad itakuwa kazi yake ya kufungia mwaka  2013 kwa kuzima kazi nyingine za filamu zilizoingia pamoja na filamu hiyo ambayo inafanya vizuri sokoni baada ya kuingia mitaani hivi karibuni.

“Kama ambavyo wengi wamenizoea ninapotoa kazi inakuwa ni bora na lazima ikimbize sokoni, sinema yangu ya Who’s Bad itafunga mwaka kama kazi bora nakuwa makini sana katika utengenezaji wa filamu na ndio kilichofanyika katika filamu hiyo wasanii wamekamua sana na kuonyesho uwezo wa hali ya juu,”anasema Nice.

Filamu hiyo imeshirikisha wasanii kama Patcho Mwamba na washiriki wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu, Mtunis amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kazi alizofanya ni kama Bar mead, Who’s Bad,Clinic Love na kusambazwa na kampuni ya Steps Entertainment.


 

Mandela hoi Kitandani



Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela
Rais wa kwanza mwaafrika wa Afrika Kusini, Nelson Mandela anaendelea kupambana na ugonjwa akiwa bado kitandani, binti yake Makaziwe Mandela amesema.
Bi Makaziwe ameliambia Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC kuwa mpinzani huyo wa siasa za ubaguzi wa rangi, "bado yupo nasi, imara, na anatia moyo".
"Hata kwa kukosa neno zuri zaidi... Akiwa bado kitandani anatufundisha somo la subira, upendo, uvumilivu," amesema, Makaziwe.

Special Introductory Fare from Dar es salaam to Morogoro



ONE WAY Tshs 99,000 (all inclusive)
RETURN Tshs 160,000 (all inclusive)

DAILY DEPARTURES

Book now to get the special fare !!

For more information, calls us on 0783 233334

Or Email to auric@auricair.com

"ENJOY THE WORLD OF FLYING - SAFARI"
Photo: Special Introductory Fare from Dar es salaam to Morogoro

ONE WAY  Tshs 99,000 (all inclusive)
RETURN  Tshs 160,000 (all inclusive)

DAILY DEPARTURES

Book now to get the special fare !!

For more information, calls us on 0783 233334

Or Email to auric@auricair.com

"ENJOY THE WORLD OF FLYING - SAFARI"

Mombasa wamsubiri Diamond

Mashabiki wa wapenzi wa mziki kizazi kipya wa jijini Mombasa jumamosi hiii tarehe 7,Desemba,2013 wanamsubiria Diamond Platinium pichani kushoto , ambaya atakae fanya shoo ya kufa mtu katika ukumbi wa Big Tree Hotel. Siku hiyo shoo itakuwa siya kukosa kwa sababu msanii Diamond Platinium kutoka Tanzania atawapa masongi ya ukweli kama `my number one`,`nataka kulewa`,`mbagala` na nyinginezo nyingi hhii si ya kukosa wana Mombasa

Waziri wa Kilimo wa ashinda tuzo ya Forbes


Akinwumi Adesina, waziri wa kilimo Nigeria
Waziri wa Kilimo wa Nigeria Akinwumi Adesina ametangazwa na jarida la Forbes Afrika kuwa mshindi wa mwaka kutokana na mageuzi yake katika sekta ya kilimo.
"Ni mtu ambaye yuko katika mwelekeo wa kuisaidia Afrika kujilisha," amesema mhariri wa Forbes Africa,Chris Bishop.
Bwana Adesina amesema anataka kuwasaidia watu kutajirika kupitia kilimo.

Dr. Migiro ateuliwa kuwa Mbunge!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dokta Asha-Rose Migiro, aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dokta. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza Desemba 2, 2013. Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.

'Kura ya Ballon d'Or ngumu ngumu zaidi'

Michel Platini


Rais wa Uefa Michel Platini amesema shughuli ya kuchagua nani kati ya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck Ribery atatunukiwa Ballon d'Or "ndiyo ngumu zaidi katika historia ya tuzo hiyo."

Katika mahojianio na gazeti la michezo la kila siku Uhispania la AS, mshindi huyo mara tatu wa Ballon d'Or winner kutoka Ufaransa alifanyia mzaha uamuzi wa Fifa wa kusongesha siku ya mwisho ya kupiga kura kwa wiki mbili hadi Novemba 29

Alisema “hili lilifanyika ili kuingiana na Ureno kufika fainali za Kombe la Dunia kupitia mabao matatu ya Ronaldo."
Platini anasema Andres Iniesta au Xavi Hernandez wangemshinda Messi kwa tuzo hiyo ya 2010 baada ya kusaidia Uhispania kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa nchini Afrika Kusini.
Mshindi wa Ballon d'Or will atatangazwa Januari 13.

GOtv Cecafa Cup:Tanzania marches to quarters

Tanzania's mainland national team The Kilimanjaro Stars have sealed their place in the quarterfinals of the Cecafa Senior Challenge Cup following their 1-0 victory over Burundi to a match played at the Afraha Stadium in Nakuru. TP Mazembe duo of Mbwana Samatta and Thomas Ulimwengu marked their first appearances in the tournament following their return from club duties.
In form striker Mbwana Samatta connected a well curled cross from Mrisho Ngassa with a solid header to score the only goal of the game in the eighth minute.
With this result, Stars finish with a total of seven points from two wins and a draw as they march on to the quarters.


Line ups:
Kilimanjaro Stars: Ivo Mapunda, Kevin Yondani (c), Erasto Nyoni, Himid Mao, Said Moradi, Frank Domayo, Salum Abubakar 'Sureboy', Mrisho Ngassa, Thomas Ulimwengu, Amri Kiemba, Mbwana Samatta.
Burundi: Arthur Arakaza, Hassan Hakizimana(c), Frederic Nsabiyumva, Rashid Harerimana, Yussuf Ndikumana, Christopher Nduwarugira, Gael Duhayinoavyi, Celestin Habonimana, Shaban Hussein, Jean